Hakuna chama cha upinzani Tanzania chenye uwezo wa kusimamisha mgombea kila Jimbo, Kata, Kijiji, Mtaa

Hakuna chama cha upinzani Tanzania chenye uwezo wa kusimamisha mgombea kila Jimbo, Kata, Kijiji, Mtaa

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,505
Reaction score
16,006
Ndugu zangu,

Namba hazidanganyi. Si CHADEMA, ACT, CUF wala chama chochote hapa Tanzania kinachoweza kusimamisha mgombea kila jimbo, kata, kijiji, mtaa. Vyama vyote hivyo vinafanya kazi mijini au kwenye sehemu ambayo viongozi wao wamezalizaliwa au dini ya viongozi wao. Mfano: Chadema ipo Hai, ACT ipo Kigoma na hivi karibuni imeingia Zanzibar sababu ya Maalim Seif.

Kwa mtazamo huu, bado itachukua karne kuifikia CCM, ni sawa leo kulinganisha makanisa, taasisi kama RC, makanisa ya CCT na makanisa ya akina Mwamposa, Gwajima et al.

Leo Zitto, Mbowe ni ''mitume'' kwenye vyama vyao; hata wafuasi wao wanakiri kuwa bila wao vyama vyao vinakufa.

Tujadili kwa hoja si viroja.
 
Kwa mbinu hii ya kuengua wagombea kwa vijisababu uchwara ili chama la mashetani lipite bila kupingwa nadhani utakuwa upo sahihi
 
Hata CCM hawana uwezo huo pia, wanalazimisha tu. Kikawaida chama kikishakuona hakina njia ya kushinda katika eneo fulani, rather than kupoteza muda na pesa za walipakodi, unatakiwa ukubali tu uhalisia. E.g. CCM hawana uwezo wa kusimamisha mgombea kisiwa kizima cha Pembaa lakini wanalazimisha tu kama wanavolazimisha kukaa madarakani!
 
Wanaokoseaga kujaza fomu ni chadema tu ccm kuna ndezi nyingi sijui kwanini hazikoseagi kujaza fomu, upinzani ukipata ufumbuzi was kujaza fomu hakika hakuna kitongoji kitakochopita bila kupingwa
 
Hata CCM hawana uwezo huo pia, wanalazimisha tu. Kikawaida chama kikishakuona hakina njia ya kushinda katika eneo fulani, rather than kupoteza muda na pesa za walipakodi, unatakiwa ukubali tu uhalisia. E.g. CCM hawana uwezo wa kusimamisha mgombea kisiwa kizima cha Pembaa lakini wanalazimisha tu kama wanavolazimisha kukaa madarakani!
CCM ni kama RC au BAKWATA hao wengine (Chadema,ACT nk) ni kama Mwamposa,Gwajima
 
Back
Top Bottom