Nilipotembelea bongo mwaka 2006 niliona utofauti MKUBWA SANA na nikawa ninajiuliza maswali mengi mengi sana na nikawa sina jibu.
Nikawa nikidhani labda ni kwasababu ya majambazi kuwa wengi!
Lakini ukweli wabongo walikuwa wanatia huruma na kila mahali ukipita kama kweli una empathy basi machozi yatakutoka!
Mpaka kieleweke kama wewe ni Mbowe utakumbuka tulikutana ukiwa na Zitto nilikwenda kumcheki jamaa yangu Tumanini.
Nilikwenda Dar kubadili passport yangu lakini nikajuta kwani wenzangu walilipa dola 50 tu hapa na mimi kimbelembele changu kwenda kubadili huko Dar kilini cost laki mbili...Karibia mara nne ya original cost!
Njiani wakati narudi niliona mengi!
Hata kituo cha mafuta nilisimama kuweka mafuta na service kidogo kabla ya kurudi moshi lakini walinzi wa kituo hicho ni harassment tupu utadhani mimi si mteja na nimeenda kuomba msaada!
Na sasa hata huko Moshi askari wanaolinda hata duka ama bureau de change anageuka kuwa askari wa bara barani na kila kitu!
Yani wakipewa bunduki sasa wao ndio wenye mamlaka yasiyo na mipaka!
Mimi kwasababu nilikuwa nikiona habari za ujambazi kila siku basi nikasema labda ni haki!
Lakini sasa nimegundua kuwa tuli tafsiri vibaya ubepari!
Kwani eti sasa hata maaskari wanalinda watu binafsi kwasababu ulinzi wa mali za umma haupo tena!
Ulinzi wa mali za umma haupo tena kwasababu mali hizo za umma ziko mikononi mwa mafisadi na polisi hao njaa wanalinda mali hizo na mafisadi wake!
Ni wazi kuwa mwenye pesa ndiye mwenye kulindwa na kuamuwa nini kifanyike!
Na ubepari wa kibongo ni wa KIMAFIA!
Kwani sasa jeshi la POLISI SI LA KUWATUMIKIA WANANCHI TENA BALI MAFISADI!
NA MWENYE ULINZI NDIOYO ALIYEKO SALAMA!
MWENYE ULINZI NI MAFISADI KWANI WAMEUPORA USALAMA WA WANANCHI AMBAO NI MALI ZAO!
Machozi yanakutoka. Ubaya zaidi ni kwamba ni shida ambazo zinaweza kuepukika! Kuna baadhi ya watu wanasema watu wajiendeleze wenyewe, ila wanasahau Nchi ni tajiri sana na kama viongozi walikuwa wanajua cha kufanya na kukifanya mambo yangekuwa tofauti kabisa.
Ila ni hao viongozi ambao hawana hata aibu ya kuweka mabillioni huko Jersey na halafu wanapishana na hawa binadamu wenzao wanaotaabika barabarani kila siku. Hata wizi ungekuwa kwenye damu, ndio waibe kiasi hicho?