Hakuna faida kuwaheshimu wafu | Mpe heshima anapokuwa hai

Hakuna faida kuwaheshimu wafu | Mpe heshima anapokuwa hai

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2015
Posts
2,451
Reaction score
2,466
Nagusia mifano michache tu.

Maradona ana historia ndefu sana pale Italia hapo kwenye club yake ya Napoli. Baada ya kufa ndio ule uwanja unaotumiwa na club yake ukapewa jina lake, hapo Maradona alifaidika nini?

Ilishindikana nini kupewa hilo jina mfu akiwa hai?

Kuna mifano mingi tu ya kusemea.
Mkapa,Kijazi n.k
Vipi hawa Messi, Ronaldo de Lima, Cristiano,Ibrahimovic,Samatta Diamond (Chibu) n.k mpaka wafe ndio wapewe heshima?

Tujifunze kutambua michango ya watu na wapewe heshima wakiwa hai,mtu akifa hasikii wala hawezi kufanya chochote,hata kama alikua na chuki na wewe hawezi kulipa kisasi tena.
 
Huku Madeira, Portugal tumeshampa heshima yake jembe letu
 
Mtoa mada umeumia kuona Kijazi interchange 😂😂😂 bado usisahau hata wasiokufa tunawabrand..
mf.
Soko la Ndugai
 
Ni kutunza historia.

Hata miaka 50 mbele wakiuliza kwanini hapa pakaitwa hivi wanaambia alikuwa mtu maarufu kwenye hili na hili.
Basi wasiseme "kwa heshima yaa" iwe ni kwa historia ya...
 
Binadamu ana thamani akiwa hai tu, ndugu zangu tusidanganyane, ukishakufa huna lolote kuku alie hai ana thamani 1000 times kuliko maiti kwasababu atakua mboga wageni wakikufikia.
 
Hii haihusiani kabisa na kilichotokea leo
Mtoa mada umeumia kuona Kijazi interchange 😂😂😂 bado usisahau hata wasiokufa tunawabrand..
mf.
Soko la Ndugai
Jibu swali hili. Mfu kupewa heshima inamsaidia nini?
 
Binadamu ana thamani akiwa hai tu, ndugu zangu tusidanganyane, ukishakufa huna lolote kuku alie hai ana thamani 1000 times kuliko maiti kwasababu atakua mboga wageni wakikufikia.
Atakua mzimu......atakua na thamani
 
Back
Top Bottom