Ndugu yangu nakukaribisha usome Quran kwani ina majibu yote ya maisha ya hapa duniani na huko tunakokwenda baada ya kufa. Usisubiri mpaka ufe ili ujue kama ni kweli au laa kwa sababu it will be too late. Its now or never. Majuto baada ya kifo huwa ni makubwa sana
QURAN 23: 99-116
99. Mpaka yanapo mfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe (tena duniani)
100. Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyo yaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi (hawezi kurudi duniani) mpaka siku watapo fufuliwa.
101. Basi litapo pulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana.
102. Ama wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio wenye kufanikiwa.
103. Na wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio walio zitia hasarani nafsi zao, na katika Jahanamu watadumu.
104. Moto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizo kunjana.
105. Je! Hazikuwa Aya zangu mkisomewa, na nyinyi mkizikanusha?
106. Watasema: Mola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tulio potea.
107. Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni (uturudishe tena duniani) Na kama tukifanya tena maasi basi kweli sisi ni wenye kudhulumu.
108. Atasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala msinisemeze.
109. Bila ya shaka lilikuwapo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanao rehemu.
110. Lakini nyinyi mliwakejeli hata wakakusahaulisheni kunikumbuka, na mlikuwa mkiwacheka.
111. Hakika Mimi leo nimewalipa kwa vile walivyo subiri. Bila ya shaka hao ndio wenye kufuzu.
112. Atasema: (Mwenyezi Mungu) Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hisabu ya miaka?
113. Watasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku (haitimii siku kamili). Basi waulize wanao weka hisabu.
114. Atasema: Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo tu, laiti ingeli kuwa mnajua.
115. Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure tu, na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?
116. Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi Tukufu.