safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Huu sio uamsho haya ni malalamiko tu.Tokea Uhuru hakuma mradi wowote wa maendeleo ulioanzia mikoa ya kusini mwa tz . Kusini imekuwa nyuma na ya mwisho kufikirika ktk kila mradi. Miaka 25 - 30 iliyopita serikali ilijinadi kuwa hauna uwezo was kupoleka maendeleo kwa kila mkoa kwa wakati Mmoja. Na kwakua ilikuwa ndio miaka 30 tokea Uhuru wananchi was kusini walikuwa na matumaini kuwa Siku zao ya kupelekewa maendeleo. Hata hivyo walikaa tens miaka 20 zaidi ndipo wakaambulia kupata barabara ya lami inayounganishana jiji la dar.
Ule usemi kuwa serikali haihangaiki na jamii zilizo lala nakubaliana nao kwa asilimia zote.
Miradi yote mikubwa ikiwemo hospitali ya rufaa kusini hakuna tokea Uhuru
Chuo kikuu au tawi lake hakuna tokea Uhuru
Kuna mradi huu wa reli SGR kusini hawafikiriwi kabisa wakati kanda nyingine hii wakipelekewa awamu ya pili ya reli. kusini sio tu hawajafikiriwa lkn wenyewe pia hawajitambu, wamelala fofofo.
Ukweli ni kuwa jamii yangu ya watu was kusini wanafurahisha na wanasikitisha na wanahitaji maombi ya haraka kutoka kwa watz.
Wanafurahisha na kusikitisha kwasababu; kusini ndio jamii pekee ambayo ccm inavuma kura nyingi wakati wa uchaguzi na huwa ni watu was mwisho kupelekwa maendeleo na serikali hii ya ccm.
Unaweza kuuliza kuna faida itapatikana ikijengwa reli kusini.
kuna rasilimali na bidhaa muhimu ambayo kama ingesafirisha kwa reli bidhaa hizo zingenuaisha watz walio wengi. Bidhaa hizo no pamoja na cement ambapo kwasasa kina zaidi ya maloli 1000 na hivyo kupelekea barabala ya lami kushindwa kuhimili uwingi na ujazo was maloli endapo kiwanda kingezalisha ktk uwezo wake halisi, kuna makaa ya mawe kuna uranium ambazo michakato ya uzalishaji bado inasuasua. Bila shaka uwepo was reli umgesisimua miradi hii mikubwa.
Jana Mh SSH ameshuhudia utiwaji saini mkopo was pesa kwa ajili ya wa ujenzi wa SGR kipande cha tatu kutoka Makutupora hadi Tabora chenye urefu wa kilometa 368, kitakachogharimu Dola za Kimarekani 1.908 Bilioni sawa na Sh4.41 trilioni kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Yapi Merkez kutoka Uturuki.
Mkopo huu ambao kwa ujumla wake no zaidi tri 14 watu wa kusini watakuwa in wasindikizaji na walipaji wakuu wa deni hili lisilo na faida yyt kwao.
Sijaja hapa kulia lia kama watz wengine bali huu in Uamsho kwa kwa waliolala fofofo. AMKENI
Kumuambia mtu kwamba "aisee wewe ni mjinga saaaaana" hapo hujamtoa ujinga bali muambie wewe ni mjinga kwa sababu hii na hii na dawa ya kuondoa fanya kadha wa kadha.
Sasa wewe hujawaamsha lolote bali umewaambia tu kwamba wamelala baaasi.
Weka mikakati namna gani wamelala,weka mikakati wafanyeje ili WATOKE HAPO WALIPOLALA ?
JE waibe ili watoke kwenye huo usingizi fofofo ?
Waingie kwa fujo kwenye siasa ili watoke kwenye usingizi fofofo ?
Wahame wote wahamie Dar ili watoke kwenye usingizi fofofo ?
Wafanyeje mkuu ?