Hakuna jamii iliyolala Tanzania kama watu wa kusini

Huu sio uamsho haya ni malalamiko tu.

Kumuambia mtu kwamba "aisee wewe ni mjinga saaaaana" hapo hujamtoa ujinga bali muambie wewe ni mjinga kwa sababu hii na hii na dawa ya kuondoa fanya kadha wa kadha.

Sasa wewe hujawaamsha lolote bali umewaambia tu kwamba wamelala baaasi.

Weka mikakati namna gani wamelala,weka mikakati wafanyeje ili WATOKE HAPO WALIPOLALA ?

JE waibe ili watoke kwenye huo usingizi fofofo ?
Waingie kwa fujo kwenye siasa ili watoke kwenye usingizi fofofo ?
Wahame wote wahamie Dar ili watoke kwenye usingizi fofofo ?

Wafanyeje mkuu ?
 

Mimi nafikiri watu wa kusini ni watu wazuri sana.

Ni kweli wamesahaulika sana. Ni waaminifu, waadilifu, wazalendo simple sana.

Wakipata Elimu wataisadia sana hii nchi. Tatizo hii nchi haijawekeza vya kutosha kusini.

Vyuo vijengwe, elimu isisitizwe unajua nina interest za kutosha huko, nimesaidia kujenga shule, hospitali.

Naongelea na mama ntilie ananiambia sasa nafanyaje kijana wangu hataki kwenda shule, naongeo na mtoto anasema shule is boring.

Muhimu kufanya shule ziwe zinawafunza watoto/ vijana wa kiume vitu vyenye faida ya moja kwa moja.

Mfano kujifunza kilimo cha kisasa, kutumia mbolea sahihi,trekta masoko.

Muhimu zaidi ni elimu ya pesa. Financial literacy. Sababu wengi wao sio maskini kivile,hawajui kutumia pesa.

Pia kufundisha kusisitiza umuhimu wa Familia. Baba, mama, watoto kukaa pamoja. Wanawake wanachacharika sana, wanaume wanaendesha wakipata pesa kulewa,kuzalisha,kutojali, wanasepa.
 
Hizo fikra zitafanyiwa Kazi? Tunasubiri na Sisi tutoe Rais atujengee uwanja WA ndege WA kimataifa, mbuga na mahoteli....Mungu ni wetu sote.
Siku nikija kuwa raisi watu wangu wa kusini nitahakikisha nafanya kila ninaloweza wakulima waneemeke aisee,kule wazazi wengi wetu ni wakulima,wanaumia sana inauma sana aisee.

Tunatakiwa tuangalie mahitaji ya wananchi wa eneo husika,watu wa kusini asilimia kubwa shida yao ni kuboreshewa kilimo chao wauze kwa bei nzuri,soko la uhakika pamoja na barabara,maji yapatikane kwa urahisi kwa wananchi,huduma za afya bora kabisa ikiwemo na elimu juu ya kujiwekea akiba yao ya maisha,haya kwa wana kusini wengi ni muhimu kuliko ndege.
 
Mkui Korosho inaingiza pesa nyingi nchini kuliko Mchele,kahawa, pamba, katani combined.

Ni kweli serikali imejisahaulisha sana na maendeleo ya kusini. Wana haki ya kulalamika

..100% malalamiko yao ni ya msingi.

..mimi hoja yangu ni kwamba wawe na plan B, na plan C.

..wahangaikie miradi ambayo inaongeza kipato cha mwananchi mmoja mmoja.

..naangalia jamii kama ya Wakinga ambao wameibuka bila msaada mkubwa toka serikali kuu.

..wakati mwingine miradi mikubwa mikubwa huwa haigusi wazawa wa eneo husika.

..mimi ningekuwa mwenyeki wa kusini nisingelilia tujengewe chuo kikuu.

..Kilio changu kungekuwa kuanzishwe elite secondary / technical school walau 2 kila mkoa kwa ajili ya wananchi wa kusini.

..kuna maana gani kuwa na chuo kikuu halafu wenyeji wa mkoa husika hawako-represented ktk jumuiya ya wanafunzi kwasababu wanafeli kwa maelfu ktk shule za sekondari?

..Sipingani na dhima nzima ya mtoa mada. Naomba nisieleweke vibaya. Ninachojaribu na kupanua wigo wa hoja yake.
 
Watu wa kusini kwanza maeneo sio shida ya kujenga,watu wa kusini ni matajiri wa ardhi,ni ngumu sana kukuta watu wamepanga labda wa kuja.kwa msingi huu sehemu ya kukaa kwa wana kusini sio tatizo.

Tatizo letu wana kusini tunatumia tusivyozalisha,na tunazalisha tusivyotumia.

Hatuwazi akiba kabisa.
Si alipatikana 'Che Nkapa' mbona hakufany hayo?
Ndio maana mimi sikubaliani na kusubiri huruma ya raisi.

Watu wa kusini wengi wanatoboa wakati walishatoka kwao kitambo sana,ukiuliza majaliwa ametoka lini ruangwa itakuwa historia,mkapa itakuwa historia,so mtu maconenction yote anayapata town.

Hata kikwete ameishi sana kule nachingwea na anajulikana na wazee wa pale,ila katoka lini ni kitambo kidogo.

Mimi naona wana kusini walioko kusini sasa hivi wanaishi hapo waingie pia kwenye siasa ili iwe rahisi wakipata ukubwa kukumbuka wanapoishi na sio kukumbuka wanapotoka.
 
Wakipata nafasi kubwa za uwakilishi au kisiasa wanahama kabisa.
Ukiachana na yule muhindi wa Mtwara (Murji sijui Sinani) aliyekuwa mbunge enzi za Mkapa niambie wale weusi wazawa wa majimbo yote ya kusini toka uhuru hadi leo kama walijihiimarisha maisha yao majimboni kwao.
 
Ndanda high school ipo kusini ni A level.

Mtwara tech ipo ni high school pia lakini idadi ya wanakusini wanaofaulu hapo hairidhishi.

Wengi wanafeli sana,na hapa ndipo linskuja suala la kwamba wana kusini wengi hawajaamka katika elimu,na laiti wakiamka basi tutaona kwamba ipo haja ya kujenga hayo mavyuo.

Ila kwa sasa vyuo sio hitajio la haraka,bali haraka sana sasa hivi watu waelimishwe na kuhamasishwa kusoma ili hivyo vilivyopo vitumike vizuri sana.

Nakupa mfano mimi nilipohitimu kidato cha nne darasa lwtu lenye wanafunzi zaidi ya 100 waliopata kwenda A level ni watu hawafiki 15.

Can you imagine waliobaki wako wapi ?

Hawa waliofaulu walipata hamasa ya kusoma,na waliofeli ni uzembe wao kwa sababu wenzao wamefaulu eneo lile lile walilokuepo wao.

Hivyo suala la kuongeza vyuo na mashule naona sio la haraka japokuwa linahitajika ila sio kwa sasa kwa maoni yangu
 
Hahaha mkuu hizo ni katika mbinu na mikakati,pengine zisiwe fanisi kufikia lengo maana kila mtu ana utashi wake.

Ila ipo siku watu wa kusini watakuja kufanya wonders sio kwa sababu ni wa kusini bali ni kwa sababu ya vijana wengi wenye uchungu na maendeleo ya huko
 
Kwani hujui zao la korosho kwa Tanzania linaongoza kulimwa wapi
 

Nakubaliana na wewe 100% ardhi, utajiri upo tele. Kila familia ina ardhi eka kibao za mikorosho ya kurithi. Ardhi inakubali mazao kibao, maparachichi, karanga, mifugo you name it inakubali.

Kila mwaka kuanzia November wanapata zaidi ya miliioni 10 hadi 100. Zinaisha zote April.

Wanaanza kutegemea mikopo, kangomba. Sasa ukitoa elimu ya pesa itasaidia sana kujipanga.

Lindi ina bahari safi sana clear, clean blue ocean, bora kabisa duniani.


Sio mbali kuna mbuga za maana, muhimu zaidi. Muhimu mipango.
 

..Good.

..nimekusoma kwamba idadi na viwango vya ufaulu lazima viongezeke.
 
Lakini kuwepo kwa vyuo kunaleta maendeleo na mzunguko wa pesa unakuwa mkubwa kama ilivyo dodoma kwa sasa mji unachangamka sana.
 
Sasa kama watu wake ni wajinga utawasaidiaje? acha CCM iwatafune, Mkapa alikimbilia Lushoto alijua hawezi kuishi na watu wajinga.
 
Kusini kumesahaulika kwa kweli. Hata huduma muhimu kama umeme na maji bdo hazijasambaa kwa wqnanchi wengi.

Chukua mfano wa wilaya ya Mbinga mjini. Badhi ya maeneo yaliyo ndani ya mamlaka ya mji hayana hata umeme.

Na jinsi watumishi wa maeneo hayo walivyojisahau, kusini kutaendelea kuwa nyuma kwa miaka mingi ijayo.
 
Nilipita huko[emoji23] mnaitia aibu

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Tungependa useme Watz karibu wote tumelala na hata wale wajamja wachache wanapiga mihayo walale kutokana na hilo..
Ila hatujajuwa ni kiasi gani tulivyolala labda mpaka tuchepuke kwa wale wa Dunia ya kwanza, ukweli unauma ila ndio hivyo..
 
Huko nyie ni wateja wazuri wa CCM na CCM inapenda sn watu wajinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…