Hakukuwa na sababu ya Profesa Mkenda kuzungumza aliyoyazungumza hadharani. Kiongozi ni kuwa na Kifua na Uvumilivu

Wewe Jamaa ni Mpumbavu Sana tu, Yaani katika Wajinga Wewe ndio umeshika Mpini, Unataka kutuambia kitu Gani? Wewe na Professor Mkenda Nani Mwenye Akili Zaidi? Chawa JUNYA Mkubwa weeee+ Ndigiri
Kwani unafahamu kiwango changu cha akili? Inaonyesha wewe ni mgonjwa wa akili
 
..nashauri ukasikilize hotuba ya Prof.Mkenda.

..Prof.Mkenda kamsifia Raisi katika hotuba nzima nyinyi mnasema kamshutumu!?

..Prof.Mkenda kasema huko mitaani anasifiwa kwa maamuzi ambayo Raisi ndio ameyafanya.

..Ninachokiona hapa ni nguvu ya social media kuupotosha umma.
Nimeisikiliza hotuba ya Mkenda, kama ilivyokawaida ya Hawa wanasiasa uchwara kazi yao ni kujipendekeza kwa wakubwa and Mkenda is no exception!
At issue katika hotuba yake ni ile lazima kuelezea hadharani kuwa wasaidizi wa Rais walikuwa wanawazuia kumuona Rais!! Alitaka kupeleka ujumbe gani kuhusu uhusiano wa Rais na wasaidizi wake vis a vis some members of the cabinet?
To me Mkenda has shown that he is not a team player hence he is a liability to the government.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Sote tumeyasikia maneno na kauli za Waziri wa Elimu Mheshimiwa Profesa Adolph Mkenda akilalamika kuwa alizungushwa kupata nafasi ya kuonana na Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Mimi Mwashambwa nimejiuliza maswali ya je kulikuwa na sababu zipi za kuyaongea hayo masuala hadharani? Yalikuwa na umuhimu upi na sababu zipi? Alishindwa nini kuyaongea faragha alipopata nafasi ya kuongea na kuonana na Mheshimiwa Rais?

Je waziri hana njia nyingine za kuwasiliana na kufikisha ujumbe wake kwa Rais? Je waziri hawezi kuwasilisha jambo hilo kwenye kikao cha Baraza la mawaziri na kutoa dukuduku lake na kero yake ili mambo yazungumzwe na kuonyana humo humo badala ya kuleta hadharani?

Pia soma:
Juu ya Waziri Wa Elimu kuna Naibu Waziri Mkuu, Waziri Mkuu ,Makamu wa Rais kabla ya kumfikia Rais Mwenyewe. Sasa kwanini asingemtumia hata mmoja wapo kati ya hao kupeleka jambo lake na kero yake hiyo?

Hata alipopelekewa kikaratasi mezani kwake kwanini na kulikuwa na sababu gani ya kujibu kwa jeuri kuwa yale aliyokuwa anayaongea yalikuwa ni Sehemu ya hotuba yake? Kwanini alikuwa anaonyesha kana kwamba yupo kwenye mgogoro na wasaidizi wa Rais na sasa anataka kuwachongea na kutunishiana misuli hadharani? Yalikuwa na sababu gani hadi ya kusema kuwa tuliambiwa tuongee kwa saa mbili tu?

Kwanini Waziri ambaye ni Profesa kabisa anakosa kifua na uvumilivu pamoja na subira ya mambo madogo kama hayo? Kama jambo dogo kama hilo linamshinda kuvumilia na kukaa kimya bila kuonyesha hasira zake hadharani,anaweza vipi vumilia mambo makubwa na kukaa nayo mpaka anaingia kaburini? Unapokuwa kiongozi mkubwa ni pamoja na kubeba maumivu na kutunza siri kwa gharama kubwa na Maumivu.

Hivi kama Rais Samia Mama yetu kipenzi asingekuwa na kifua na uvumilivu na kuamua kuzungumza kila kitu hadharani. Unafikiri angezungumza mangapi mazito baada ya kuapishwa kwake kuwa Rais? Au mmesahau ni nini Mkuu wa Majeshi wetu mstaafu Mheshimiwa Jenerali Venance Mabeyo alichokisema na kilichotokea baada ya kifo cha Hayati Mwalimu Daktari John Pombe Joseph Magufuli?

Mmesahau Kauli ya Jenerali Mabeyo kuwa kuna watu walisahau katiba inasema nini na kwamba akawakumbusha Matakwa ya Katiba mara baada ya kufa kwa Rais? Hivi mnaichukuliaje kauli hiyo? Mnaelewa Maana yake? Mnataka niwafungulie mabano ili muelewe?

Je mnafikiri watu hao waliosahau matakwa ya katiba Hawapo hai? Mnafikiri hawapo Tanzania? Mnafikiri hawapo serikalini?? Mnafikiri Mama yetu Mpendwa hawafahamu? Mnafikiri Mama yetu kipenzi hafahamu kilichotokea baada ya kifo cha Hayati? Au mnafikiri amekaa kimya kwa sababu hajui kitu?

Jibu ni kuwa anafahamu kila kitu na ameamua kukaa kimya na kuendelea na kazi kwa sababu anajua maana ya uongozi. anajua maana ya kutunza siri. Anajua Ukubwa ni jalala. Anajua jambo gani linapaswa kuzungumzwa hadharani na lipi halipaswi kuzungumzwa hadharani. Anajua kuna mambo yanapaswa kukaa kifuani na kubakia kama siri mpaka Kifo.

Na huo ndio uongozi. Ndio Ukubwa.Ndio uongozi unavyotaka hivyo kwa kiongozi wa juu kuwa na kifua ,kutunza siri,kuwa na subira, uvumilivu na kujizuia kuongea vitu kwa msukumo wa hasira,jazba, mihemuko na kukurupuka. Kama Rais Samia angetaka kuongea kila kitu hadharani basi Nchi ingesimama. Nasema tena kuwa NCHI ingesimama hii.

Viongozi wetu jifunzeni kuwa na siri,vifua, uvumilivu na subira. Tumieni busara na hekima katika kuzungumza hadharani na chagueni maneno ya kuzungumza mbele ya hadhira. Na ikiwezekana someni hotuba mlizoandaliwa kuliko kutumia hisia bila mantiki kuzungumza na kujikuta mkiharibu na kuleta taswira mbaya kwa jamii .

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kwa hiyo unaona ni sawa huyo Rajabu akitukana mawaziri wanaomsaidia rais? Wakati mwingine ni vizuri ukifikiria kwa kutumia ubongo kuliko kutumia tumbo lako. Wewe Mwashamba kweli, kwa hiyo akinyamaza ingekusaidia nini? Bado una ile mentality ya kijamaa ya kuficha ficha vitu.
 
Umesema ukweli mchungu kabisa
 
Kwa hiyo unaona ni sawa huyo Rajabu akitukana mawaziri wanaomsaidia rais? Wakati mwingine ni vizuri ukifikiria kwa kutumia ubongo kuliko kutumia tumbo lako. Wewe Mwashamba kweli, kwa hiyo akinyamaza ingekusaidia nini? Bado una ile mentality ya kijamaa ya kuficha ficha vitu.
Nani aliyetukanwa?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Sote tumeyasikia maneno na kauli za Waziri wa Elimu Mheshimiwa Profesa Adolph Mkenda akilalamika kuwa alizungushwa kupata nafasi ya kuonana na Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Mimi Mwashambwa nimejiuliza maswali ya je kulikuwa na sababu zipi za kuyaongea hayo masuala hadharani? Yalikuwa na umuhimu upi na sababu zipi? Alishindwa nini kuyaongea faragha alipopata nafasi ya kuongea na kuonana na Mheshimiwa Rais?

Je waziri hana njia nyingine za kuwasiliana na kufikisha ujumbe wake kwa Rais? Je waziri hawezi kuwasilisha jambo hilo kwenye kikao cha Baraza la mawaziri na kutoa dukuduku lake na kero yake ili mambo yazungumzwe na kuonyana humo humo badala ya kuleta hadharani?

Pia soma:
Juu ya Waziri Wa Elimu kuna Naibu Waziri Mkuu, Waziri Mkuu ,Makamu wa Rais kabla ya kumfikia Rais Mwenyewe. Sasa kwanini asingemtumia hata mmoja wapo kati ya hao kupeleka jambo lake na kero yake hiyo?

Hata alipopelekewa kikaratasi mezani kwake kwanini na kulikuwa na sababu gani ya kujibu kwa jeuri kuwa yale aliyokuwa anayaongea yalikuwa ni Sehemu ya hotuba yake? Kwanini alikuwa anaonyesha kana kwamba yupo kwenye mgogoro na wasaidizi wa Rais na sasa anataka kuwachongea na kutunishiana misuli hadharani? Yalikuwa na sababu gani hadi ya kusema kuwa tuliambiwa tuongee kwa saa mbili tu?

Kwanini Waziri ambaye ni Profesa kabisa anakosa kifua na uvumilivu pamoja na subira ya mambo madogo kama hayo? Kama jambo dogo kama hilo linamshinda kuvumilia na kukaa kimya bila kuonyesha hasira zake hadharani,anaweza vipi vumilia mambo makubwa na kukaa nayo mpaka anaingia kaburini? Unapokuwa kiongozi mkubwa ni pamoja na kubeba maumivu na kutunza siri kwa gharama kubwa na Maumivu.

Hivi kama Rais Samia Mama yetu kipenzi asingekuwa na kifua na uvumilivu na kuamua kuzungumza kila kitu hadharani. Unafikiri angezungumza mangapi mazito baada ya kuapishwa kwake kuwa Rais? Au mmesahau ni nini Mkuu wa Majeshi wetu mstaafu Mheshimiwa Jenerali Venance Mabeyo alichokisema na kilichotokea baada ya kifo cha Hayati Mwalimu Daktari John Pombe Joseph Magufuli?

Mmesahau Kauli ya Jenerali Mabeyo kuwa kuna watu walisahau katiba inasema nini na kwamba akawakumbusha Matakwa ya Katiba mara baada ya kufa kwa Rais? Hivi mnaichukuliaje kauli hiyo? Mnaelewa Maana yake? Mnataka niwafungulie mabano ili muelewe?

Je mnafikiri watu hao waliosahau matakwa ya katiba Hawapo hai? Mnafikiri hawapo Tanzania? Mnafikiri hawapo serikalini?? Mnafikiri Mama yetu Mpendwa hawafahamu? Mnafikiri Mama yetu kipenzi hafahamu kilichotokea baada ya kifo cha Hayati? Au mnafikiri amekaa kimya kwa sababu hajui kitu?

Jibu ni kuwa anafahamu kila kitu na ameamua kukaa kimya na kuendelea na kazi kwa sababu anajua maana ya uongozi. anajua maana ya kutunza siri. Anajua Ukubwa ni jalala. Anajua jambo gani linapaswa kuzungumzwa hadharani na lipi halipaswi kuzungumzwa hadharani. Anajua kuna mambo yanapaswa kukaa kifuani na kubakia kama siri mpaka Kifo.

Na huo ndio uongozi. Ndio Ukubwa.Ndio uongozi unavyotaka hivyo kwa kiongozi wa juu kuwa na kifua ,kutunza siri,kuwa na subira, uvumilivu na kujizuia kuongea vitu kwa msukumo wa hasira,jazba, mihemuko na kukurupuka. Kama Rais Samia angetaka kuongea kila kitu hadharani basi Nchi ingesimama. Nasema tena kuwa NCHI ingesimama hii.

Viongozi wetu jifunzeni kuwa na siri,vifua, uvumilivu na subira. Tumieni busara na hekima katika kuzungumza hadharani na chagueni maneno ya kuzungumza mbele ya hadhira. Na ikiwezekana someni hotuba mlizoandaliwa kuliko kutumia hisia bila mantiki kuzungumza na kujikuta mkiharibu na kuleta taswira mbaya kwa jamii .

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Ukiona ivyo ujuwe tabia izo zimekuwa kero kupitiliza, wasomi wa aina ya Prof Mkenda huwa wamenyooka sana
 
Hakukuwa na haja ya kusema "..Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan"
 
Ungekuwa umewahi kuwa kiongozi wa ngazi yoyote ile ungeelewa hiki nilicho kiandika hapa
Uzuri silikwa urefu wa kamba na siko tayari kula kwa urefu wa kamba,wala kwa kichaka cha uchawa kwa wala kwa urefu wa kamba.
 
Nimeisikiliza hotuba ya Mkenda, kama ilivyokawaida ya Hawa wanasiasa uchwara kazi yao ni kujipendekeza kwa wakubwa and Mkenda is no exception!
At issue katika hotuba yake ni ile lazima kuelezea hadharani kuwa wasaidizi wa Rais walikuwa wanawazuia kumuona Rais!! Alitaka kupeleka ujumbe gani kuhusu uhusiano wa Rais na wasaidizi wake vis a vis some members of the cabinet?
To me Mkenda has shown that he is not a team player hence he is a liability to the government.
... Nakubaliana na wewe. Amefanya jambo la hovyo sana kama Kiongozi
 
Back
Top Bottom