Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
HAKUNA JAMBO GUMU SANA KAMA KUPAMBANA NA MWENYE HAKI
Na, Robert Heriel
Kwa kweli kuna mambo magumu Sana Duniani lakini gumu kuliko yote ni kupambana na Mwenye haki.
Tena kuna mambo rahisi Sana duniani, lakini rahisi kuliko yote ni kupambana na muovu.
Hakuna Jambo rahisi Kama kupambana na mtu muovu.
Mwenye haki hata awe dhaifu Kama nini, lakini anatisha, ana nguvu,
Nilishawahi kujaribu mambo hayo, nilishawahi kupambana na wenye haki ili kujua uzito na ugumu wake.
Kisha nikapambana na waovu katika Hali Ile Ile ya kudadisi ugumu wake.
Ndipo nilipogundua kuwa kupambana na mwenye Haki ni kazi ngumu mno kuliko Jambo lolote Duniani, na hakuna Jambo rahisi Kama kupambana na muovu.
Kupambana na mwenye haki ni kupambana na Nafsi yako. Yaani unapambana na mtu mwenye haki huku roho yako ikikuuma, moyo wako ukijisikia Fedheha, na akili yako ikiwa imechanganyikiwa na hofu kubwa ndani yake.
Kupambana na mwenye haki ni kujishtaki mwenyewe kuwa wewe ni mtu mbaya, ni kujihukumu kuwa wewe haustahili.
Niliwahi kupambana na watu wenye haki, kuwapinga, na kuwaandama; ndipo nikagundua kuwa kuwapinga wenye haki ni kujipinga mwenyewe, na kuwaandama watu wema ni kuiandama roho yako.
Kupambana na mwenye haki ni kupambana na MUNGU.
Kwa maana Mungu ni Haki.
Na hakuna kazi ngumu na isiyowezekana Kama kupambana na MUNGU.
Kumuua mwenye haki ni kujaribu kumuua MUNGU,
Watu wote waliowaua wenye haki basi walijaribu kufanya jaribio la mauaji Kwa MUNGU muumba mbingu na Nchi.
Watu wote tuliowahi kuwapinga na kuwaandama wenye haki, ni wazi tulikuwa tunapingana na kumwandama MUNGU.
Mwenye haki anaogopeka jamani, mwenye haki anatisha jamani,
Niulizeni Mimi.
Mwenye haki silaha yake ni Haki, na ulinzi wake upo Kwa MUNGU.
Mtu muovu silaha yake ni Uovu, ulinzi wake upo Kwa watu wanaomzunguka na Mali alizonazo.
Hujikusanyia walinzi wengi wenye silaha kubwa ijapokuwa hana usalama Kwa maana wamlindao wanafanya kazi bure.
Muovu hujilinda na waovu wenzake,
Lakini kamwe hawezi jilinda mbele ya wenye haki.
Basi nikagundua kuwa Mtu muovu haogopeshi wala hatishi isipokuwa Kwa waovu wenzake.
Hata awe na mamlaka, cheo, au awe tajiri au mwenye sifa yoyote kubwa katika jamii ya wanadamu; Mtu mwovu hatishi,.
Na hakuna kazi rahisi Kama kumuandama mtu muovu.
Nilishawahi kuwaandama viongozi waovu nikaona ni kazi rahisi sana, kuliko kuwaandama watu wema.
Viongozi waovu na Wafuasi wao Jambo kubwa walilonitisha nalo na ambalo hutisha watu ni Mamlaka yao, hutisha kukuua, huwatisha watu kuwafunga jela, hutisha watu kuwafilisi au kuwaletea madhara ya kimwili.
Mtu muovu ndivyo alivyo, na mambo hayo kamwe hayajawahi kumtisha mtu mwema na mwenye HAKI.
Mwenye haki atatishwa ikiwa utamtisha Kwa kumtumia MUNGU.
Niligundua pia, Hakuna watu waoga Kama watu waovu.
Waovu hujitutumua mbele za watu lakini wawapo peke yao hupepesuka Kwa wasiwasi.
Niligundua piah Waovu ndio hujifanya wema mbele za watu, na kuwasingizia wengine kuwa ni wabaya ili wapate sababu ya kuwafanyia mambo Yao maovu.
Kupambana na maovu hutumii nguvu kubwa Kama kupambana na mwenye haki.
Waovu wote wanajua mwisho wao mi mbaya.
Wanajua mwisho wao ni mbaya Kwa sababu walishauharibu.
Mungu ndio mwanzo na mwisho yaani Alfa na Omega.
Muovu akishapambana na mwenye haki kashaharibu Alfa na Omega.
Hivyo hana wakati tena, yupo na atapotea Kama upepo tuu.
Miaka kadhaa iliyopita,
Niliwahi kuwaandikia baadhi ya viongozi wakubwa kuhusiana na dhulma na matendo Yao maovu dhidi ya binadamu wenzao.
Niliwaambia kuwa, Mungu ni mwenye haki na mwaminifu.
Atakuwa mwaminifu katika Maovu Yao Kama alivyo mwaminifu katika wema wao.
Niliwaambia kuwa, Kama watashupaza shingo lazima laana na adhabu Kali kutoka Kwa Mungu itawaandama wao na kizazi chao, kuanzia wao wenyewe , watoto mpaka vitukuu.
Ingawaje nilitoa angalizo pia, laana haitampata mtoto WA muovu ambaye alimkanya mzazi wake mkaidi na mdhalimu.
Lakini kama mtoto alikaa kimya wakati Baba au Mama yake ambaye ni kiongozi akiwa anafanya Maovu Kwa kigezo cha kacheo au vimamlaka mshenzi alivyonavyo, basi Kama Mungu aishivyo laana itawaandama.
Viongozi wote waovu wanalijua hili, kuwa; hakuna Jambo gumu Kama kupambana na mwenye haki.
Hata hivyo kuna kazi ambazo Kama mtu Hatakuwa mwaminifu basi atajikuta akipambana na Mkono wa Mungu Kwa kupigana na wenye haki.
Kazi hizo ni Kama Uaskari Kwa Aina zake, uhakimu au ujaji Kwa Aina zake,
Kazi hizi ni nzuri lakini Kwa sehemu kubwa ukileta mchezo zinageuka kazi za wenye laana Kwa maana wengi wao hujikuta wakishindwa kujizuia Kwa tamaa mbaya.
Kazi hizi ukileta mchezo unaweza jikuta unaipa familia yako laana kisa upuuzi utakaoufanya.
Kazi yoyote ambayo itakufanya uiamini na kuitegemea kama fimbo inayoweza chapia watu wengine hata wenye HAKI ni hatari Kwa maisha yako pamoja na kizazi chako.
Kazi yoyote itakayokufanya ujione wewe ni Bora kuliko wengine, kazi yoyote itakayokufanya uwadharau watu wengine, kazi hiyo jichunge nayo sana.
Ni hatari, ni kaburi, ni Uwanja WA vita yako na MUNGU.
Kazi yoyote itakayokufanya usiwe mnyenyekevu mbele za watu hasa wenye haki, ni Bora uiache. Kazi hiyo ni hatari.
Mwisho, hakuna kazi rahisi Kama kupambana na muovu hata angekuwa anacheo gani.
Lakini hakuna kazi ngumu Kama kupambana na mwenye haki hata angekuwa yupo Hoi taaban kidaraja au kimaisha.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro