Hakuna kitu kinauma kama kuona mtaa uliokulia nyumba nyingi zimefanywa kuwa maduka, biashara, n.k.

H

Kama nchi.hatuna plan..kutenganisha.makazi.na biashara hiyo ndiyo sababu

Hii nchi si ya wakulima tena bali ni ya wafanyabishara,kila mtanzania kwasasa anamiliki walau fremu ya biashara moja!kitu ambacho ni kizuri
Kibaya ni pale bidhaa zinazouzwa karibia zote hutoka nje ya nchi,HII NI HATARI SANA KWA KILIMO NA VIWANDA VYETU
 
Acha kabisa , nikiangalia fremu na ghorofa zilizojengwa maeneo ya kuanzia mbezi shule mpaka Makonde nashangaa Sana, ni mabadiliko ya muda mfupi Sana na maeneo yote haya yalikuwa ni ya wazi
 
Kuna kipindi unatamani kuwapeleka watu wa karibu kama watoto sehemu ulipokulia lakini pashapoteza asili, unabaki kuwahadithia tu sehemu flani niliishi kabla hapajabadilika
 
Hana shida ya pesa, Lakini akitangulia mbele ya haki, madalali wataanza kuwasaka watoto wauze eneo, ofa za milioni 100, 200, n.k. kwa usawa huu watoto hawachomoi
Sure, kwanza mshua ni mkoloni balaa,,pia ana eneo kubwa huko chanika kama eka3 alijenga kajumba kadogo huko pia kazungukwa na mijumba ila hauzi hata robo
 
wa kiusa moshi town tujuane hapa..nikirudi dar steet nimekuwa mgeni kabisa maeneo ayameuzwa yamebadilishwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…