Hakuna chama kilichotamba duniani kama Baath Party

Hakuna chama kilichotamba duniani kama Baath Party

Watanzania wengi hawaitaki ccm tatizo upimzani wameshindwa kujipanga kama wangejipanga au kuwa na watu makini watu milioni kumi na nne waliokataa kupiga kura robo tatu wangepiga kura.

CCM inashinda kutokana na madhaifu ya wapinzani.
 
Sidhani kama unaweza kukiri, ila umetumia mfano mbovu na ndo maana pushback ya watu imekuwa jinsi ilivyo.

Chama cha Ba’ath na mambo yaliyopelekea kudondoka kwake ni tofauti sana na mazingira yetu hapa Tanzania na CCM.

Kwamba sijui mazingira ya CCM na Baath ni tofauti kabisa?

Au sijui Africa kuna vyama vingine kandamizi kama huko Rwanda na Uganda na bado vinadunda?
 
Iraq democracy ndio imeshamiri?😂😂😂😂😂
IS/ISS, suicide bombs, kidnapping for ransoms etc are order of the day, and we call that democracy!

Nakubaliana kabisa kuwa si vema kupoka ushindi wa vyama vingine kimagumashi, ila kama kweli democracy ingekuwa ipo Iraq, hata Baath party ilistahili Kupewa nafasi kushiriki kwenye democracy hiyo.
 
Iraq democracy ndio imeshamiri?😂😂😂😂😂
IS/ISS, suicide bombs, kidnapping for ransoms etc are order of the day...and we call that democracy!
Nakubaliana kabisa kuwa si vema kupoka ushindi wa vyama vingine kimagumashi, ila kama kweli democracy ingekuwa ipo Iraq, hata Baath party ilistahili Kupewa nafasi kushiriki kwenye democracy hiyo
Two wrongs do not make it right.

Kama now Iraq ni pabaya zaidi haiondoi ukweli Baath walichangia kufika hapo
 
Yanayoikuta Iraq tunayajua.
Hali yq Iraq inasikitisha tofauti na unavyosema.
Iraq ni shida unadai kuna demokrasia.
Demokrasia ipi Uraq iliyopasuka!
Kama ndio Demokrasia hiyo itupite tuu.
 
Two wrongs do not make it right..

Kama now Iraq ni pabaya zaidi
Haiondoi ukweli Baath walichangia kufika hapo

Indeed I dont support what Sadam and his gang were doing. And if two wrongs dont make something right, barring the Baath party to exist is not a democracy that people are talking about.
 
Uelewa wa Watanzania (baadhi) kuhusu Siasa za Kidunia ni mdogo sana, sasa unawezaje kulinganisha Baath na CCM kwa mfano? USA alivamia Irak kumuondoa Sadamu Husseni na siyo kukiondoa Chama cha Baath, sasa USA avamie Tanzania kumuondoa nani? na Kwa sababu gani? Magufuli anamaliza muda wake 2025, sasa USA ivamie kuondoa CCM? CCM ni ni kwanza? CCM ni Taasisi na siyo mtu, na mnafikiri ni uamuzi rahisi kwa USA kutumia Majeshi yake kuivamia nchi nyingine ambayo siyo threat kwa namna yoyote ile kwa USA? Ni Raisi gani wa USA atakuwa mjinga hivyo?

Jielimisheni kwanza Siasa za Kidunia zinavyokwenda kama ingekuwa rahisi kivivyo si wangeshavamia Uganda kwanza kumuondoa Museveni au unafikiri ni ninyi tu ndiyo wenye malalamiko hapa Duniani?

Ngoja niitafute hotuba ya George Bush nadhani itatatua ubishani uliopo kati yako na huyo jamaa, kwa kifupi sana kabla sijaileta,USA ilitoa idadi ya zaidi ya watu 50 ambao walikuwa most wanted kule Iraq akiwemo Saddam na wanachama wenzie wa hiko chama ambao iliwatuhumu pamoja na mambo mengine ukiukwaji wa haki za binadamu.

katika hotuba yake nyingine wakati anahotubia bunge la Marekani George bush alisema sababu za kwanini marekani ivamie Iraq akataja pia uminywaji wa Democrasia,akamtuhumu saddam kumiliki weapons of mass destruction na akaongelea mauaji ya raia ambavyo vyote vilisimamiwa na chama,

Hivyo basi kukitoa chama madarakani ilikuwa ni moja ya sababu ya kuvamia Iraq. unachosema ni sawa sawa na mtu aseme uvamizi wa allied forces ujerumani haukulenga kukitoa chama cha Nazi madarakani wakati baada ya vita viongozi wote wa Chama cha Nazi walipelekwa nuremberg trial na chama cha Nazi kikafutwa kabisa.
 
Baath party walikuwa maharamia haswa
 
Nazi. Sijui kama nimetaja vizuri. Hao jamaa waliua vibaya sana.

Kiufupi.

HAKUNA JAMBO JIPYA DUNIANI.

"Wasiosoma ni chakula cha wasomi, wasomi Ni chakula cha wanasiasa, wanasiasa Ni chakula cha wafanyabiashara".
Kwa hiyo tunakulana??? Hahahahaaa...
 
Bro ona aibu ata kidogo Iraq hii hii iliyogeuka magofu na vita ya wenyewekwa wenyewe, unaisifu ina demokrasia na inachagua wabunge wanaotakiwa.
Kwa hiyo kabla ndo kulikuwa na demokrasia bora kuliko hii ya sasa?
 
Chama cha Baathi kilikuwa mpaka Syria hawa naweza kusema ni kama taasisi walikuwa walikuwa wako katika kila idara ya serikali ni kama mfumo wa CCM sasa hivi, na ndio sababu kubwa USA walipomuondoa madarakani Saddam kosa kubwa walilolifanya ni kuvunja chama na kuwaondoa viongozi,

wanachama na wafuasi wa chama cha Baathi mpaka katika vyombo vya usalama hii ndio ikaleta balaa la muda mrefu kukawa na visasi na kama kuanza kuunda kila kitu upya maana chama kilikuwa na mizizi kila sehemu ikawa utafukuza mpaka wapi, na chama cha Baathi cha Iraq na Syria (bado kipo) hawa walikuwa sio mchezo wana majasusi kila kona ni mfumo wa maisha ya watu hujajiunga na Baathi huna nafasi kupata kazi.

Ziko clip za Saddam katika mikutano ya chama alikuwa kapata taarifa kuna viongozi walikuwa wanataka kupinga uongozi wa chama, aliwataja mbele ya watu basi ukitajwa unainuka, ukisimama tu unatolewa nje ndio unapotezwa moja kwa moja uasi ndani ya chama kama ndoto maana kuna ujasusi wa hali ya juu. Kurudi hapa kwetu ndio kama CCM,

Sote tunajuwa wafuasi wa CCM sio hawa wanaoshika kanga na kofia tu, wako kila sehemu maofisini, idara zote, vyombo vya usalama mpaka majeshi yote huwezi kupewa kitengo kama wewe sio CCM toka zamani ndio maana unaona wakistaafu kama ma judge au wanajeshi wanapewa nafasi katika serikali hata na wengine wanarudi wanakuwa majasusi ndani ya chama, hata watu wa kitengo wakistaafu wanakuja kufanya kazi za kijasusi ndani ya chama.

Kuiondoa CCM unaondoa mfumo wote wako kila sehemu na wao wanajuwa hilo ndio maana hawatumii nguvu sana katika kampeni. usisikie hizi story za viongozi wa usalama kuwa hatuna chama tunasimamia amani tu hilo hakuna wote viongozi wote wa vyombo vya usalama na maofisi yote idara zote wako na wanafanya kazi kuhakikisha kila kitu under control.

Kwa ufupi kuiondoa CCM ni kama kuiondoa Baathi na kuna gharama. KANU kenya waliondolewa sababu hawakuwa na mfumo kama wa CCM na zaidi KANU iliondolewa na wana KANU wenyewe wamejigawa tu nje lakini ni walewale kina Kenyata, Mudavadi na wengine wengi hakuna jipya ni kama kwenda mahakamani kubadili jina lako kisheria lakini utabaki yuleyule.
Hoja nzito.... Ukweli mtupu...
 
Mbona sioni post namba moja ya uzi huu!? Post imeanzia namba mbili!
 
Back
Top Bottom