Njia za utulivu ni kutafuta njia ambazo wananchi watakuwa na uwezO wa kuamua jambo lao bila ridhaa ya serikali.
Mfano mfumo wa majimbo ni mpaka serikali itake kwma haijataka huwezi fanya lolote lile hata kama wanancho wote wameliwafiki.
Solution zitafutwe njia ambazo hata bila serikali basi njia hizo zinatekelezeka bila shida yoyote.
Kuna mikoa haina mfumo wa majimbo na bado wamenyookewa tu na miji inaenda vizuri.
Kama mikoa hiyo imeweza kuendelea bila mfumo wa majimbo maana yake kuna njia zilitumika zisizokuwa hizo za mfumo wa majimbo,basi na sisi tuzotumie hizo ama tuboreshe zaidi ya hizo ili tufikie levo ya uafadhali.
Maendeleo kusini bila majimbo inawezekana kama ambavyo maendeleo bila majimbo imewezekana mikoa mingine.
Nadhani niseme nimeshindwa kukushawishi ili nawe ushawishi
Wengine..
Labda nikueleze kwa kutumia lugha ya kiuchumi kueleza faida ya serokali ya majimbo ktk zama hizi na kwa jamii ya watu waliolala.
Ni hivi nchi yetu imeingia ktk uchumi wa kati wa chini (lower middle-income economies - those with a GNI per capita between $4,046 and $12,535 (2021). Uchumi wa kati wa chini ni maana wake wasatani wa pato LA mtu mmoja mmoja ni laki 7 kwa mwexi. wenye uhakika was kupata walau sh laki 7 kwa mwezi. Kwa tz watu hao ni waajiriwa peke yao. Ajira za serikali kwa zaidi ya 90% kusini zimechukuliwa na wageni. kwa Mikoa unayoona imepiga hatua ya maendeleo ni ile ambayo INA vijana waliojiriwa na seikali na sekta binafsi. Kwa maana kwa makusudi serikali iliamua kuweza huko ktk elimu, afya viwanda nk
Na kwa makusudi serikali iliwabaguabaadhi ya kanda ikiwemo na kwa kiasi kikubwa ya kusini. Nafasi za kazi serikali 90% zikachukuliwa na wageni. Sio kwa sababu vijana hawana weledi laa, kwasababu ajira wanapeana kwa kujuana na Sera ya nchi ya ajira inaruhusu kufanywa wanayofanya.
Suala LA pili muhimu ni hili.... Jamii yyt ikitaka ijikwamue na isonge mbele lazima iwe na mirija yakuingiza pesa. Mfumo was serikali kuu umekata mirija yote ya kuingiza pesa kwa halmashauri. Matokeo yake mapato yote ya serikali yanakwenda hazina kuu na rais na ndie anaeamia wapi ziende sh ngapi.
Kwa vigezo hivi viwili nakwa jamii iliyolala kutaka kupita njia ambayo jamii iliyoamka imepitia tens kwa nguvu na maamuzi ya kisiasa.Nanyi mpite bila ya kutumia nguvu ya kisiasa ni kanuni isiyokubalika.
Ni Serkali ya majimbo ndio itaweza kutupitisha njia hiyo.
Serikali za majimbo hupewa nguvu na Uhuru zaidi huwalazimu 75% ya ajira kipaumbele wanapewa wazawa was kanda husika ktk nafasi zote nyeti. Mfano huo unaweza kuona ktkserikali ya jimbo LA znz katiba ya Kenya na nigeria. Hii inamaana kwamba serokali ya majimbo italazimisha mchakato wa ajira uangaliwe upya kwa kusinu utakuwa na manufaa makubwa kwao hivyo nao kuweza kuendeleza miji yao.
Serikali ya majimbo inapewa nguvu na mamlaka ya kukusanya mapato na 75% hayo yatumike ndani jimbo/kanda. Na 25% yanakwenda serikali kuu.
Bado tu huoni faida ya serokali ya majimbo na kuanziaha jukwa litaloelimisha na Kuhamasha wanakusini na watz kwa ujumla kipindi cha uchaguzi kupiga kura na tuchague chama ambacho kitabadili muundo wa serikali kutoka serikali kuu hadi serikali za majimbo yenye Uhuru zaidi was kujiamulia mambo yao wenyewe