Chama cha Baathi kilikuwa mpaka Syria hawa naweza kusema ni kama taasisi walikuwa walikuwa wako katika kila idara ya serikali ni kama mfumo wa CCM sasa hivi, na ndio sababu kubwa USA walipomuondoa madarakani Saddam kosa kubwa walilolifanya ni kuvunja chama na kuwaondoa viongozi,
wanachama na wafuasi wa chama cha Baathi mpaka katika vyombo vya usalama hii ndio ikaleta balaa la muda mrefu kukawa na visasi na kama kuanza kuunda kila kitu upya maana chama kilikuwa na mizizi kila sehemu ikawa utafukuza mpaka wapi, na chama cha Baathi cha Iraq na Syria (bado kipo) hawa walikuwa sio mchezo wana majasusi kila kona ni mfumo wa maisha ya watu hujajiunga na Baathi huna nafasi kupata kazi.
Ziko clip za Saddam katika mikutano ya chama alikuwa kapata taarifa kuna viongozi walikuwa wanataka kupinga uongozi wa chama, aliwataja mbele ya watu basi ukitajwa unainuka, ukisimama tu unatolewa nje ndio unapotezwa moja kwa moja uasi ndani ya chama kama ndoto maana kuna ujasusi wa hali ya juu. Kurudi hapa kwetu ndio kama CCM,
Sote tunajuwa wafuasi wa CCM sio hawa wanaoshika kanga na kofia tu, wako kila sehemu maofisini, idara zote, vyombo vya usalama mpaka majeshi yote huwezi kupewa kitengo kama wewe sio CCM toka zamani ndio maana unaona wakistaafu kama ma judge au wanajeshi wanapewa nafasi katika serikali hata na wengine wanarudi wanakuwa majasusi ndani ya chama, hata watu wa kitengo wakistaafu wanakuja kufanya kazi za kijasusi ndani ya chama.
Kuiondoa CCM unaondoa mfumo wote wako kila sehemu na wao wanajuwa hilo ndio maana hawatumii nguvu sana katika kampeni. usisikie hizi story za viongozi wa usalama kuwa hatuna chama tunasimamia amani tu hilo hakuna wote viongozi wote wa vyombo vya usalama na maofisi yote idara zote wako na wanafanya kazi kuhakikisha kila kitu under control.
Kwa ufupi kuiondoa CCM ni kama kuiondoa Baathi na kuna gharama. KANU kenya waliondolewa sababu hawakuwa na mfumo kama wa CCM na zaidi KANU iliondolewa na wana KANU wenyewe wamejigawa tu nje lakini ni walewale kina Kenyata, Mudavadi na wengine wengi hakuna jipya ni kama kwenda mahakamani kubadili jina lako kisheria lakini utabaki yuleyule.