Siku zote tumekuwa tukisema wale machawa wa mama mama mama, ni watu waliokosa akili maana hakuna mwenye akili anayeweza kukubali kuwa chawa, kumbe machawa wamekuwepo tangu kale, na Bwana, Mfalme wa Mbingu na nchi alikwishawalaani. Leo nimelifikia neno la Mungu linaloweka wazi kuwa uchawa ni laana. Hii ina maana wale wanaojiona ni waumini, lakini wameingia kwenye uchawa, basi tayari wamejiondoa kwenye njia ya Bwana. Lakini wakosoaji au wakemeaji wa mambo mabaya, wana baraka za Mungu. Andiko hili linatoka kwenye Biblia, kitabu cha Mithali:
" Yeyote anayemkemea mtu aliyekosea atapata kibali mwishowe kuliko mwenye ulimi wa kujipendekeza " (Mithali28:23).
Mwashambwa, jitafakari juu ya njia uliyoamua kuiendea. Siku zote itafute hekima ya Mungu, nawe utapokea baraka ya Bwana.
Tena juu ya watawala, imewekwa wazi kuwa kiongozi mbaya akianguka, watu watafurahi. Hivyo tusishangae watu wanaposhangilia mabaya yanapowapata watawala wabaya:
" Wasio haki wainukapo mamlakani, watu hujificha; bali waovu waangamiapo, wenye haki husitawi. " (Mithali28:28).