Hakuna faida ya kuwa na marafiki

Hakuna faida ya kuwa na marafiki

Zamani nilikuwa nawashangaa Watu ambao wana
Marafiki Wachache (SMALL CIRCLE), nikawa najiuliza
yaani Dunia ilivyo na watu wengi hivi inawezekanaje
mtu akawa na MARAFIKI 7 TU?? Lakini sasa
nimeelewa jambo 1, HAKUNA FAIDA ya kuwa na
Marafiki Lundo ambao Hawakuingizii Hata Senti 5... A relationship should be a WIN-WIN SITUATION... Peaneni dili...Huyu awe na Bar na Iwe Bar yenu
wote, mnywe na kula ili RAFIKI YENU AINGIZE HELA..
Huyu awe na INSURANCE COMPANY, na Circle yote
ikate Bima kwake AINGIZE HELA... Huyu awe na
BAKERY na wote mnunue Mikate hapo na kumsaidia kuitangaza Wateja waongezeke...
HUO NDIO URAFIKI! Hamna Faida ya kuwa na Marafiki
Jeshi ambao ukipata hata shida ya Elfu 50 WOTE
WAMEFULIA HAWANA MSAADA, na hawakuingizii
Hela, ila ikifika Kila Ijumaa wao ndio wa kwanza
kutuma meseji za "OYA BATA WAPI LEO" Bata wako Bandani Wamelala
Kenge wa Maziwa we!
isee uko kama mimi,me marafiki wa kipuuzi puuzi sina,ushenzi wa kuwa na marafiki muda wote wanaongea pumba na kulia njaa me sitakagi kabisa,weekend nikichoka naenda zangu kula mtungi narudi home kimya kimya ile mambo ya kufatana fatana kama ruba ni kuambukizana upuuzi tu
 
"Marafiki sihataji hawaletagi Maendeleo"

Labda baadae wakitokea aje mmoja wa kuongea nae na mmoja wa kumuongelea
 
1473942688432.jpg
Marafiki weng ni hatari sana hata M.Mungu katuonya katika maandiko yake Matakatifu!!!..
 
Na wewe ungekuwa ni miongoni mwa waliofulia, ungejisikiaje marafiki zako wote wa karibu ambao angalau wanajiweza kuliko wewe wakikutupa kwa kuwa umefulia? Kataa marafiki wanaoweza kukupotosha na kukuharibia maisha yako tu lakini si kwa kigezo cha kufulia. Marafiki ni muhimu kwetu kwa namna yeyote ile sio lazima wawe wanakusaidia. Futa hiyo dhana ya kusaidiwa, hatuishi ili tusaidiwe ila ni wajibu wetu kila mmoja ajisaidie wenyewe.
Safi kabisa nadhani mtizamo wako wewe ndo upo sahihi.. Kula five Kaka umetisha mtoa maadA lazima ajue kuwa watu wametofautina maisha, vipato na mambo mengi muhimu ni kwenda nao vizur.. huwezi kusema hutaki marafiki akati Kuna shughuli nyingine Bila watu haziendi.. Unaonaje ikiwa una marafiki saba na wote Wana uwezo halafu kwenye harusi au msba au janga lolote wakajitokeza Hao saba tu. Mwisho tupendane wote
 
Dah mimi ninao wanne tu! kati yao yupo ndugu wa tumbo moja....watu waliobakia ni kusalimiana, hamna cha zaidi.
 
Dah....mimi nipo wazi kabisa kama ni mvivu halafu hata wazo lolote la kutoka kimaisha huna....nakupigachini... Labda uwe dem[emoji4]
 
Zamani nilikuwa nawashangaa Watu ambao wana
Marafiki Wachache (SMALL CIRCLE), nikawa najiuliza
yaani Dunia ilivyo na watu wengi hivi inawezekanaje
mtu akawa na MARAFIKI 7 TU?? Lakini sasa
nimeelewa jambo 1, HAKUNA FAIDA ya kuwa na
Marafiki Lundo ambao Hawakuingizii Hata Senti 5... A relationship should be a WIN-WIN SITUATION... Peaneni dili...Huyu awe na Bar na Iwe Bar yenu
wote, mnywe na kula ili RAFIKI YENU AINGIZE HELA..
Huyu awe na INSURANCE COMPANY, na Circle yote
ikate Bima kwake AINGIZE HELA... Huyu awe na
BAKERY na wote mnunue Mikate hapo na kumsaidia kuitangaza Wateja waongezeke...
HUO NDIO URAFIKI! Hamna Faida ya kuwa na Marafiki
Jeshi ambao ukipata hata shida ya Elfu 50 WOTE
WAMEFULIA HAWANA MSAADA, na hawakuingizii
Hela, ila ikifika Kila Ijumaa wao ndio wa kwanza
kutuma meseji za "OYA BATA WAPI LEO" Bata wako Bandani Wamelala
Kenge wa Maziwa we!

Ndiooooo
 
Kimsingi Urafiki ni swala la kijamii..
Ndo maana mtoto anapokuwa around miaka 4/5 tunajiuliza kama ame-achieve social milestone ya 'uwezo wa kujenga na kuendeleza urafiki'..urafiki unakujenga kihisia, uwe mvumilivu, honest, courageous na virtues zingine, urafiki unakupa kumbukumbu njema...urafiki ni mtamu...
So binafsi sioni haja ya kufanya urafiki kuwa solely swala la kiuchumi..hatuishi ili tupate pesa tu..WE ARE LIVING A LIFE.
I have very good friends who are poor and stupid friends who are rich..I love all of em as long as they bring hapinness than money does.
Poor friends are like a coat of many colors Dolly parton talked of.
Anyway, Cha msingi ni kuwa na watu wanaoendana na attitude yako.
 
kweli hali ya uchumi imeporomoka tunaanza kukataa hadi marafiki
 
Tulipokuwa vijana tulishangaa kwa nini matajiri hawana marafiki,kumbe waliona mbali.
Na wengi waliofanikiwa hawana mlolongo wa marafiki,na hata ukitaka kuwazoea huwezi pata kitu,funga safari nenda kwake hata maji ya kunywa hupati na utaishia kukaribishwa ndani ya geti lakini nje ya nyumba🙂
alafu matajiri wengi mabahili
 
Hii Mada yako ina ukweli mtupu.

Btw: We Don Need Friends Nowdays

"We Only Needs Business/ Educational Partners"

Marafiki wengi wanafiki / mzigo.
Kweli kabisa
 
nahis it goes with age unapozd kukua ndio circle inapopungua
 
Na wewe ungekuwa ni miongoni mwa waliofulia, ungejisikiaje marafiki zako wote wa karibu ambao angalau wanajiweza kuliko wewe wakikutupa kwa kuwa umefulia? Kataa marafiki wanaoweza kukupotosha na kukuharibia maisha yako tu lakini si kwa kigezo cha kufulia. Marafiki ni muhimu kwetu kwa namna yeyote ile sio lazima wawe wanakusaidia. Futa hiyo dhana ya kusaidiwa, hatuishi ili tusaidiwe ila ni wajibu wetu kila mmoja ajisaidie wenyewe.
Mlundikano wa marafiki hewa wasio na faida yoyote ndo kitu kinachopingwa, soma vizuri post
 
Back
Top Bottom