Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hip hop ni ukweli tupe WATANZANIA ukweliWatanzania woote tu tumelala, ndio maana viongozi wanafanya wanavyojisikia.
Nchi inapelekwa pelekwa kama meli iliyokosa nahodha.
Kaka wazo lako zuri sana na linatekelezeka vizuri ikiwa serikali yenyewe itaamua vizuri kufanya hivyo kutokana na misukumo mbalimbali.Kaka wazo lako zuri sana na linatekelezeka vizuri ikiwa serikali yenyewe itaamua vizuri
Nakubaliana nawe. Nilikwenda arusha eneo la mgaramtoni, nikaenda tena merarani. Pale vijiji kwa ktkt karibu na KIA, Ukweli nilijistukia, nikasema kweli tz ni kubwa na kwa mfumo huu wa serikali kuu unaolazimisha watz wote wawe na tamaduni moja, vazi moja la taifa haitowezekana. Faida moja ya serikali za majimbo ni kukuza tamaduni za kila eneo. natamani kwa mfano kila mwezi jiji la arusha litenge siku moja kwa mwezi au mwaka kuvaliwe vazi la kimasai ambalo kwass linapoezwa ka sehemu ya kuenzi na kukuza tamaduni ya kimasai. Ukweli ni kuwa kusini na kastazini ni sawa na Qatar na Dubai. Qatar wanategemea gesi na qubai wanategemea utalii. Uliza sasa nano anapaswa kuwa tajiri. Pia jiulize kati ya misri na SA gn ni tajiriKuna Mzee wa mmmoja alinipa ushauri na nakwambia leo chukua hii;
Popote utakakuwa kulingana na Jiografia utakayoikuta usikae eneo la Kusini lina Mambo yake.
Mfano.
Tanzania Kusini kuna Lindi, Mtwara nk. Ambayo huwezi linganisha na Arusha na Kili vya Kaskazin
Bara la Afrika Kusini kuna Swaz, Zimba, Tanza, SA nk ambazo kamwe huwezi zilinganisha na Egypt na Morroco za Kaskazin
Mwili wa Binadam kusini kuna Nyayo, visigino nk ambavyo kamwe huwez linganisha na Kichwa kule Kaskazin.
Hata kwenye Kijiji chako eneo lililo Kusini ni Maskini na lina mambo ya ovyo ovyo kulinganisha na Kaskazini
Kwa vile tupo katika kubadilishana mawazo basi naomba uwe unasoma kwa utulive sana kile ninachokiandika.Nazidi kujifunza kutoka kwa kundi la watu tena wenye uwezo kufikiri kuwa na wao wanaamini kuwa jukumu la kufikiri na kufanya maamuzi kwa niaba ya makundi mengine si lao Bali kuna kikundi maalum (watumishi wa Seikali)
Nimesoma ila nahisi husomi ninachoandika ama unasoma nusu nusu ama hujaelewa hoja yangu mkuu.Kaka wazo lako zuri sana na linatekelezeka vizuri ikiwa serikali yenyewe itaamua vizuri kufanya hivyo kutokana na misukumo mbalimbali.
Nazidi kujifunza kutoka kwa kundi la watu tena wenye uwezo kufikiri kuwa na wao wanaamini kuwa jukumu la kufikiri na kufanya maamuzi kwa niaba ya makundi mengine si lao Bali kuna kikundi maalum (watumishi wa Seikali). Nasema ni watumishi wa serikali kwa kuwa watu wengi wanapozungumzia Serikali wana maana ya mile kikundi cha watu wanaohudumu ktk serikali ilio madarakani ikiongozwa na raid na waziri mkuu.
Na kwamba mabadiliko yyt wanayoyahitaji wao wataendelea kuyasubiri hadi pale kikundi hicho (wahudumu wa Serikali) watapoamua kufanya mabadiliko hayo. Lkn ukweli ni kuwa serikali nu sisi wananchi na wale tunawatuma nini wafanye kwa niaba yetu. na wasipofamya tunayo nguvu ya kuwawajibisha. Kwa kuwaondoa wale na kuwaweka wengine ambao wanaongea kwa niaba yetu.
Kuisuburi serikali iliyo madarakani kutoa idhini kwa jamii kwa kuruhusu kufanya mabadiliko ni kutojua wajibu wetu kama jamii.
Binafsi nilidhani tunahitaji jukwaa ambalo litakuwa na kama sio waanzilishi basi wawakilishi kutoka kusini. Dunia imebadilika, siasa za miaka 30 iliyopita si za sasa.
Siasa za sasa lazima uwe ni sehemu ya wafanya maamuzi wa taasisi iliopo. Siasa za sasa n kuonyesha nguvu yenu na uwepo wenu kama wananchi ni muhimu.
Kuwa na taasisi/jukwaa/chama kitachojimbanua kujinadi kwa sera zinazosimamia uhuru wa wajitawala dhidi ya Sera zinaopinga.
Jamii inayokosa jukwaa la kujitambulisha ni jamii iliyolala. Na jamii au wananchi waliolala wataendelea kulazwa na watawala. Kwani kazi kubwa ya watawala ni kuwafanya Wananchi waliolalala walale zaidi.
Jukwaa litakalotoa nafasi ya majadiliano na kufikia muafaka baada ya kujadili na kupembua na kuainishisha mahusiano yao, matatizo yao juu ya siasa, uchumu, utamaduni nk
Lkn kwa kuwa jamii yenyewe ni ya watu wanyonge na basis Kuna haja kwanza ya kuwekeza ktk mambo ya kisaikolojia kwa jamii hii wajitambie kuwa wao so wanyonge bali ni wenye thamani.
Ili waelewe thamani yao,
Wajihisi nao wanapaswa kufanya maamuzi yenye maslahi kwao kama mtanzania nchini.
Waachane na ile dhana kuojiona ni mwenye wasiofaa kusikilizwa.
Kama mtu asiye na hadhi ya watz. Na kutojifikia na kujinyanyapaa na kutojiamini.
hali hii ndio inayonifanya nifikirie kuna haja ya kuanzisha jukwaa letu. Huko kwengine wakilihitaji hatutowazuia. Lkn chombo hicho kijikite zaidi kusini, kama Act znz na Chadm Arusha na moshi. Hii ndio njia pekee rahisi ya kuiondoa ccm
Ukija kupata tu unabadilika wew ,si unaona hawa tuliokuwa nao wananchi wanalia kuhusu bei ya korosho Kumbe wao ndo wanakampuni zao wananunua hzi korosho tena matani kwa matani ,hakuna hata mbunge anayepgia kelele bei za korosho bt mbaya zaid viongozi wa huku wameshindwa hata kuwatetea wananchi wao kuhakikisha ule mzigo wa korosho wote unasafirishwa kupitia Ile bandari ya mtwara ambayo muda. Si mrefu imefanyiwa maboresho ili angalau kuwepo kwa fursa za msimu bt mwishon unasikia korosho nying zinaenda Dar na kuwaacha wananchi midomo waziSiku nikija kuwa raisi watu wangu wa kusini nitahakikisha nafanya kila ninaloweza wakulima waneemeke aisee,kule wazazi wengi wetu ni wakulima,wanaumia sana inauma sana aisee.
Tunatakiwa tuangalie mahitaji ya wananchi wa eneo husika,watu wa kusini asilimia kubwa shida yao ni kuboreshewa kilimo chao wauze kwa bei nzuri,soko la uhakika pamoja na barabara,maji yapatikane kwa urahisi kwa wananchi,huduma za afya bora kabisa ikiwemo na elimu juu ya kujiwekea akiba yao ya maisha,haya kwa wana kusini wengi ni muhimu kuliko ndege.
Kifupi ni hivi. Chama kupitia ajenda na ilani zao zinapaswa kujinadi kupitia mikutano na makonganamo. Ilani na Sera zao zikikubalika kwa wananchi, chama hicho hupigiwa kura na kuunda serikali.Kwa vile tupo katika kubadilishana mawazo basi naomba uwe unasoma kwa utulive sana kile ninachokiandika.
Mimi ninachosema ni kuwa kwa sasa utaratibu wa kinchi ulivyo,kuna mambo wewe kama mwwnanchi huwezi kuyaamua mpaka serikali itoe idhini ya jambo hilo.
Mfano wa mambo hayo ni hili suala la serikali ya majimbo ulilolisema,hili suala hata kama wananchi wakaamua kwamba wanataka serikali ya majimbo maadanu serikali haijaamua hiyo seikali ya majimbo haiwezi kutokea kamwe.
Sasa kwa kuwa mpaka serikali iamue kufanya ndio litafanikiwa basi sisi jukumu letu wananchi tuendelee kupigia kelele hiyo serikali ya majimbo lakini pia hiyo isiwe ndio njia tunayoitegemea pekee kwa ukombozi wetu,bali tuwe na njia zingine ambazo njia hizo hazihitaji mpaka serikali itoe idhini na ifanye kama kule kwenye serikali ya majimbo.
Kusema
Hakuna haja kukumbatia chama Kama bendera kufata upepo. Kipindi Fulani nilikwenda kufanya kijiutatfiti kwa kuwauliza kwann mmetoka CUF na kwenda ACT wengi walijibu tumemfata Maalim . nikawauliza maalim akishinda urais znz jamii ya watu wa kanda ya kusini mtafaidika vp urais wa Maalim Seif (Mungu Amrehemu) hawakuwa na jibu. Hawakuwa na jibu kwa kuwa Maalim seif alijipambanua kuwa anapigania Uhuru zaidi wa znz kujiamulia mambo yao wenyewe.
Hivi kuna kabila limeenea nchini kama wachaga na wasukuma?..itakua huijui hii nchi.Mbona miradi ya maendeleo kusini ipo tena hata zaidi ya kaskazini? Huyu aliyeandika huu uzi anaendaga kusini kweli. Barabara kutoka Dar-Lindi-Masasi-Mtwara lami. Barabara kutoka Masasi-Tunduru-Songea lami. Kutoka Songea-Mbinga-Mbamba Bay lami. Songea-Njombe-makambako-Mbeya lami tena ya siku nyingi. Wilaya ya Nanyumbu ina stand ya kisasa(Mangaka), Songea wana stand ya kisasa(Shule ya Tanga). Njombe wana stand na soko la kisasa. Wakati mkoa kama Manyara ni vumbi tupu. Hakuna stand wala soko. Wilaya ya Mbulu ambayo mji wake ulijengwa na wajerumani tangi 1905 mpaka leo ni vumbi. Wilaya za Kieto na Simanjiro vumbi. Mi naona wamejengewa miundo mbinu mizuri kuliko kanda zingine. Ninachokiona ni wapole siyo waongeaji wala siyo watu wa sifa mfano km wachaga, wana ushamba flani hawatembelei maeneo mengi wao wanajua Tanzania ni Dar ukiuliza habari kwa mfano ya Arusha hajui chochote anaweza kukuambia Arusha ni kubwa kuliko Dar Es Salam..
Kwahili nakupinga..mbona south Africa ipo kusini ila inamaendeleo makubwa kuliko somalia ai congo iliyopo kaskazini..pia kwa marekani ya kaskazini southerners ndio eneo lenye maendeleo makubwa kuliko northerners? Unaliongeleaje hili?Kuna Mzee wa mmmoja alinipa ushauri na nakwambia leo chukua hii;
Popote utakakuwa kulingana na Jiografia utakayoikuta usikae eneo la Kusini lina Mambo yake.
Mfano.
Tanzania Kusini kuna Lindi, Mtwara nk. Ambayo huwezi linganisha na Arusha na Kili vya Kaskazin
Bara la Afrika Kusini kuna Swaz, Zimba, Tanza, SA nk ambazo kamwe huwezi zilinganisha na Egypt na Morroco za Kaskazin
Mwili wa Binadam kusini kuna Nyayo, visigino nk ambavyo kamwe huwez linganisha na Kichwa kule Kaskazin.
Hata kwenye Kijiji chako eneo lililo Kusini ni Maskini na lina mambo ya ovyo ovyo kulinganisha na Kaskazini
Niliamini kabisa kuwa CCM imemtumia Membe MTU wa kusini kugawa kura za wapinzani. Hivyo binafsi nilipenda wangeenda Chadema.Sasa mkuu kwanini unakua na wivu na wao kuwa wafuasi wa Maalim Seif na kuwa ACT? Ulitaka waende Chadema? au CCM?
Wapinzani ni lazima wasimamishe mgombea mmoja ili kupambana na CCM, Chadema ni ngumu sana kui overtake ACT mikoa ya kusini na Pwani, Maalim Seif alikua ni Taasisi, Alikitengeneza CUF ki ideology za kibingwa kabisa, Lipumba ndie akaja kuwa failure kwenye kukiendeleza chama, Chama kilipoteza dira njiani Lakini zile ngome kuu kabisa zika survive, Na Maalim Alipotoka CUF na kungia ACT CUF ikapotea na ACT ikaibuka.Niliamini kabisa kuwa CCM imemtumia Membe MTU wa kusini kugawa kura za wapinzani. Hivyo binafsi nilipenda wangeenda Chadema.
Niseme tu kwamba siamini kwamba wananchi wanaweza kuwa pamoja huku wakiwa na vyama tofauti na kila chama kina ajenda yake.Kifupi ni hivi. Chama kupitia ajenda na ilani zao zinapaswa kujinadi kupitia mikutano na makonganamo
Hapa utawagawa wananchi kwa sababu ukiunda chama tu maana yake unawavuta watu na kuwagawa kiuvyama uvyama.Ilani na Sera zao zikikubalika kwa wananchi, chama hicho hupigiwa kura na kuunda serikali.
Hiko chama kingine unachosema mkuu kitakuwa na wafuasi wana kusini,na Ccm kitakuwa na wafuasi wana kusini hapo maana yake umewagawa wanakusini wale wale katika mapande mawili na sisi lengo tuwapate wanakusini wote katika kundi moja wakiwa na usemi mmoja wa serikali za majimbo.Na kingine kije na serikali may b 8 za majimbo zenye kuwa na nguvu na Uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe.
Kumbuka pia kuna watu wana vyama vyao wataipinga hiyo hoja kwa sababu tu sio chama chao,na wewe ni shahidi kuna chama kina hoja nzuri lakini watu wameingiza ushabiki wanapinga hoja hizo na kweli chama kinaonekana hakina maana hakuna wafuasiNaamini chama hicho kitakubalika kwa kanda ya kusini. Na bila shaka majimbo mengine nchini.
Ninachoamini ni kwamba suala la CCM kutoka madarakani ni jambo linalowezekana.Au huamini kuwa siku moja ccm itatoka madarakani?!?!
Ngoroso sio zao mkuu?..wekeni jitihada kwenye KILIMO.
..hakikisheni mnayo mazao ya muda mfupi, na muda mrefu...