Hakuna kitu kinauma kama kuona mtaa uliokulia nyumba nyingi zimefanywa kuwa maduka, biashara, n.k.

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Kuna maeneo ya makazi tuliyowahi kukulia yaliyokuwa yanawaweka watu pamoja huwa yanaanza kupoteza asili yake kwa kugeuzwa kuwa maeneo ya biashara,

unakuta majirani karibu wote uliowahi kuwajua wamehama wameuza plot, mtaa umejaa fremu, magorofa, bar, lodge, gereji, magodauni, n.k.

  • Nyumba za Majirani mliowahi kufahamiana hawapo tena
  • sehemu zilizoacha alama kwenye maisha yako hazipo tena
  • viwanja mlivyokutana na marafiki yamejengwa maduka, n.k.

Nawaonea huruma wasio na vijiji vya kurudi, yani wao wamekulia mjini inakuwa ngumu kurudi hayo maeneo
 
Unaporudi makazi uliyokulia kuna kumbu kumbu huwa zimo kichwani za mitaa uliyoishi kwenye ukuaji wako, familiza za majirani mliojuana, sehemu zilizoacha alama kwenye maisha yako, viwanja mlivyokutana na marafiki, n.k.

Ghafla eneo hilo linaanza kushambuliwa na wenye fedha zao kuzinunua nyumba na kuzibadili au kujenga upya maduka, lodge / hotel, nyumba za kupanga, maduka, makampuni, parking, n.k.

Unaweza kukosa hamu kabisa ya kurudi maeneo hayo
Wewe umekulia mitaa ya barabarani? Shukuru hizo nyumba zimekuwa maduka, Magufuli alitaka kuzibomoa iwe barabara! Hujaona Sinza kunavyopendeza siku hizi? Kama Ulaya!
 
Sehemu yoyote babarabara inaweza kupanuliwa kama kuna potential, leo 2024 nimakazi ya watu ghafla 2040 mji umehamia huko barabara zinapanuliwa
 
Unachosema ni kweli, nlienda Kwa anko wangu mitaa fulani tabata, ulikuwa mtaa wa makazi fresh tu ila saivi majirani wote wameuza plot kabaki yeye tu Yan mtaa umejaa una gereji kubwa, magodauni, hotels, lodge, maduka makubwa makubwa

Inshort kawekwa kati na hataki kuuza maana nje ya mji ana eneo kubwa tu kama ekari5
 
Hana shida ya pesa, Lakini akitangulia mbele ya haki, madalali wataanza kuwasaka watoto wauze eneo, ofa za milioni 100, 200, n.k. kwa usawa huu watoto hawachomoi
 
Hii ni kama cycle ya makazi Tanzania. Sehemu nzuri inapimwa na kuanza kujengwa. Kuna kuwa na nyumba nzuri na makazi safi. Baada ya wazazi kustaafu na wengine kufariki pesa zinakata eneo hilo. Nyumba zinaanza kuuzwa kwa wawekezaji, na kwa vile hatuna zoning(kitu ambacho ni kizuri kwa upande fulani) basi kila aina ya vurugu itaingia kwenye eneo hilo. Maeneo yote mazuri mazuri yanapitia hii cycle.
 
Kuna maeneo ya makazi tuliyowahi kukulia yaliyokuwa yanawaweka watu pamoja huwa yanaanza kupoteza asili yake kwa kugeuzwa kuwa maeneo ya biashara,

unakuta majirani karibu wote uliowahi kuwajua wamehama wameuza plot, mtaa umejaa maduka, lodge / hotel, gereji, magodauni, n.k.

  • Nyumba za Majirani mliowahi kufahamiana hawapo tena
  • sehemu zilizoacha alama kwenye maisha yako hazipo tena
  • viwanja mlivyokutana na marafiki yamejengwa maduka, n.k.

Nawaonea huruma wasio na vijiji vya kurudi, yani wao wamekulia mjini inakuwa ngumu kurudi hayo maeneo
Yaani mkuu umeelezea my feelings kabisa ambayo huwa naipata nikipita eneo nililokulia (Tabata Bima), huwa nasikitika sana. Maeneo yenye kumbukumbu zinazoibua hisia kali, now yamekua baa, lodge, na ma fremu ya biashara. Maeneo ya viwanja tulivyocheza mpira enzi hizo utotoni, now yote ni majengo ya biashara. Mara zote nikipita yale maeneo napata hisia za huzuni sana.
Kuna uwanja mmoja wa mpira ulikua karibu na shule ya St Mary's pale, tulikua tunaenda kupiga boli pale timu yetu ya mtaa, tunakiwasha vibaya kabisa. Sasa hivi pote pamepigwa frame.
Kuna shortcut moja tulikua tunapita kutoka Bima kwenda Tabata Kimanga, tunakatiza bondeni hadi Kimanga....! Ile njia now haipo, kote ni majengo.
Wakati umekwenda wapi?
 
H

Kama nchi.hatuna plan..kutenganisha.makazi.na biashara hiyo ndiyo sababu
 
Back
Top Bottom