Hakuna Fao la Kujitoa NSSF duniani kote - Ramadhan Dau


Tatizo mmeshazipangia pesa zetu mzitumie kwenye uchaguzi 2015 kununulia kanga na fulana siyo!!
Imekula kwenu pesa yetu ni chungu hailiwi.Tunajua Dau ni rafiki wa Dhaifu wamekaa na kushauriana
huu ujinga aliokuja kuusema.Hii itawagharimu kuliko inavyomgharimu Zuma S.A
 
Sheria ya workmana compnsation mpaka leo haijasainiwa hii ya mifuko ya jamii imesainiwa haraka sana kuna ajenda gani nyie???
 
Dau asituzingue na historia ya wenzetu. Inamaana kama kenya wanakunya barabarani kwa hiyo na sisi tuige kunya barabarani?
Kenya baadhi ya wastaafu au walioachishwa kazi wakiwa na umri mdogo wengi wao wamepoteza haki zao. Tusiige upumbavu tuige uwerevu
 

Mazindu M.

Unachozungumza ni kweli kabisa lakin huku kwetu sisi thamani kubwa ipo kwa mzawa na mgeni baadae. Sera zetu zote zinamwangalia mwananchi zaidi kuliko mgeni na hata panapotokea ilmu ipo sawa baina ya mgeni na mwenyeji basi mwenyeji anapata ujira zaidi kulinganisha na mgeni.

Kifupi sera zetu zinalinda sana wenyeji tofauti na huko Sera zenu zinamwangalia na kulinda wageni zaidi kuliko wazawa.

Kumbuka huku kwetu mfanyakazi anaweza kujengewa au kununua nyumba kutokana na mafao yake ya Uzeeni. Anapata hata mikopo ya kuanzishia Biashara mbalimbali na security yake ni pesa zake za uzeeni.

Ni wakti muafaka kuangalia wazawa kwanza na kunufaisha wazawa zaidi ya wageni. Wenye mamlaka ya kufanya hayo yote ni Serikali na Bunge.

 
Ni kweli anayosema lakini atutajie nchi yoyote ambayo pesa zao za mafao zinawekezwa kwa stahili ya uwekezaji wa tanzania ambapo pesa zinatolewa kienyeji ili kuifuraisha serikali au wakubwa wa serikali na ukopeshaji kwa watu wasio wanachama kama Manji kuwataja wachache
Atueleze namna gani atarudisha pesa zilizowekezwa kwenye miradi ambayo mpaka sasa hivi haijarudisha pesa kama machinga complex,general tyre,kiwira mine kuitaja kwa uchache
Pia atueleze kwanini riba wanayotoa kwa mafao ya wafanyakazi ni ndogo 1.8% kwa mwaka ambayo hailingani na riba za kibenki wala mfumuko wa bei wa Tanzania
hatueleze kwanini wafanyakazi hawapewi hisa kwenye miradi ya uwekezaji wa nssf wakati ni pesa zao ndio zinatumika
 



Na hawa ni mashahidi wa miaka ijayo:

 
Dr, dau . Wewe unalala gorofani unakula mpaka unasaza , sitarehe zote duaniani ukipenda unapata ebu fikiria wachimaji na wafanyakazi wengine wanaacha kazi hali zao mbaya ,kiukweli wanatisha , wana umri wa mika 23 mpaka 40 eti wasubiri mpaka 55 to 60 haiwezekani. Fikiria hata hawa masikini hawa . Usione kwa kuwa wewe unmejaliwa kipato ukadhani wote ni hivyo hapana. Kwa wale wanaoendelea na kazi hao sawa .lakini wanaoacha tafadhalia sana dau wapeni fedha zao. Wewe kinakuuma nini. Au umejengea madaraja na mabweni dodma? Kuwa mwenye upendo kwa masikini na wewe utabarikiwa kwa kauli yako ya jana ni kama wewe si mtanznia . Kuwa nahuruma walau kidogo dr. Dau. Utajiri wako unaweza kugeuka kuwa laana kama utaendele kudharau masikini hawa.
 
Sijui DUNIANI kote anakuelewaje?

Types of UK Pensions.

Brief explanations of the different types of UK pensions are given below, please follow the links for more information.

Basic state pension.
Although an entitlement for most people, the amount received from the basic state pension will depend on the amount of national insurance contributions paid. more >>

State Second Pension.
On 6 April 2002, the State Second Pension (S2P), introduced by the Child Support, Pensions and Social Security Act 2000 replaced the State Earnings Related Pension Scheme (SERPS). more >>

Personal and Stakeholder pensions.
Personal pensions, introduced on 1 July 1988, originally aimed to give people who were not part of a company pension scheme their own portable pension, designed on a money purchase basis although since April 2001 certain individuals who are members of company pension schemes can also take out personal pensions. more >>

Occupational pension schemes.
Employers can set up occupational pension schemes for their employees.Public sector schemes typically offer pension accrual of 1/80th of final remuneration for each year of service up to a maximum of 40 years plus a tax free lump sum of up to 1.5 x final remuneration.
Private sector schemes can be either final salary schemes known as defined benefit schemes or money purchase schemes known as defined contribution schemes. more >>

Additional Voluntary Contributions (AVCs).
It is now compulsory for companies to offer employees the opportunity to invest additional contributions into their occupational scheme where there is one, in order to boost retirement benefits. more >>

Free Standing Additional Voluntary Contributions (FSAVCs).
Free standing additional voluntary contribution schemes (FSAVCs) were introduced in 1987. more >>

Self Invested Personal Pension Schemes (SIPPS).
From April 6th 2006 Government proposals for pension simplification came into effect. This has lead to many new opportunities for people to invest their savings for the long term with greater flexibility when it comes to retirement and ways of generating an income. more >>


State Earnings Related Pension Scheme (SERPS).
The State Second Pension (S2P) replaced SERPS with effect from 6 April 2002. more >>
 
Ustaadhi Ramadhani Dau anapotulinganisha na nchi nyingine in terms of hii sheria ya fao la kujitoa, pia aende mbali atueleze ni kwa namna gani mifuko ya NSSF katika nchi hizo inawanufaisha wananchama kwa kuwakopesha kujenga nyumba, kusomesha watoto wao ama wao wenyewe ikiwa ni pamoja na kujifanyia shughuli nyengine za kimaendeleo kwa kutumia hizo michango zao za pensheni. Lakini pia atuambie kiwango cha security ya ajira katika nchi nyengine kama kinawiana na hapa kwetu.

Kama hayo niliyoyataja yanafanyika huko kwa wenzetu na hapa kwetu hayafanyiki basi anatakiwa aache kutuletea ujuaji wa kijinga ambao hauna maana yoyote kwa wananchama ambao ndiyo wenye fedha zao. Wakijifanya kuziba masikio sasa kwa mara ya kwanza wataiona hasira ya wafanyakazi mwaka huu.

Na wabunge wetu nao wakiamua kulikalia kimya suala hili bila kuilazimisha serikali kurudisha fao la kujitoa katika mifuko yote ya pensheni kama ilivyokuwa awali basi watambue kwamba hatutawaelewa kamwe katika hili, na vita yetu itaelekezwa kwao moja kwa moja.
 
Waarabu tunausemi unaosema '' NI RAHISI SANA KUWADANGANYA WATU, LAKIN NI VIGUMU SANA KUWAFAHAMISHA WATU KUWA MUMEDANGANYWA"

Je WaTz mnaweza kuishi dunia ya peke yenu? Dr amesema hakuna kitu kama hicho sasa kama mnabisha pitia mifumo yote ya pension Duniani muhakikishe maneno yake.

Lakin mimi namini kabisa alichobainisha ni kile kinachotumika Duniani kote. Ushauri wangu kwenu ni kuwa Murekebishe SERA zenu za Ajira na kazi
1.ziwe zinamlinda zaidi mwananchi badala ya mgeni.
2. Pesa za pension ziwe zinaweza kusimama kama dhamana kwa mwanachama kuweza kukopa bank.
3. Pension ziwe na saccos zake kukopesha wanachama wake.
4. Kuboresha mafao kwa wananchama.

Yote yatawezakana kama Serikali yenu na Bunge lenu litakapo jaribu kuangalia nchi nyingine zinafanyaje.
 
Hivi mi nauliza "where are these hounourable members?" Tuliwachagua kufanya nini? Jamani tumeshachoka na maamuzi ya kiimla. Wasiporekebishia wafanyakazi fao la kujitoa, ni vizuri tupate orodha ya waheshimiwa wetu ambao hawakutusupport, maana 2015 siyo mbali. Halafu ndo na wao waelewe msemo adui muombee njaa. (maana wakishindwa kurekebisha na wao pia wabanwe na huo huo msumeno).
 
Watu wa Maifa Makubwa ya ulaya na Marekani wanapenda kuweka historia ya jambo fulani,
hasa kwa kuanzisha kitu au Mfumo mpya then Dunia inaiga/ kufuata..., hapa kwetu is unlike kwani
wataalamu na Viongozi wetu wengi ni vihiyo, hawana uwezo wa kuleta new ideas na ubunifu kwani
wamezoea "Copy and Pest", bila hata aya na kukosa kujiamini , jitu linasema bila ya kuangalia uhalisia
wa mifumo ya kazi ya wananchi...,kwakweli hana Mashiko kimtazoma wa Mawazo.



 
Ahahaha!!!! Dau anataka kuhalalisha wizi wa duniani kwingine Tanzania. Kwi kwi kwi kwi kwi kwi!!!
Hii fukuza fukuza hata ya serikali iliyokuja kwa jina la kustaafisha kila siku watu wanastaafishwa kwenye mashirika mbali mbali hiyo nayo iko duniani kote?? Sawa hakuna shida lakini sio kila kitu cha duniani kote ni halali kwetu. Huu ndio ujuha tulionao wa kukopi na kupesti ili wahalalishe matumizi mabaya ya wafanyakazi maskini wanaoishi kwa kupunjwa mishahara!
Kazi kwenu wafanyakazi msipochangamka shauri yenu. Mmeshaliwa na wakina Dau ambao mwisho wa siku wanatafuta wapewe nafasi ya kugombea uongozi kupitia bunge au lichama linaitwa sisi M.
 

Na kuvumilia kwenye kazi ya kusuasua, bosi mwenye majungu na written warnings kibao, halafu tena ubaniwe hela yako...Aisee hata ladha ya mate inakuwa shubiri.
 

Nakuunga mkono Barubaru, ndio maana mwanzoni nilipingana na wewe kulinganisha issue ya fao hilo la kujitoa hapa Tanzania na huko kwenu, hapa kwetu nidhamu ya pesa hakuna kabisa, mashirika mengi ya umma yalikufa sababu zikiwa ni nyingi, moja wapo ni hii, serikali kujichulia pesa na kwenda kufanya mambo ambayo hayana uhusiano wowote na hiyo shirika, utakuta pesa inachukulia kwenda kwenye kampeni za ccm, mbio za mwenge, safari za waheshimiwa au posho za vikao, kwa mwendo huu wa akina Dau, sitashangaa nikisikia mifuko hii imefirisika siku moja, biashara lazima ifuate miiko yake, ni kweli suala la kujengwa daraja la kigamboni ni la muhimu, na ni kweli kwamba ujenzi wa chuo kikuu cha dodoma aua hosteli za Mabibo ni muhimu, lakini hebu tujaribu ku imagine, Mkurugenzi mkuu wa mashirika haya angekua Mzungu, hivi unadhani wangechukua hizo pesa na kwenda kufanyia mambo hayo? siasa za ccm ndio zinazofirisi nchi hii, uliisha wahi kujiuliza, how comes waastafu wa uliokua jumuia ya Africa mashariki kwa nchi zingine waliisha lipwa, mbona hapa Nyumbani badala ya kulipwa wamenunuliwa gari la maji ya kuwasha? ukweli ni huu, mimi kama mfanyakazi, sina imani kabisa na serikali ya ccm kwamba inaweza kunitunzia pesa zangu hadi nitakapo fika uzeeni, kama waliweza kuiba pesa za EPA ili tu ccm iingie madarakani, na kumbuka wakati ule wa uchaguzi wa 2005 ccm haikua na upinzani mkubwa kama leo, hivi 2015 watatumia pesa kiasi gani ili waendelee kua madarakani, na hizo pesa watatoa wapi?

Nashukuru kwa kunipa masikio yako.
 
Me nashangaa, sijui hata hawafikiriii hawa watu???? hivi fikiria umefanya kazi na kampuni kama sita na pengine ni mikoa tofauti, hivi utakapofikisha umri wa kustaafu hizo fomu za mafao yako anakujazia nani???? au ndo unaanza kuzunguka tena kutoka ofisi moja hadi nyingine??? na hiyo gharama unapata wapi??? si matokeo yake utakuta mafao yako utakuta umeshayamalizia kwenye gharama za kufatilia hizo fomu zako zijazwe?????? na huwezi jua wakati mwingine hizo ofisi zilishafungwa na kufa. Mimi nina wasi wasi hiyo hela wameshakula wanatafuta njia rahisi ya kututapeli pesa zetu. sidhani kama wanaona mbali hawa watu, la sivyo ni wabinafsi, wanajali matumbo yao na familia zao wanatusahau sisi ambao kimsingi ndio mabosi wao maana hayo hayo mafao yetu ndo yanawaweka hapo maofisini.
 

Kumbe " Asasi ya Kusaidia Uwekezaji Kwenye Kilimo (Pass)" ni ya NSSF?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…