Hakuna haja ya kuzalisha umeme wa ziada wakati huu, tuzime mashine za ziada tuhifadhi maji ukame unakuja

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Viongozi wetu wanatuambia sasa mashine 3 kati ya 9 za bwawa la umeme la Nyerere zinazalisha umeme na inavyoonekana mashine 1 hadi 2 zinazalisha umeme wa ziada ambapo ni 235MW kila moja.

Taarifa za TMA zinaonesha kutakuwa na ukame kuelekea mwisho wa mwaka hadi mwanzo wa 2025. TANESCO ili kuepuka mgao umeme wa ziada ungezimwa ili kuhifadhi maji kwa ajili ya uzalishaji wa umeme kipindi cha ukame.
 
Wazo zuri, hivi umeme wa ziada unakuwaje, namba wajuzi mnifahamishe tafadhali,
 
Wazo zuri, hivi umeme wa ziada unakuwaje, namba wajuzi mnifahamishe tafadhali,
Ni mitambo kuzalisha umeme usiohitajika sasa CCM wasipokumbushwa wataacha mpaka maji yaishe bwawani alafu watatuletea siasa zisizo na mantiki yoyote.
 
Ni mitambo kuzalisha umeme usiohitajika sasa CCM wasipokumbushwa wataacha mpaka maji yaishe bwawani alafu watatuletea siasa zisizo na mantiki yoyote.
Du, kumbe ndio hivyo, Yani unazalisha umeme ambo hauutumiii,
 
Mgao ni sherehe kwa wakubwa kupiga pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…