Hakuna cha hujuma, Yanga wapo serious na wanamaanisha kazi kazi

Kazi kweli ndo maana lucy aymel alituita nyani mashabiki wa Tanzania leo hapa kila mtu anakubali yanga team bora kisa kamfunga simba siku yanga akija kufungwa ndo utajua kwa nini wazungu wanatuona hatuna akili maana tunasahau haraka sana.
Kazi kweli na ndio maana Rage alituita mbumbumbu,tatizo letu sisi mashabiki wa majeneza tulijiona kuwa timu ni Bora baada ya kuwafunga st George.

Halafu hatutaki kuwapa utopolo heshima Yao. Wamemaliza ligi unbeaten wamechukua vikombe vyote sisi tukiambulia kikombe Cha mapinduzi masikini. Halafu Leo hii tunaanza kuwakashfu kwenye media? Sisi Majeneza hatujielewi kabisa
 
Duuu! Wewe na hao washabiki wa simba wote akili zenu sawa, yaani mchezaji kupigwa tobo ndio unaona kuna kiashilia cha rushwa?
 
Duuu! Wewe na hao washabiki wa simba wote akili zenu sawa, yaani mchezaji kupigwa tobo ndio unaona kuna kiashilia cha rushwa?
We umesoma comment yangu vizuri au wanzuki ya Jana haijakuisha kichwani?
 
You said it all.
 
👏👏👏👏 Umeongea kiufundi Sana na kimpira aswaaa, Sasa hivi yanga wanachokifanya ni kuwaonyesha kwa vitendo kwamba wako vizuri sana kuanzia ndani ya uwanja mpaka nje ya uwanja, habari za propaganda za kina babra na Ahmed Ally wamewaachia wao waendelee nazo lakini wao wameinvest uwanjani, unapobisha unajibiwa uwanjani full stop!
 
Mo na babra uwa wanawadanganya wachezaji wanaosajiliwa na Yanga ni wa mkopo na wanaamini
 
Kocha ambaye hajashinda hata mechi moja ya kimataifa sasa kati ya simba na yanga nani haipi uzito derby kama sio simba ile derby ya ligi kuu simba alicheza akiwa kapumnzika siku mbili toka alipocheza kimataifa ila nyinyi mwezi mzima mnajiandaa wazee wa simba wameamua kuizarau yanga hawaipi kipaombele tena haiwezekani team imfunge al ahly na Kaizer chief waje wafungwe na wavuvi wa kigamboni think twice na hapo ndo mwisho wenu wa kujifariji subirini mcheze mechi mbili za kimataifa mrudi kigamboni mkacheze na friends rangers.
 

Una feli kaka. Endelea kuamini Hivyo , ukija kustuka hata nafasi ya 3 utaikosa
 
Sasa mbona mnalialia
 
Hizi ndio akili za MBUMBUMBU sasa.
 
Kazi kweli ndo maana lucy aymel alituita nyani mashabiki wa Tanzania leo hapa kila mtu anakubali yanga team bora kisa kamfunga simba siku yanga akija kufungwa ndo utajua kwa nini wazungu wanatuona hatuna akili maana tunasahau haraka sana.
Punguza kuwapapatikia Wazungu. Haohao Wazungu wako wana misemo:
  • History is written by victors.
  • He who laughs last, laughs best!
 
This time ligi ni ngumu

Simba ajiangalie. SINGUDA BIG STARS HATARI FIRE
 
Unapodili na waswahili, utawaonyesha njia wanakudhihaki. Siku moja wakitumia njia yako wanakudharau na kukusema kuwa haujui unachokifanya. Yanga mna uswahili mwingi.
 
Hilo ni kweli na mimi nimelisema hapa juzi juzi. Simba wanajua umuhimu wa kuishinda Yanga hasa kwa mashabiki wake ila hawaichukulii mechi hiyo kwa uzitooo sana kama zamani. Huu ndiyo ukweli. Mtazamo na malengo yao ni mengine kwa sasa. Yanga bado wanaikamia Simba halafu wanaenda kusumbuliwa na timu kama Polisi.
 
Kazi kweli ndo maana lucy aymel alituita nyani mashabiki wa Tanzania leo hapa kila mtu anakubali yanga team bora kisa kamfunga simba siku yanga akija kufungwa ndo utajua kwa nini wazungu wanatuona hatuna akili maana tunasahau haraka sana.
This is another Gorilla. Maelezo yote hayo umeona Yanga kumfunga Simba tu?
 

Maelezo yako yamekosa mantiki pale uliposema kwenye Ligi Simba hajamfunga Yanga, kwa hiyo kipimo chako ni Simba kutomfunga Yanga kwa sababu ya nguvu kubwa ambazo Yanga hutumia dhidi ya Simba, na hilo limefhihirika huko nyuma ambapo Simba imechukua vikombe vyote lakini haikuifunga Yanga labda mara chache kama zile 4-1 msimu fulani kama miwili au mitatu iliyopita. Kiubora Yanga wamejitahidi, lakini makosa ya mechi ya juzi huwez kusema Simba ni mbovu kiivyo dhidi ya Yanga. Chemistry ya Simba haijapata muunganiko, wakati Yanga ni kikosi cha msimu uliopita na nyongeza kiasi ya wachezaji huku Mwalim akiwa ni Nabi ambaye amekua na team kwa misimu mitatu sasa, ambapo hata Nabi mwanzoni wakati anaingia Yanga alikua wa kawaida sana, sema baada ya muda anawnza kuonekana.
Yote kwa yote, Yanga anakamia lakini anafungika vizuri kabisa. Jana kashinda 2-1 dhidi ya polisi, hiyo inakupa picha anafungika vizuri tu! Huo uzuri unaotajwa hapa ni kukuza jambo bila kuakisi uhalisia.

Ni kweli kibongobongo Yanga ya sasa ime improve, lakini haitishi kabisa! Hivi magoli yale mepesi waliyofungwa Simba ni kwa sababu Yanga ni bora sana? Ni big No, ni kwa sababu ya makosa katika mchezo. Yanga wanapata kuongea kwa sababu ya makosa ambayo Simba waliyafanya kipindi cha pili. Lakini pia team ya Yanga, bado iko na uswahili mwingi sana, angalia geti walilotumia kupita wakati wanaingia uwanjani, purely un professional. Kimataifa sijui watafanya hivyo? Simba ijiepushe na mambo ya namna hii ya hovyo.
Kando ya hapo, hata wakati Simba ikiwa bora ilishafungwa na Kagera sugar pale Taifa, imefungwa na Prison kule Mbeya nk. Kufungwa ni mchezo, lakini hata ukifanya tathmini, mechi za ngao ya jamii bado ni kama Pre Season, team bado haziwi timamu( fitness).
Kwa hiyo, hoja yako imekaa kishabiki zaidi badala ya Critical Scientific Analysis.
 
Hakuna hoja ya kishabiki hapo huo wote ni ukweli, kwani Kuna mtu asiyejua kuwa makosa tena madogo kabisa ndo yanaghalim team.?
Kosa lako ndo goli la mwenzio na Kila mahali iko hvyo..
Tuje kwenye magoli, naona umejifanya kuya-undermine magoli waliyofungwa Makolo ni dhaifu Sawa, Sasa team kubwa kama Simba inakuwaje inaruhusu kufungwa magoli dhaifu tena yakianza kupita kwenye matobo ya wachezaji...Halafu kama mmeona kuruka ukuta kwa Yanga kunawanufaisha nanyi si Mruke ili mshinde kama Mlivyowasha moto kule SA na bado mkala za Uso.

Tukutane tena kwenye Ligi tar 23 October Ila Suala la kuifunga Yanga msahau miaka hii, Hadi Mama anaachia hii nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…