Hakuna kitu kinauma kama kuona mtaa uliokulia nyumba nyingi zimefanywa kuwa maduka, biashara, n.k.

Hakuna kitu kinauma kama kuona mtaa uliokulia nyumba nyingi zimefanywa kuwa maduka, biashara, n.k.

H

Kama nchi.hatuna plan..kutenganisha.makazi.na biashara hiyo ndiyo sababu

Hii nchi si ya wakulima tena bali ni ya wafanyabishara,kila mtanzania kwasasa anamiliki walau fremu ya biashara moja!kitu ambacho ni kizuri
Kibaya ni pale bidhaa zinazouzwa karibia zote hutoka nje ya nchi,HII NI HATARI SANA KWA KILIMO NA VIWANDA VYETU
 
Acha kabisa , nikiangalia fremu na ghorofa zilizojengwa maeneo ya kuanzia mbezi shule mpaka Makonde nashangaa Sana, ni mabadiliko ya muda mfupi Sana na maeneo yote haya yalikuwa ni ya wazi
 
Yaani mkuu umeelezea my feelings kabisa ambayo huwa naipata nikipita eneo nililokulia (Tabata Bima), huwa nasikitika sana. Maeneo yenye kumbukumbu zinazoibua hisia kali, now yamekua baa, lodge, na ma fremu ya biashara. Maeneo ya viwanja tulivyocheza mpira enzi hizo utotoni, now yote ni majengo ya biashara. Mara zote nikipita yale maeneo napata hisia za huzuni sana.
Kuna uwanja mmoja wa mpira ulikua karibu na shule ya St Mary's pale, tulikua tunaenda kupiga boli pale timu yetu ya mtaa, tunakiwasha vibaya kabisa. Sasa hivi pote pamepigwa frame.
Kuna shortcut moja tulikua tunapita kutoka Bima kwenda Tabata Kimanga, tunakatiza bondeni hadi Kimanga....! Ile njia now haipo, kote ni majengo.
Wakati umekwenda wapi?
Kuna kipindi unatamani kuwapeleka watu wa karibu kama watoto sehemu ulipokulia lakini pashapoteza asili, unabaki kuwahadithia tu sehemu flani niliishi kabla hapajabadilika
 
Hana shida ya pesa, Lakini akitangulia mbele ya haki, madalali wataanza kuwasaka watoto wauze eneo, ofa za milioni 100, 200, n.k. kwa usawa huu watoto hawachomoi
Sure, kwanza mshua ni mkoloni balaa,,pia ana eneo kubwa huko chanika kama eka3 alijenga kajumba kadogo huko pia kazungukwa na mijumba ila hauzi hata robo
 
wa kiusa moshi town tujuane hapa..nikirudi dar steet nimekuwa mgeni kabisa maeneo ayameuzwa yamebadilishwa sana
 
Back
Top Bottom