Hakukuwa na sababu ya Profesa Mkenda kuzungumza aliyoyazungumza hadharani. Kiongozi ni kuwa na Kifua na Uvumilivu

Kila kitu kina utaratibu wake ambao hata Mheshimiwa waziri anaufahamu. Lakini fahamu ya Kuwa waziri ana njia nyingi sana za kuwasiliana moja kwa moja na Mheshimiwa Rais
Si inasemekana mapete anazuia watu wasimfikie mama au?? Maria huyoo siteai
 
We komredi Mwamshamba ndio ujue kama waziri kumpata Rais imekua mbilinge mbilinge hivyo unafikiri ni picha nzuri hiyo? Usitetee kila kitu ili mradi una maslahi yako na safari hii tunakupeleka GOMA tunakuja kukukamata hapo hapo kwa shemeji yako Gomaaaa moja ukamfanyie na Uchawa yule madevu wa Congo sijuii Kanali Nangaa yule uone🤣
 
Huu ujinga wa kutaka kuficha kila kitu ndo unaharibu utaratibu wa nchi
 
😀😀Embu acha utani wako hapa. Tangia lini mimi nikakaa kwa mashemeji.
 
Ujumbe hapo ni kwamba Waziri hana imani na rais pia, kamshitaki kwa wananchi. Siku mambo yakiharibika wananchi wajue kuwa waziri hakuwa hata na access na rais.

Huelewi wapi?
 
He will talk January language it's only a time
 
Yaani Steve Nyerere na Shilole wana nguvu kuliko PM, uliona wapi huu upuuzi?
Naona umechanganyikiwa kabisa siku hizi na kuanza kuandika ujinga kinga tu. Shilole ni nani na ana nafasi gani ya uongozi mpaka useme yupo huu ya waziri Mkuu? Umewahi kuona huyo Shilole akitoa hotuba kabla ya waziri Mkuu au kiongozi yeyote yule? Huyo Shilole ana cheo gani cha kiserikali?
 
Ujumbe hapo ni kwamba Waziri hana imani na rais pia, kamshitaki kwa wananchi. Siku mambo yakiharibika wananchi wajue kuwa waziri hakuwa hata na access na rais.

Huelewi wapi?
Siyo kweli. Unakumbuka kuna siku Rais alieleza namna ambavyo Mheshimiwa Waziri wa Fedha alivyokuwa akimpigia simu Mheshimiwa Rais kumueleza baadhi ya mambo? Huoni kuwa hapo inaonyesha wazi kuwa waziri anaweza hata kumpigia simu Mheshimiwa Rais?
 
Kauli yake inadhihirisha kuwa Kuna shida kubwa sana kwenye serikali hivi sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…