Hakimu mkazi au resident magistrate ni nani?

Watu kama mtihani 90 percent mngefeli, swali liko wazi kwa nn iitwe mahakama ya hakimu mkaazi? Unataja kazi zake, mara level yake halafu unalalamika necta wanapendelea.
 
Watu kama mtihani 90 percent mngefeli, swali liko wazi kwa nn iitwe mahakama ya hakimu mkaazi? Unataja kazi zake, mara level yake halafu unalalamika necta wanapendelea.
Watu wanapuyanga tu mkuu
 
Asante kwa ufafanuzi mkuu
 
Yule hakimu wake anaishi ndani ya jengo hilo la mahakama,
ndo maana inaitwa mahakama ya makazi kisutu,
yaani mahakama ya hakimu mkaaji wa mule mule ndani ya mahakama ya kisutu
Aisee
 
Nimekupata vyema mkuu naomba niswalishe nami kidogo juu ya
kazi za hawa ni zipi mahakamani?
1.KARANI
2.WAKILI
3.PP

Natamani sana kujua kazi zao na pia elimu zao.

Karibu mkuu..
Hapo ni sawa na unauwa mbu kwa rungu kwenye kichwa cha mtoto mchanga
 
Kwa hakimu mkazi kuhusu kesi kuendeshwa na majaji tuu ni uongo.Andy Lyamuya alikuwa jaji lini? Mahskimu hspa huitwa wakazi na mkuu wao ni principal resident magistrate yaani hakimu mkazi kiongozi.
Aisee
 
Shukrani mkuu
 
Hakuna kitu kama mahakama ya mkoa kwenye mfumo wa sheria zetu. Mfumo wa mahakama unaanzia 1. Mahakama ya Mwanzo. 2. Mahakama ya Wilaya. 3.Mahakama ya Hakimu Mkazi. 4.Mahakama Kuu, na 4. Mahakama ya Rufaa.
Zamani zile kulikuwa na somo tulikuwa tunafundishwa lilikuwa linaitwa siasa, mwalimu wetu alikuwa anaitwa Rugimbi mashoto a.k.a iskariote, alikuwa anaandika mahakama za mkoa/mahakama za hakimu mkazi
 
hivi ni nini tofauti ya mahakama ya hakimu mkazi na mahakama ya wilaya?
 
Mpaka sasa mahakimu wakazi wako mahakama za mwanzo ila wameweka critelia lazima awe kafaulu lawschool
 
Hakimu mkazi ni hakimu ambaye anasikiliza kesi katika mahakama ya hakimu mkazi, mahakama hii ni sehemu ya aina tano za mahakama katika mfumo wa mahakama hapa Tanzania yaani 1. mahakama ya mwanzo, 2. mahakama ya wilaya 3. mahakama ya hakimu mkazi 4. mahakama kuu na 5. ni mahakama ya rufani. Jina hakimu mkazi haina maana kwamba hakimu huyo anaishi katika jengo la mahakama hiyo kama wachangiaji wengine walivyochangia.
Tembelea Войдите на Facebook
View attachment 2364169
 
Maelezo Mengi lakini bado hujajibu
Swali la mdau.
 
Sio swali rahisi, wengi hawajui.

Lisu katoa ufafanuzi wa kihistoria kwamba huyu ni hakimu/jaji aliyekuwa anaishi eneo la mahakama enzi za ukoloni kushughulika na kesi za dharura muda wote.
Hili swali linapaswa kujibiwa na mtu yeyote aliyesoma Civics Form Two na kuendelea. Kabla yakukujibu naomba kujua wewe umefikia level ipi ya elimu? Kama umevuka form two basi kuna shida kwenye mfumo wa elimu yetu.
 
Kwa nini anaishi ndani ya jengo la mahakama?
Yule hakimu wake anaishi ndani ya jengo hilo la mahakama,
ndo maana inaitwa mahakama ya makazi kisutu,
yaani mahakama ya hakimu mkaaji wa mule mule ndani ya mahakama ya kisutu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…