Hakuna cha Kamera, wala ushirikina - Polisi


Machozi yanakutoka. Ubaya zaidi ni kwamba ni shida ambazo zinaweza kuepukika! Kuna baadhi ya watu wanasema watu wajiendeleze wenyewe, ila wanasahau Nchi ni tajiri sana na kama viongozi walikuwa wanajua cha kufanya na kukifanya mambo yangekuwa tofauti kabisa.

Ila ni hao viongozi ambao hawana hata aibu ya kuweka mabillioni huko Jersey na halafu wanapishana na hawa binadamu wenzao wanaotaabika barabarani kila siku. Hata wizi ungekuwa kwenye damu, ndio waibe kiasi hicho?
 
Haya kweli ni mambo!!!!!! Hii ni vunja mbavu, pamoja na kuwa implication yake ni kubwa kwa taifa letu. Mimi nadhani Spika amepigwa chenga ya mwili. Anahitaji support yetu. Hapa wote tumefungwa la kisigino, lakini nasisi tumemfunga la kisigino Rostam na KKKT. Mapambano yanaendelea
 
Spika asingekuwa taahira kupeleka police ''NOTHING''. Wana maana ni mwehu!
 
1. Chiligati awe na la kujibu kwa kutudanganya kuwa kuna matu alikuwa anatafuta kwa kukaa, na pia atueleze alionaje? maana camera hazikuona hicho kitendo,

2. watuambie huo unga waliutoa wapi, na kwa nini waliupima wakati hakuna aliengia ndani ya bunge kutafuta kiti wala kumwaga unga?

3. Wote watueleze kwanini lakini wanatufanya sisi wajinga kiasi hicho? yaani haya ni matusi tena ya nguoni kwa wananchi wote!!!!

samahanini kwa lugha mbaya, nimeudhika mno
 
I smell something fishy here..my poor country TZ where are you heading to??
Inauma sana tunaposoma uozo na aibu za chama tawala siku hadi siku.
 
Tunataka MOTIVE!
KWANINI UNGA ULIKUWA BUNGENI NA KWANINI ULIPELEKWA KWA MKEMIA NA TUNATAKA KAULI ZA WALIOHOJIWA!
POLISI WASEME WALITUMIA VIGEZO GANI KUFIKIA CONCLUSION!
ACHENI HIZO BANA!

Mhhh!!!!!!!!!!
 

Good/hard questions!
More questions than answers...
 

Hii ni aibu sana, ila naamini MWISHO WA UBAYA AIBU
 
Nimewaambia tukubali hamtaki nyie mmeng'ang'ania tu.. mnafikiri watatoa majibu tofauti na haya?
 

Je hiyo vumbi waliitoa wapi?...walifagia bunge na kukusanya vumbi?...au je waliikusanya katika sehemu(viti vya kina Mwakyembe and Co) tu?...kama hivyo ni kwa nini?

Hivi jamani si ingekuwa bora waongee uwongo uliopo karibu na ukweli?....huu ni uwongo wa ngapi tumepata kutoka vyombo vya dola?...Muungwana kama una masikio na macho ,huoni kuwa vyombo vya dola hivi vina ku undermine?....serikali yako inaonekana ni uozo?
 
Tunataka MOTIVE!
KWANINI UNGA ULIKUWA BUNGENI NA KWANINI ULIPELEKWA KWA MKEMIA NA TUNATAKA KAULI ZA WALIOHOJIWA!
POLISI WASEME WALITUMIA VIGEZO GANI KUFIKIA CONCLUSION!
ACHENI HIZO BANA!

Lakini Hata Hosea alisema mkataba wa richmond hauna hata chembe ya ufisadi
kiko wapi sasa
Wote tunajua ngoma ya kitoto siku zote huwa haikeshi
 
Meremeta ni mali ya jeshi kwa hiyo hairuhusiwi by sheria kuiongelea kwenye public!,

Sasa ni vumbi tu lililokutwa bungeni, huu ni uchunguzi wa polisi uliochukua zaidi ya mwezi mmoja!

Only in Tanzania!
 
Kwangu haya sio matokeo ya kushangaza. NI kweli ameshika dume sisi tumeshika magalasa. This guy will get away with everything, nguvu ya fedha, inasema yeye si fisadi na hakufanya lolote baya. Kama serikali inashindwa kupropve kuwa yuko guilty inawezekana siku watanzania wakafanya hivyo na wakatoa hukumu.
 
Yooote hayo yalitabiriwa hapa JF kwamba at the end of the day hakutapatikana chochote bungeni kuhusu ule unga na hata hizo video.
 
Kweli tunachekwa sana na wenetu wa nje tunaonekana ni taifa la wapumbavu. Kuna mambo ambaye ni exclusivley Tanzanian. Leo nimeeulizwa "is there anything good comes out of here?" Kusema kweli nimeshindwa kujibu, and that is when i say i am not proud of ........
 
Meremeta ni mali ya jeshi kwa hiyo hairuhusiwi by sheria kuiongelea kwenye public!,

Sasa ni vumbi tu lililokutwa bungeni, huu ni uchunguzi wa polisi uliochukua zaidi ya mwezi mmoja!

Only in Tanzania!


Mkora said:
Lakini Hata Hosea alisema mkataba wa richmond hauna hata chembe ya ufisadi
kiko wapi sasa
Wote tunajua ngoma ya kitoto siku zote huwa haikeshi .

Hebu tuangalie upande wa pili wa thumni.....inawezekana kuna njama za kuifanya serikali ya Muungwana kuwa ni mbovu?.....au ndio anatafutiwa njia ya vote of no confidence?.......huko tuendako inawezekana hizi ni harakati za impeachment?....(ni mawazo tu)
 

Kama ni Mwungana mbona amekaa kimya? Hawa ni watendaji chini yake. Amewachukulia hatua gani. Usilaumu njama. Laumu inaction ya Mwungana. He is his own worst enemy.
 

Hata hivyo nakubaliana na MT kwa msharti kuwa kabla ya wabunge wote hawajajadili MUSTAKABALI WA NCHI ESP KUHUSU RIPOTI...Taarifa zote za wabunge wote na hisa ama nafasi wanazomiliki kwenye makampuni ziwekwe wazi ili kusiwe na bias bali THE TRUTH!
 

Ukweli ni kwamba hawa jamaa wa hili kundi wana nguvu sana, ni almost serikali ndani ya serikali yetu, muungwana naye pia inaonekana kuwa either wamemizdi nguvu au yuko nao, kwa sababu haiwezekani hata Waziri Mkuu akaogopa watu ndani ya serikali ambayo yeye ndiye kinara, sasa anamuogopa nani?

Maana sio siri tena among wakuu wa taifa kuwa uamuzi wake on Meremeta, haukuwa wa kwake, kwa sababu according to the data in the private anaongea maneno mazito sana dhidi ya mafisadi, sasa iweje akija public anakuwa bubu? Anamuogopa nani? Hatuwezi kusema kuwa anamuogopa Shein,

Sasa Pinda anamuogopa nani? Hata huu uamuzi wa polisi na unga wa vumbi, hauwezi kuwa umeamuliwa bila ya kumfahamisha mapema, ndio maana umechukua karibu mwezi mzima kuutoa maana yake ni kwamba walikuwa kwanza wana-touch base zote kwanza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…