Hakuna jambo baya kama kuhisi umeathirika na unaogopa kwenda kupima

Duh kumbe hadi wewe!??
Mimi hata nikiwa niko njia kuu ila Uoga uko pale pale,mtoa mada amepita mulemule.

Ukawaida usio wa kawaida[emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
mkuu kwani ukisoma soma zile dalili za mwanzo wiki nne hadi sita!! unaonaje.
Mimi sahizi nina kwenda mwezi wa 5 sitaki demu nataka nimalize mwaka kabisa..maana hizo mambo sikia kwa jirani tu
Dalili hizo kama

Koo Kavu

Mafua baada ya wiki mbili tangu ukutane na muathirika (Zinaweza kuwa zaidi ya wiki mbili)

Kupungua Uzito/Kukonda

[emoji23]
 
Hahaha tena mie ndio niko kwenye risk ya kuupata kwa namna nyingi tu....sio mdau wa condom japo ni mzuri wa kushauri watu watumie
Unaposema sio mdau wa condom...Ukiwa na maana??
 
[emoji28][emoji28][emoji28] umenikumbusha mbaliii,hata Mimi kuna kipindi Fulani miaka ya nyuma kidogo kabla sijawa mama, nilikuwaga na boy friend baada ya kuachana naye nikasikiaga wanamsema eti ana ngoma bwana,hiyo hali ilinitesaa sanaaa Kwa muda mrefu,halafu kupima nikiwa naogopa,kweli kidogo niwe chizi sababu ya mawazo[emoji14],ikatokea tu siku moja najisikia vibayaaa,nikaenda hospital,Dkt akanichukua vipimo vingi vingi kumbe alichukua na cha HIV ila hakuniambia,

Majibu yalivyokuja akawa ananisomea sikuwa na wazo kabisa kama atakuwa amepima na HIV, basi akanisomea kisha akasema tumepima pia na HIV huna,weuweeee,nilitamani nimrukieee Kwa furahaaa,baada ya hapo nikapona kabisa hata sikuendelea kuumwa,jamani kumbe stress ni mbaya aisee inatesaa maana nilikuwa naumwa vitu havieleweki, na nilipima vipimo vingii hawakuona ugonjwa wowote.Cha ajabu baada ya Majibu hayo nikawa nimepona kabisaaa [emoji28],nanikawa nimejijengea utaratibu wa ku pima kila wakati...Yule Dr aliniokoa bana.
Ungempa sasa kama asante.
 
Ktk maisha hofu ndio kitu kinatesa na kuleta matatizo mengi kwa watu. Hii ilinitokea nikiwa bado primary, nilipigwa sindano ila dawa haikutoka, nilipoona inachukua muda nikamuuliza dokta kulikoni? Akajibu hii sindano imeziba kwa sababu ya nyama maana ilikuwa kijijini kwa wafugaji huko ndani enzi hizo wanachemsha sindano. Kesho yake nikarudi kumalizia dozi ya sindano tano, nilipofika kwa dokta nikamkuta mama mmoja anamlalamikia dokta kuwa tangu mtoto wake apigwe sindano ameanza kuumwa zaidi na huenda sindano za dokta zimemuambikiza HIV. Kengele ikagonga kichwani, hapo ndipo chemi chemi ya mawazo ilipoaanza.

Nilijiona nami nimeshaambukizwa, nilikosa amani, nyumbani naogopa kusema maana ukimwi ni ugonjwa wa aibu na kipindi hicho unyanyapa ulikuwa mkubwa sana. Nilinyamaza kimya na kubaki na mateso, niliona misha hayana thamani. Nilienda sekondari huko ndiko mawazo yalipokuwa mengi maana haikuwepo tena michezo ya utotoni. Kwa hofu nilianza kupata vidonda, sijui vilitoka wapi. Sikuwa na ujasiri wa kumwambia mtu, nilibaki nalo moyoni, nilibaki kuwa mpenzi wa majarida ya Femina. Nakumbuka kuna toleo moja la Femina lilitoa column moja yenye kichwa cha habari "Silence pain" . Hii ilikuwa ni stori ya dada mmoja alikuwa ameathirika ila hakuwa tayari kumwambia yeyote. Nami niliamua kuchukua falsafa yake , ingawa niliendelea kuumia zaidi. Nikiwa likizo kipindi niko kidato cha tatu, muda wa kurudi shule ulifika nikapewa ada na Mjomba wangu. Nikijiuliza kwa nini nipoteze muda na pesa za mjomba bure? Sirudi shule, kwa hofu nilianza kuumwa usiku huo na kesho yake nikapelekwa hospitali. Nilipimwa vipimo vingi ikiwamo na HIV, majibu yalitoka sina ugonjwa wowote. Nilipumua kwa nguvu na kufurahi, kesho yake nikarudi shule.

Ila baada ya wiki Ibilisi akarudi tena, mara nikaanza kusikia sauti ikiniambia walikudanganya bado una ngoma. Nilirudi kwenye mawazo moja, nilikuwa mtu nisiyejali chochote nilikuwepo tu ili siku ziende. Niliendelea na mawzo hadi kidato cha tano . Nikiwa likizo niliamua liwalo na liwe, nilienda hospitali ya mkoa morogoro na kupima kituo cha ushauri nasaha. Majibu yalikuwa negative, na hapa ndipo nilipopoonea na mawazo mabaya na hofu maana nilikutana na Mama ambaye alinipa ushauri vizuri sana. Alinifundisha mengi na kuniondolea hofu.

Nawashaurini wanajukwaa wenzangu, ukiwa na jambo lolote linalokutatiza maisha, tafuta mtu mmoja mwaminifu na mwambie kuliko kufa na mzigo moyoni, Watu ni dawa, unaloliona mlima kwa mwenzako ni tambarare
 
Kuna kipind nilijua tayar nimewaka sasa siku moja naingia Google naangalia dalili nikaona moja ni Kama mpya hv sijawah kuiskia ambayo ni kusikia mdomo unakua na uchungu flani hv, hazikupita hata wiki mbili nami nikaanza kuona mdomo tayar unapiga indicator ya uchungu. Kudadrekiii nikaona huu ni uboya hyo siku nikanywa pombe zangu za kutosha halaf nikajitosa angaza na mambo yakawa fresh na baada ya siku mbili lile pepo linalo Leta dalili nalo likasepa
 
Bila picha ya VVU na Ukimwi basi uu uzi ni batiri
 
Hii hapa mkuu
images.jpg
 
Usiombe hii kitu uwe nayo kwenye mawazo yako na sana sana uwe unaingia kwenye platform mbalimbali kusoma dalili za huo ugonjwa (VVU na UKIMWI) au tabia zake baada ya kuambukizwa na ukawa una shaka juu ya hizo dalili.

Binafsi niliwahi kudumbukia kwenye haya mawazo (hata ukipitia thread zangu za kitambo utagundua hiko kitu)

Matokeo yake nilipata vidonda vya tumbo na kukonda sana na niliamini kweli nimeupata[emoji23].

Lakini nilichogundua ni kwamba yale mawazo yalikuwa ni source ya mimi kupata vidonda vya tumbo na kukonda. Nikaacha hayo mawazo en nowdays nanenepa tu[emoji23] despite sikuenda kupima na niko na msimamo wa kutokwenda kupima.

Ushauri Wangu Kwa Vijana Wenzangu: 1. Tutake Risk huu ugonjwa upo jamani[emoji3]

2. Hakuna kitu kibaya cha kukiogopa kama uoga wenyewe[emoji871]

Am done unaweza kuongezea [emoji124]
Ninakuelewa sana aisee, hii hali ilinikuta mimi pia na ilinikondesha sana, acha tu
 
Ktk maisha hofu ndio kitu kinatesa na kuleta matatizo mengi kwa watu. Hii ilinitokea nikiwa bado primary, nilipigwa sindano ila dawa haikutoka, nilipoona inachukua muda nikamuuliza dokta kulikoni? Akajibu hii sindano imeziba kwa sababu ya nyama maana ilikuwa kijijini kwa wafugaji huko ndani enzi hizo wanachemsha sindano. Kesho yake nikarudi kumalizia dozi ya sindano tano, nilipofika kwa dokta nikamkuta mama mmoja anamlalamikia dokta kuwa tangu mtoto wake apigwe sindano ameanza kuumwa zaidi na huenda sindano za dokta zimemuambikiza HIV. Kengele ikagonga kichwani, hapo ndipo chemi chemi ya mawazo ilipoaanza.

Nilijiona nami nimeshaambukizwa, nilikosa amani, nyumbani naogopa kusema maana ukimwi ni ugonjwa wa aibu na kipindi hicho unyanyapa ulikuwa mkubwa sana. Nilinyamaza kimya na kubaki na mateso, niliona misha hayana thamani. Nilienda sekondari huko ndiko mawazo yalipokuwa mengi maana haikuwepo tena michezo ya utotoni. Kwa hofu nilianza kupata vidonda, sijui vilitoka wapi. Sikuwa na ujasiri wa kumwambia mtu, nilibaki nalo moyoni, nilibaki kuwa mpenzi wa majarida ya Femina. Nakumbuka kuna toleo moja la Femina lilitoa column moja yenye kichwa cha habari "Silence pain" . Hii ilikuwa ni stori ya dada mmoja alikuwa ameathirika ila hakuwa tayari kumwambia yeyote. Nami niliamua kuchukua falsafa yake , ingawa niliendelea kuumia zaidi. Nikiwa likizo kipindi niko kidato cha tatu, muda wa kurudi shule ulifika nikapewa ada na Mjomba wangu. Nikijiuliza kwa nini nipoteze muda na pesa za mjomba bure? Sirudi shule, kwa hofu nilianza kuumwa usiku huo na kesho yake nikapelekwa hospitali. Nilipimwa vipimo vingi ikiwamo na HIV, majibu yalitoka sina ugonjwa wowote. Nilipumua kwa nguvu na kufurahi, kesho yake nikarudi shule.

Ila baada ya wiki Ibilisi akarudi tena, mara nikaanza kusikia sauti ikiniambia walikudanganya bado una ngoma. Nilirudi kwenye mawazo moja, nilikuwa mtu nisiyejali chochote nilikuwepo tu ili siku ziende. Niliendelea na mawzo hadi kidato cha tano . Nikiwa likizo niliamua liwalo na liwe, nilienda hospitali ya mkoa morogoro na kupima kituo cha ushauri nasaha. Majibu yalikuwa negative, na hapa ndipo nilipopoonea na mawazo mabaya na hofu maana nilikutana na Mama ambaye alinipa ushauri vizuri sana. Alinifundisha mengi na kuniondolea hofu.

Nawashaurini wanajukwaa wenzangu, ukiwa na jambo lolote linalokutatiza maisha, tafuta mtu mmoja mwaminifu na mwambie kuliko kufa na mzigo moyoni, Watu ni dawa, unaloliona mlima kwa mwenzako ni tambarare
Duh,pole Sana,uliteseka Kwa muda mrefu Sana tena ukiwa bado mdogo Sana,hii hali inatesa Kwa kweli,kwanza unaathirika kisaikolojia na kiafya pia, yaani unaona maisha hayana thamani halafu kila wakati wewe una hofuu tuu.Na hali kama hii ikiendelea Kwa muda mrefu Sana wakati mwingine humletea mtu magonjwa makubwa makubwa,au kuteteleka Kwa afya ya akili
 
Mimi ni heri nijipime mwenyewe kuliko kwenye kituo cha VCT, wale watu wanaleta tension zisizo na ulazima kuanzia namna wanavyoongea hadi utoaji wa majibu. Wanadhani ule upole ndo unaotakiwa kumbe ndo unatisha zaidi!
 
Back
Top Bottom