Hakuna jamii iliyolala Tanzania kama watu wa kusini

Hapo CCM kuvuna Kura tutake radhi, unalijua vibe la CUF kusini? Au bado ulikuwa hujaanza kufatilia siasa? Unawajua chadema tu?
Anyway tulishazoea kubaguliwa tangu enzi za Mwalimu, na reli aliing'oa....kikubwa uhai tu, wote tunavuta pumzi moja.
Em ona tu kila kiongoz anavyo ng'ang'ana kujenga kwao, lakini kwa mwalim pako ovyo. Pengine ni nature yetu sio kwamba tumelala

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Naunga mkono hoja nakumbuka siku moja nilimsikia hayati magufuli akitokea lupaso kumzika mkapa aliongelia hiyo hoja kwanini kusini kuchelewa kwa maendeleo na miradi yote ya maana Mikoa ya kaskazini & magharibi alijitetea ujinga eti namnukuu alisema kuchelewa kwa maendelea kusini kulichangania na harakati za kupigania uhuru kwa nchi za kusini musimbiji na afrika kusini ili kuwazuia makaburu wasifike dar kwa urahisi kuja kuwauwa wanaharakati wa afrika kusini na msumbiji hivyo serikali ya nyerere ambayo ilikuwa inawsaidia wanaharakati hao na kuwanusuru wasiuwawe ndio wakaaamua kusitisha maendeleo kusini yaan miundo mbinu kwa sana na elimu kiasi kwa kweli baaada ya kusikia hayo nafsi iliuma sana.lakini naamini hipo siku nasi kusini tutakuwa juu maaana kile kizazi cha waliolala sasa ni wazee kitakwisha sio muda mwingi kuanzia sasa
 
Kama n kwel bas nyerere alikuwa hayawani kabisa yaan alikuwa radhi kuona watu wake wakipata tabu sababu ya wageni

Ujamaa kweli ulikuwa n ujinga na upumbavu uliokomaaa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Niseme tu kwamba siamini kwamba wananchi wanaweza kuwa pamoja huku wakiwa na vyama tofauti na kila chama kina ajenda yake.

Hapa utawagawa wananchi kwa sababu ukiunda chama tu maana yake unawavuta watu na kuwagawa kiuvyama uvyama...
Moja ya faida ya jambo letu hili tuna Uwezo mzuri wa Kufikiri. Na tunafikiri ktk pande zote hasi na chanya.

Moja ya faida ya wazo hili kufaulu kwake ukiweka uzani wa kufaulu au kufeli. Kufaulu kuko kukubwa. Na sababu kuu tatu ambazo hujaifikiria ni kuwa kukubalika kwa vyama vyote vilianzia kwenye ukanda kwa kutumia nguvu za viongozi wa kijamii. Vyama vyote vilivyoanzisha vikiwa na ajenda ya utaifa vilibaki kuwa in vidogo vidogo.

Jambo LA pili muhimu ni kuwa
tathmini ya kawaida kabisa inaonyesha ccm inazidi kupozeta nguvu na hasa kipindi hiki cha SSH kutokana na mgawanyiko was ukanda ndani ya chama. (Fursa).

Tatu kama tutaamua kufikiria mbali badala ya mbele tutaona kuna haja ya kutengeneza mwanasiasa was kikanda ambae yeye atakuwa no kamaanawakilisha kanda husika ambapo kwa sasa hatuna mwanasiasa was aina hiyo kusini.

Kwa hiyo ktk jambo lolote linalohusu jamii vikwazo haviepukiki Bali muhimu ni kufocus ktk jambo lenu.

Kwa kuanzisha majukwaa litakalotambulisha uwepo wetu.

Binafsi nakubaliana na wanaosema tuhamasishane ktk maendeleo ya MTU mmoja mmoja tukazanie elimu but my friends hayo yote huwa in rahisi kupitia nguvu na vuguvugu za kisiasa. Kwa kudai pia kipande chetu cha keki ya taifa tunachonyimwa. Vuguvugu za kudai uwekezaji was miradi sio inayodhaminiwa na serikali hasa kuoitia miundo mbinu sisi kama walipa kodi lkn kodi zetu tunazotoa zinawanufaisha kanda nyingine kwa kiasi kikubwa.

Tunahitaji kupigania uwepo was mpango na ratiba ya serikali wa kuweka reli ya SGR kusini, kama tulivyopigania mpango uleuliosababisha vurugu kusini kuweka mitambo yote ya kuzalisha umeme wa gesi vijengwe kwa kanda husika.

Na hizi mambo ya kukazania ktk elimu au uchumi wa MTU mmoja mmoja utafanikiwa kwa rahiso iwapo serikali itatufikia ktk mipango hiyo.
 
Hivi kuna kabila limeenea nchini kama wachaga na wasukuma?..itakua huijui hii nchi.

#MaendeleoHayanaChama
Ingawa sijakuelewa una maana gani, nafikiri mi nakuzidi kuijua hii nchi. We kwasababu ni mchaga ukisikia tu neno mchaga akili inakuruka maana mmejaa sifa za uwongo na kijinga.

Wachaga hawako kila eneo km wapo sehemu zingine ni wachache sana. Nyie wachaga mna utapiamlo wa akili. Mmejaa ulimbukeni, ushamba usioisha.

Uchagani mbona kuna umaskini wa kutisha mpaka mmekimbia kwenu? Nyie si mnaishi km wakimbizi ndani ya nchi hii. Mshukuru mwl. Nyerere mngekufa mafukara ya ajabu. Watanzania hawana ukabila nyie na umaskini wenu mmekaa kikabila.
 
Wapinzani ni lazima wasimamishe mgombea mmoja ili kupambana na CCM, Chadema ni ngumu sana kui overtake ACT mikoa ya kusini na Pwani, Maalim Seif alikua ni Taasisi...
Hatuihitaji CHADEMA kwasasa. Tunahitaji chama kikanda. Kufikiria chama kitakachomea kitaifa kitachumua zaidi ya miaka 50 kukuwa kwake.

Serikali yyt inapeleka nguvu zake kwa watu ambao tayari wameamka. Na nafasi moja ya kuonyesha jamii imeamka na inajitambua ninkwa kupitia jukwaa LA kisiasa.

Si CCM, si ACT, si CHADEMA iko tayari waachia nafasi za juu watu wenye nguvu kutoka kanda ya kusini.
TTunahita Maalim sefu wetu, tunahitaji Mbowe wetu.

Pamoja ya kuwa ACT INA wafuasi wengi kusini but mwelekeo was kiongozi was chama kwasasa in hauendani na mahitaji ya wanakusini.

Kusini adui yao mkuu so chadema, so CUF Bali in CCM.

But kiongozi wa acT anaikumbatia. Chama nikaelekea kuwa kama cha mzee wety Mrema. Tofauti PEKEE Kati Ya ACT Na TLP Ni Rangi Za Bendera Zao. Huyu Njano Huyu Purple Lakini Misimamo, Maono, Fikra, Siasa Zao N.k Ni Sawa Kabisa. Ni Ngumu Sana Kuitofautisha TLP ACT ya Tanganyika.
 
Mleta mada ameona kuandika uzi wake bila kuitaja CCM kutapelekea katibu mkuu wa Chadema aache kumtumia bando na buku ya kula kama anavyowatumiaga wanaharakati wengine. Nchi hii kuna baadhi ya vijana wamekubali kuuza utu wao kwa sababu ya njaa zao.
Unaacha kijadili hoja ya mtoa mada unaiwaza chadema tu.ccm lazima itajwe maana yenyewe ndio chama kilichounda serikali hii iliyoshindwa kwenye mambo mengi ukilinganisha na umri wa nchi na rasilimali zilizopo.Sasa kama wewe ulioni hilo ni ujinga wako.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Labda kwa kuwa mimi siamini kuwa vuguvugu za kisiasa zinaweza kutufikisha pahala pazuri.

Mimi naamini katika kutekeleza ajenda kwa njia ya utulivu,isiyo na hamasa,njia ambazo hata serikali hazitakuwa kikwazo na kutuletea FFU kutupiga mabomu.

Hizi siasa za namna hii mimi niko mbali nazo,naamini katika kufanya mambo ambayo yatakuwa hayatufanyi tuangaliwe kwa jicho baya na serikali
 
Ye mwenyewe hajui sasa sijui anatarajia Malaika waje walete mabadiliko anayoyatamani?.

Huenda waliopo wote wana akili kama za Mleta uzi kwa hiyo hakuna miujiza ya kusubiri.
 
Nijuavyo kwa Jamii ya kusini ilihitajika/inahitajika nguvu sana na pengine kupigana mijeledi ili kuwafanya Wanainchi kuthamini elimu Dunia ukilinganisha na jamii za sehemu nyingine.

Inaonekana kama vile walio/Wanaohamasisha elimu akhera na mambo ya kimila na kitamaduni wamekuwa/wana nguvu na inaonekana ni kama wana nguvu sana.

Ni kujiuliza nini kilikuwa kinaendelea tangu ukoloni huko kusini ukilinganisha na Kaskazini au kwingine?...ni nani wa kulaumiwa, Mkoloni, Serikali baada ya uhuru au Wakazi wenyewe wa Kusini?.

Bila kusahau pia jiografia ya kupakana na 'matatizo', nchi kama Msumbiji ni tabu tupu kulinganisha na Kaskazini waliopakana na Nchi kama Kenya n.k.

Huwezi kuacha kuzingatia miundombinu kwa maeneo yanayotumika na Wauzaji na Wanunuzi wengi hapa tukijumuisha na Watalii kutoka Kenya wakati Msumbiji hakuna kinachoendelea.

Kuna hotuba ya Mwalimu anasema "Maendeleo huvutwa na Watu wenyewe" akimaanisha kwa kadri mnavyojipanga maendeleo yanawafuata tu na si maendeleo kutangulia na kusubiri Watu.

Tujiulize nini kilikuwa kinaendelea kusini ukilinganisha na Kaskazini tanga zama hizo?.
 
Kuna mda unaongea point ila mda mwingine unazingua.ukorofii huo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Umeongea jambo muhimu sana.Nilikua sikubaliani na Jpm kupeleka Ikulu Dodoma mapema wakati bado nchi inachangamoto nyingi ambazo bado hazijatatuliwa.ila kupitia andiko hili nimebadilisha mawazo nakuona ni sawa tu kwa alichokifanya magufuli kwa dodoma.Kwasababu naamini bila shughuli za kiserikali mkoa kama dodoma kuendelea pakubwa ingechukua karne nyingi sana.Na ni ukweli kua ata mikoa ya kusini na maeneo mengine ya pembezoni mwa nchi yako nyuma kimaendeleo kwasababu hakuna shughuli au miradi mikubwa ya kiserikali inayochochea ustawi wa maeneo hayo.Sasa njia pekee ya wananchi wa maeneo hayo kuyakomboa maeneo yao ni kuwekeza katika elimu,elimu itakayoamsha vichwa vyakufanya wajitambue.Ziko fursa nyingi zinazoweza kufanywa na wananchi wa uko bila kuisubiri serikali,na kupitia juhudi za wananchi kupitia hizo fursa ndipo na serikali italazimika kufanya makubwa.Lakini pia watu wajitahidi kuchagua viongozi watakaokua tayari kujitoa kwa ajili ya watu.Mambo mengi yanakwama kwasababu ya aina ya viongozi tulionao.Hii nchi ni kubwa sana kwahiyo yapasa tuwe na viongozi wenye mawazo mapana yakulikomboa taifa badala yakuwaza matumbo yao.Waliopo wamechoka na hawana tena uvuvio mpya wakututoa hapa tulipo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Jadili hoja nini kifanyike.mambo ya chuki wewe ndiye unayeyaleta.Nchi ni yetu sote na kama kuna mahali kuna changamoto ni jukumu letu sote kuliongelea.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Siamini pia ktk vurugu. Kudai mfumo wa majimbo 8 au 10 in vision tu isiyo ya vurugu. Binafsi sipendi kuwa kama cuf ile au chadrma hii, na sio act ya bara. Bali kuwa kati na kati. Akili nyingi ndio itakayoongoza. Au sijui kama kuna Njia gn hizo za utulivu unazofikiria.
 
Njia za utulivu ni kutafuta njia ambazo wananchi watakuwa na uwezO wa kuamua jambo lao bila ridhaa ya serikali.

Mfano mfumo wa majimbo ni mpaka serikali itake kwma haijataka huwezi fanya lolote lile hata kama wanancho wote wameliwafiki.

Solution zitafutwe njia ambazo hata bila serikali basi njia hizo zinatekelezeka bila shida yoyote.

Kuna mikoa haina mfumo wa majimbo na bado wamenyookewa tu na miji inaenda vizuri.

Kama mikoa hiyo imeweza kuendelea bila mfumo wa majimbo maana yake kuna njia zilitumika zisizokuwa hizo za mfumo wa majimbo,basi na sisi tuzotumie hizo ama tuboreshe zaidi ya hizo ili tufikie levo ya uafadhali.

Maendeleo kusini bila majimbo inawezekana kama ambavyo maendeleo bila majimbo imewezekana mikoa mingine.
 
Mimi sio mchaga ila kwa kua wewe umejaa ujinga..ngoja ni kuelimishe hivi unajua kitu kinachoitwa wachaga ndio kabila lililoelimika kitambo hata kabla ya uhuru..wakati huo nyie wamakua na wamakonde majajua hata kuvaa wala kuongea kiswahili...wachaga ni watu wenye umoja na utajiri..wanaushirikiano mkubwa.

Hivyo huwezi jilinganisha nao..kaa kwakutulia uendele kuotoka korosho..usijifanishe na wachaga.

#MaendeleoHayanaChama
 

[emoji706]
 


Nadhani niseme nimeshindwa kukushawishi ili nawe ushawishi
Wengine..

Labda nikueleze kwa kutumia lugha ya kiuchumi kueleza faida ya serokali ya majimbo ktk zama hizi na kwa jamii ya watu waliolala.

Ni hivi nchi yetu imeingia ktk uchumi wa kati wa chini (lower middle-income economies - those with a GNI per capita between $4,046 and $12,535 (2021). Uchumi wa kati wa chini ni maana wake wasatani wa pato LA mtu mmoja mmoja ni laki 7 kwa mwexi. wenye uhakika was kupata walau sh laki 7 kwa mwezi. Kwa tz watu hao ni waajiriwa peke yao. Ajira za serikali kwa zaidi ya 90% kusini zimechukuliwa na wageni. kwa Mikoa unayoona imepiga hatua ya maendeleo ni ile ambayo INA vijana waliojiriwa na seikali na sekta binafsi. Kwa maana kwa makusudi serikali iliamua kuweza huko ktk elimu, afya viwanda nk

Na kwa makusudi serikali iliwabaguabaadhi ya kanda ikiwemo na kwa kiasi kikubwa ya kusini. Nafasi za kazi serikali 90% zikachukuliwa na wageni. Sio kwa sababu vijana hawana weledi laa, kwasababu ajira wanapeana kwa kujuana na Sera ya nchi ya ajira inaruhusu kufanywa wanayofanya.

Suala LA pili muhimu ni hili.... Jamii yyt ikitaka ijikwamue na isonge mbele lazima iwe na mirija yakuingiza pesa. Mfumo was serikali kuu umekata mirija yote ya kuingiza pesa kwa halmashauri. Matokeo yake mapato yote ya serikali yanakwenda hazina kuu na rais na ndie anaeamia wapi ziende sh ngapi.

Kwa vigezo hivi viwili nakwa jamii iliyolala kutaka kupita njia ambayo jamii iliyoamka imepitia tens kwa nguvu na maamuzi ya kisiasa.Nanyi mpite bila ya kutumia nguvu ya kisiasa ni kanuni isiyokubalika.

Ni Serkali ya majimbo ndio itaweza kutupitisha njia hiyo.

Serikali za majimbo hupewa nguvu na Uhuru zaidi huwalazimu 75% ya ajira kipaumbele wanapewa wazawa was kanda husika ktk nafasi zote nyeti. Mfano huo unaweza kuona ktkserikali ya jimbo LA znz katiba ya Kenya na nigeria. Hii inamaana kwamba serokali ya majimbo italazimisha mchakato wa ajira uangaliwe upya kwa kusinu utakuwa na manufaa makubwa kwao hivyo nao kuweza kuendeleza miji yao.

Serikali ya majimbo inapewa nguvu na mamlaka ya kukusanya mapato na 75% hayo yatumike ndani jimbo/kanda. Na 25% yanakwenda serikali kuu.

Bado tu huoni faida ya serokali ya majimbo na kuanziaha jukwa litaloelimisha na Kuhamasha wanakusini na watz kwa ujumla kipindi cha uchaguzi kupiga kura na tuchague chama ambacho kitabadili muundo wa serikali kutoka serikali kuu hadi serikali za majimbo yenye Uhuru zaidi was kujiamulia mambo yao wenyewe
 
Ndanda hospital ni referral hospital


That's one,nisihangaike tena maana inaonekana unazungumza usilolijua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…