Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
My people,
Natambua kabisa bandiko hili halikubaliki kwa wengi wenu na mna haki ya kufanya hivyo kama ambavyo nami nina haki ya kuandika hayaGuys Serikali inaondoka madarakani pale tu ambapo jeshi au majeshi ya Ulinzi na Usalama yakiwa pamoja na wananchi na kujitenga na Dola,hapo ndio mtegemee back up yao
Lakini
Kwa hapa Tanzania hilo halipo kabisa,bado Amiri JESHI MKUU anaungwa mkono kwa asilimia Mia na Jeshi na vyombo vya Ulinzi na Usalama
Na kwa jinsi inavyosemekana muundo wa jeshi letu baada ya mara kadhaa kutaka kupindua Serikali ya Hayati Kambarage Nyerere,likaundwa katika namna ambayo ni vigumu sana kwa CDF kufanya uasi au kupindua Meza
Inahitaji ushirikiano wa vitengo Vinne tofauti kukubaliana kwa pamoja na kupitisha hilo jambo,kitu ambacho ni kigumu kwakuwa Kati ya hao wanne hapo kuna watu wa karibu wa Amiri JESHI MKUU.
Pili mama yenu aliwaambia kwamba nguvu aliyotumia 29 October iliendana sambamba na nguvu ambayo Gen Z waliiitumia,kwahiyo kama mkiamua kuandamana basi mjichagulie nguvu ambayo AMIRI JESHI MKUU atawapimia kwa kiwango ambacho mtaweza kustahamili.
Mama aliwaambia wazungu WHO ARE YOU??
Sasa sijui nyie ni Akina nani mpaka mtake kuingusha dola yake
Msiseme hamkuonywa!!
Ni hayo tu!