Mkurugenzi wa NSSF Dr Ramadhan Dau amesema Fao la kujitoa limeondolewa ili kuendana na mfumo wa kimataifa kwani duniani kote hakuna Fao la kujitoa.
Amesema hata Zanzibar na Kenya hakuna kitu kama hicho.
Mkurugenzi huyo alitoa tamko hilo alipokuwa akihojiwa na Kamati ya bunge ya mashirika ya umma inayoongozwa na Zitto Kabwe.
Source: ITV Habari
UPDATES.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Muswada wa mafao wawaliza wafanyakazi
Muswada wa marekebisho ya sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambao unatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano wa Kumi wa Bunge, umewaacha solemba wanachama wa mifuko mingine baada ya marekebisho hayo kurejesha fao hilo kwa mfuko mmoja pekee.
Sheria ya mafao ilipitishwa katika mkutano wa Bunge wa Aprili mwaka huu na kuwazuia wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuruhusiwa kuchukua mafao yao hadi wafikishe umri kati ya miaka 55 na 60.
Baada ya wanachama wa mifuko hiyo na wadau wengine wakiwamo wabunge kuipinga sheria hiyo, serikali iliahidi kuwa itaifanyia marekebisho na kuwasilisha muswada kwa hati ya dharura.
Tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, amekwishawasilisha muswada huo katika Ofisi Ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam, ikiwa na maana kuwa utajadiliwa kwenye Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza wiki ijayo.
Muswada huo unakusudia kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali.
Kwa mujibu wa muswada huo, ambao NIPASHE imeuona, sehemu ya sita inapendekeza marekebisho kwenye Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), sura ya 372 kwa kuongeza kifungu kipya cha 44 ili kutoa fursa kwa mfuko huo kutoa fao la kujitoa kwa mwanachama wake.
Kwa maana nyingine ni kwamba wanachama wa mifuko mingine kama NSSF itaendelea kutumia sheria ambayo imelalamikiwa na wafanyakazi.
HOJA YA JAFO YAZIKWA
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kisarawe (CCM), Seleman Jafo, ambaye wakati wa mkutano wa Bunge wa Bajeti, alitaka kuwasilisha muswada binafsi, alisema amepata barua kutoka kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah, ikimtaarifu kwamba, serikali itawasilisha muswada wa marekebisho hayo, hivyo hana sababu ya kuandika muswada mpya.
Jafo alisema kwa kuwa alikwishawasilisha hoja ya kutaka marekebisho kwenye sheria ya hifadhi ya jamii, Bunge lilimweleza kwamba ni fursa kwa serikali au Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii; hivyo serikali imeazimia kuiwasilisha kwenye mkutano ujao.
Lakini kwa hali hii ni kwamba serikali haitatatua matatizo ya msingi ya hoja yangu, muswada unatakiwa uguse mifuko yote kwa sababu malalamiko ni ya wafanyakazi wote, alisema.
SUGU AIONYA SERIKALI
Kwa upande wake, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, aliionya serikali kutochezea wafanyakazi kwa kuwa kufanya hivyo ni kuhamasisha fujo.
Alisema ni vyema marekebisho yatakayowasilishwa bungeni yakarejesha fao la kujitoa kwa mifuko yote kwa kuwa wafanyakazi wengi hawana usalama kazini.
Tunajua faida ya pensheni uzeeni kwa sababu ni msaada mtu anapostaafu, lakini kwa mfumo wa nchi yetu ambayo wafanyakazi hawana usalama wa kazi haiwezi kufanyakazi ipasavyo, alisema.
Sugu alisema wafanyakazi kama wa migodini au hostelini wanafanyakazi katika mazingira magumu na wanaweza kuachishwa kazi wakati wowote hivyo fao la kujitoa litawasaidia.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau, alisema fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii halimo katika sheria za kimataifa.
Dk. Dau, alisema hayo alipokuwa akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) katika kikao kati ya kamati hiyo na bodi na menejimenti ya shirika hilo, katika Ofisi Ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana.
Alisema pia ni Tanzania Bara pekee ndiko ambako kuna fao la kujitoa katika mifuko hiyo, lakini katika nchi za Kenya, Uganda, duniani kote, hata Zanzibar, suala hilo halipo.
Hata hivyo, alisema mwanachama wa NSSF anapoamua kujitoa, anaupunguzia Mfuko mzigo wa kumtunzia pensheni yake ya uzeeni, badala yake na kujiumiza mwenyewe.
Shinikizo la kutaka serikali kuirekebisha sheria hiyo ili wanachama wa mifuko walipwa mafao wakati wanapoacha kazi, liliilazimisha serikali kukubali yaishe na kuahidi kuwasilisha muswada wa marekebisho ya sheria ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2012.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, aliliambia Bunge la bajati kwamba kabla ya kuwasilishwa, muswada huo utapelekwa kwa wadau ili watoe maoni na pia Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) itatoa elimu kuhusu fao la kujitoa.
Hata hivyo, alisema wapo baadhi ya watu waliotafsiri kuwa kusitishwa kwa fao la kujitoa kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii imefilisika kwa kuwa imewekeza kwenye miradi mibaya, jambo alilosema sio la kweli.
Kabaka alisema kuwa mifuko hiyo haina hali mbaya kifedha wala haijafilisika na kwamba kuzuia fao la kujitoa ni utekelezaji wa sheria.
Waziri Kabaka alisema mchakato wa kuwasilisha muswada huo utaanza mara moja kwa kuwashirikisha wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Kabla ya kauli ya Kabaka, Bunge lilipitisha Azimio lililowasilishwa na Jafo, la kuletwa bungeni muswada wa dharura wa marekebisho ya Sheria Na. 5 ya mwaka 2012 inayozungumzia marekebisho ya Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo ndani yake inaelezea kuzuiwa kwa fao la kujitoa kwa wafanyakazi.
Kutokana na mapendekezo ya muswada huo kutowatuhusu wanachama wa mifumo kingine kuchukua mafao kabla ya miaka 55 au 60, wanachama hao huenda wakashinikiza kwa njia za maadamano na migomo.
Aidha, upo uwezekano wa kuzuka mjadala mkali bungeni kwa kuwa na wabunge nao ni wanachama wa mifuko hiyo.
Naomba kuuliza Udaktali wa Ramadhani Dau ni wa MIFUGO au Phd? Kila nikimtafakari sipati jibu hata kidogo. Uwezo wake wa kuelewa mambo ni mdogo sana na huenda ameathiliwa na madrasa. Amefanikiwa kupanda mbegu ya UDINI katika Shirika la NSSF sasa ameamua kuleta maisha magumu kwa wafanyakazi. Tunajua utajiri mkubwa alioupata ni kutokana na miradi mibivu aliyoianzisha tangu awe Mkurugenzi wa NSSF. Sasa amekuwa tajiri kiasi cha kuanza kuiga kila jambo linalofanywa na MABWANA wa inje.
Tanzania sio lazima kufuata mambo yanayofanywa na jirani zetu au Ulaya. Tanzania ni Nchi huru inatakiwa kufuata mambo yake. Kama kwa wenzetu hawana fao la kujitoa; sio lazima na sisi tuwafuate. Kenya kula mirungi ni kitu cha kawaida, lakini Tanzania ni sawa na dawa za kulevya. Tanzania tunaruhusu kushafirisha sandalwood, wakati Kenya imezuiliwa. Bila shaka Mr. Dau elimu yake ni kukopi na kupesti ndo maana kila kitu anawaza kuiga nje na jirani wanafanya nini.
Wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii wanahitaji kuyachukua mafao yao mara baada ya kuacha au kuachishwa kazi. Ajira za Tanzania hazina uhakika ukilinganisha na hizo Nchi anazotaka kukopi mambo yao.
Anadai eti kujitoa kwa Mwanachama kwenye mifuko ya hifadhi ni faida kwa mfuko husika. Sasa kwanini anakataa kujitoa kwa Mwanachama? Au tuamini maneno ya mtaani kuwa NSSF imewekeza kwenye miradi feki mingi kiasi kwamba wamefilisika?
Time value of money vipi? Wao wanawekeza pesa zetu kwenye mabenki kwa RIBA hadi ya 20% kwa mwaka, wakati Mwanachama hapati gawio la faida ya RIBA. Huu ni wizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii dhidi ya pesa za Wanachama. Mr. Dau asifikili Watanzania ni wajinga hata kama wameufumbia macho uozo alioufanya pale NSSF kwa kuligeuza Shirika la Uma kuwa taasisi ya KIDINI.
Mimi na familia yangu tumeamua kufunga na kuomba ili laana ya Mungu aliye hai ishuke juu yake na uzao wake wote. Maana mbegu anayoipanda ni sumu katika Taifa letu na sasa anaingilia Uchumi wa Watanzania wasio kitu.