[emoji28][emoji28][emoji28] umenikumbusha mbaliii,hata Mimi kuna kipindi Fulani miaka ya nyuma kidogo kabla sijawa mama, nilikuwaga na boy friend baada ya kuachana naye nikasikiaga wanamsema eti ana ngoma bwana,hiyo hali ilinitesaa sanaaa Kwa muda mrefu,halafu kupima nikiwa naogopa,kweli kidogo niwe chizi sababu ya mawazo[emoji14],ikatokea tu siku moja najisikia vibayaaa,nikaenda hospital,Dkt akanichukua vipimo vingi vingi kumbe alichukua na cha HIV ila hakuniambia,Majibu yalivyokuja akawa ananisomea sikuwa na wazo kabisa kama atakuwa amepima na HIV, basi akanisomea kisha akasema tumepima pia na HIV huna,weuweeee,nilitamani nimrukieee Kwa furahaaa,baada ya hapo nikapona kabisa hata sikuendelea kuumwa,jamani kumbe stress ni mbaya aisee inatesaa maana nilikuwa naumwa vitu havieleweki, na nilipima vipimo vingii hawakuona ugonjwa wowote.Cha ajabu baada ya Majibu hayo nikawa nimepona kabisaaa [emoji28],nanikawa nimejijengea utaratibu wa ku pima kila wakati...Yule Dr aliniokoa bana.