Hakuna kitu kinaumiza kama unaamka Asubuhi na hujui utaenda wapi

Nakumbuka hiki kipindi nilisota sana mawazo mengi, ila nashukuru Mungu nilikutana na mtu akanipa mchongo nipo nafanya mpaka sasa napambania nipate mtaji nijiajiri, ili niepukane na kadhia kama hizo ikitokea sina kazi tena.
Naomi mambo
Ukishika sana hela nyingi hata muda wa kula unakua hauna muda hautoshi kwahiyo tumia muda huu kula vizuri
 
Ilinikumba hiyo. Niliachishwa KAZI, account zikafungwa, miezi sina mishe , mke akaanza uzinguzi full balaa.
 
Daaaah siku Moja nikiwa Sina mishe nikaamua kwenda kujitolea kweny ofisi Moja....nkakatuna na mfanyakazi Amefanya KAZI miaka 10 Cha ajabu ananiomba mim nauli Ile Hali Sina hata mia mfukoni.....
 
Hiyo hali ilinikuta mwaka 2017 au 18 nikawa naenda baharini kuzurura tu kule.

Kuna siku njaa inapiga vibaya sana nikawa nimepumzika nyuma ya makao makuu ya CRDB kama unaelekea Azania Bank kuna fundi viatu pale.
Kuna akina dada wawili waliniletea kipaseli cha wali aisee kutokana na njaa inavyopiga sikujaribu kabisa kusema sitaki nataka.

Kwa maelezo yao ule wali walikuwa wanapeleka kwa mafundi sasa wakawa wameondoka mapema ile siku.

Yaani nahisi nilikuwa na shida hadi zikawa zinang'aa kwa mbali.
 
Kwahiyo mzee miezi.mitatu unaamka asubuhi unaenda town kuzurura ili uwende sawa na majirani?

Haya ndio matatizo ya kutoishi maisha yako,kama ulienda kwa ajili ya kutafuta riziki ni sahihi ila kama kwa ajili uonekane nawe unapambana dah pole sana
Tulia mkuu hata mimi nilikua na jeuri kama wewe
 
Pole na hongera .

M A I S H A yana mambo Sana Ila pia nilichojifunza we need to invest more is our mind hasa nyakati hizi ambazo anayefanya Kazi ya nguvu analipwa hela ndogo kuliko anayefanya Kazi ya kutumia Akili.

Nimepitia Hicho kipindi but God is Good I never went to bed with hungry hiyo watu watanionaje huwa sijali kabisa kwakuwa this is my life.
 
Kwahiyo mzee miezi.mitatu unaamka asubuhi unaenda town kuzurura ili uwende sawa na majirani?

Haya ndio matatizo ya kutoishi maisha yako,kama ulienda kwa ajili ya kutafuta riziki ni sahihi ila kama kwa ajili uonekane nawe unapambana dah pole sana
Mkuu binadamu real kama ww mmebaki Wachache sana hapa duniani, mmjojawapo ni ww
#ishi maisha yako kuwa wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…