GE2025 Hakuna Kiongozi Amewahi kupata Mapokezi Makubwa kanda ya Ziwa kama Aliyoyapata Rais Samia

GE2025 Hakuna Kiongozi Amewahi kupata Mapokezi Makubwa kanda ya Ziwa kama Aliyoyapata Rais Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Watanzania,

Nimefuatilia na kuendelea kufuatilia Mikutano ya Kampeni ya Rais Samia kanda ya Ziwa. Kwa hakika hakuna kiongozi yeyote yule wa ngazi yoyote ile amewahi kupata Mapokezi makubwa ,ya Heshima kama aliyoyapata RAIS wetu Mpendwa na Mama yetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Kwa hakika Mama amepokelewa kishujaa , Mama amepata Mapokezi ya kipekee, Mama amepata Mapokezi ya heshima , Mama amepata Mapokezi ya kihistoria,Mama amepata Mapokezi yaliyoacha alama ambayo haitafutika wala kufutwa na mtu yeyote yule.

Ni Mapokezi ambayo yalihudhuriwa na watu wengi sana katika historia ya kampeni za kisiasa katika Taifa letu. Ni Mapokezi ambayo yaliyoonyesha upendo walionao watu wa kanda ya ziwa kwa Rais wetu Mpendwa. Ni Mapokezi yaliyoonyesha kupendwa ,kukubalika na kuaminika kwa Rais Samia.

Ni Mapokezi yaliyoonyesha Imani kubwa waliyonayo watu kwa Rais wetu. Ni Mapokezi yaliyoonyesha utayari wa watu kumpatia kipindi cha pili kuliongoza Taifa letu. Hii yote ni kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Rais wetu ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake madarakani.

Hii yote ni kutokana na miradi mikubwa Ya Mabilioni kwa mabilioni ya kimkakati na kimaendeleo iliyotekelezwa na kupelekwa na Rais Samia . Hii yote ni kutokana Kugusa Maisha ya watu,kuinua uchumi wa watu, kuwawezesha watu kustawi ,kuwawezesha watu kutimiza ndoto zao,kuwapa watu Matumaini na kuboresha Maisha ya watu.

Iwe ni kwa vijana ,akina Mama ,wazee na watu wa Makundi mbalimbali unaona namna Rais wetu alivyofanya uwekezaji na Kugusa Maisha yao.Ndio maana hata ukiangalia kitakwimu unaona Mama Ametoa Mabilioni mengi sana kutekeleza miradi ya maendeleo kanda ya ziwa. Miradi ambayo imetoa fursa za ajira kwa vijana na kusogeza huduma za kijamii karibu kabisa ya wananchi.

Kwa Hakika Rais Samia ni kipenzi cha watanzania, ni chaguo la Mungu,Ni Mbarikiwa na mwenye kibali Mkononi pake. Usishindane na aliyeinuliwa na Mungu. Rais Samia kainuliwa na Mungu na ndio sababu ya kukubalika kwake na kupata mapokezi Makubwa kwelikweli kila akanyagapo na kuweka miguu yake
Screenshot_20251003-192807_1.jpg
i.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Screenshot_20251012-133108_1.jpg
 
HaMachiach
Hizo ni ziara za kiserikali wala sio kampeni.
Kampeni gani wagombea ubunge wakipewa nafasi ya kuongea badala ya kuomba kura wanamwomba mgombea urais miradi! Hizo utasema ni kampeni?
 
Hizo ni ziara za kiserikali wala sio kampeni.
Kampeni gani wagombea ubunge wakipewa nafasi ya kuongea badala ya kuomba kura wanamwomba mgombea urais miradi! Hizo utasema ni kampeni?
Wivu tu ndio unaokusumbua
 
Who cares! Halafu mbona hamyaoneshi na yale malori yaliyotumika kuwabeba hao watu kama ng'ombe kuja kuwashuhudia wasanii wa bongo muvi na bongo fleva, wakiongozwa na Bi Khadija Kopa?
Kwani wasanii wao sio watanzania? Sio wapiga kura? Hawana haki ya kupiga kura?
 
Yaani unaandika ktk mtandao uliofungwa na hiyo serikali yako? Sasa wenzio wataipataje hii habari bila V.P.N?.

Kama unampenda kweli huyo Samia si ungefuata sheria aliyoweka usiingie ktk mitandao aliyoifunga ili uoneshe mapenzi ya kweli na misimamo.
 
sasa km anagawa hela kwanini watu wasijazane tena wanasafirishwa bure kwenda mkutanoni na kurudishwa makwao
 
sasa km anagawa hela kwanini watu wasijazane tena wanasafirishwa bure kwenda mkutanoni na kurudishwa makwao
Unaweza vipi kugawa pesa kwa mafuriko ya watu maelfu kwa mamillioni wanaohudhuria katika mikutano ya Rais wetu Mpendwa?
 
Kwa hill nyomi la mtia nia analopata yeye ndio alitakiwa awe wa kwanza kudai tume huru ila nyomi lote hilo hataki tume huru hii ni maajabu
 
Nyomi zote za sa100 ni fake...sio za kizalendo kwamba watu wafike mkutanoni kwa usafiri wao binafsi.

Watu wengi mkutanoni hasa vijana na watoto hujazana kutazama show za bure za wasanii, hawakuja mkutanoni eti wamevutiwa na mgombea kama mgombea!
Kundi hili ndio wengi zaidi, kikubwa kwao ni KUSHANGAA!!.
 
Nyomi zote za sa100 ni fake...sio za kizalendo kwamba watu wafike mkutanoni kwa usafiri wao binafsi.

Watu wengi mkutanoni hasa vijana na watoto hujazana kutazama show za bure za wasanii, hawakuja mkutanoni eti wamevutiwa na mgombea kama mgombea!
Kundi hili ndio wengi zaidi, kikubwa kwao ni KUSHANGAA!!.
Embu na wewe kaitishe mkutano uone kama kuna watu watakuja kukusikiliza. Hata wajinga wenzako hawawezi kuja.
 
Back
Top Bottom