Hakuna Kauli mbovu na ya kizembe niliyowahi kuisikia kama hii ya "Tafuta Hela"

MTU mwenye Akili timamu hawezi kumwambia mwenzake "tafuta hela" huu ni msemo wenye kejeli Tu Kwa watu.
Wajinga wenye milioni 2 bank ndiyo wanatumia misemo hii yakifala Ila Kwa MTU mwangaikaji hawezi kubeza maisha ya wengine kwasababu hapa duniani mpaji ni MUNGU Tu na unaweza kutafuta hiyo pesa masaa 24 na usipate hata mia
 
ni kauli ya kizembe na kishetani sana. haihamasishi bali inakwaza. zamani kabla sijapitia maisha fulani nilikuwa naamini wasio na pesa ni wazembe, nikapigika sana, nilifanya kazi kwa bidii sana lakini nilikuwa sitoki, Mungu akaona anionyeshe kwamba yeye ndiye mpaji hata kama tunajibidiisha, nilipopata somo Mungu akafungua njia, nikapata pesa bila kutoa jasho jingi kama nilivyotegemea kwasababu MKono wa Mungu ulinitangulia. Mwombe Mungu aende pamoja nawe, mpe Mungu kilicho cha Mungu, hasa fungu la kumi na malimbuko. utakuja kutoa ushuhuda hapa. ingekuwa uongo ningewaambia, imetokea kwangu kabisa.
 
Tafuta hela bana . Kama kuiba iba . Fanya ufanyalo tafuta hela . Fungua kibiashara fanya kila namna kuongeza kipato. Acha kulia lia
 
Mkuu tafuta pesa acha maneno
 
Tafuta hela bana . Kama kuiba iba . Fanya ufanyalo tafuta hela . Fungua kibiashara fanya kila namna kuongeza kipato. Acha kulia lia
Mashauri amangana

Biashara Hazilett pesa zinaleta madeni na mali😀

Uibe kabisa tata?😀
 
Kabisa mkuu.

Sasa mtu ni Researcher au Prof. Au mtaalam wa Pathology unamwambia tafuta hela... anazitafuta wapi?

Kauli iliyokosa maadili na ku degrade nguvu ya shughuli nyingine za kijamii.
Pathologist wa cases za forensic ukimwambia atafute pesa ni kwamba awe anapokea rushwa ya kupindisha ukweli wa matukio ya case kama vifo na mengineyo ambayo yakiwa yanakuhusu wewe uliyesema tafuta hela itakuumiza. Wakifuata haki wasidhulumu nafsi ya mtu kuna wapuuzi wachache wanamuambia atafute hela...Shabash🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…