Hakuna kitu kinaumiza kama unaamka Asubuhi na hujui utaenda wapi

Hakuna kitu kinaumiza kama unaamka Asubuhi na hujui utaenda wapi

Hiyo Hali uisikie tu kwa mpita njia akihadithia. Tena ina unafuu ukiwa gheto kwako, vuta picha ile unakaa kwa broo halafu shem ni mnoko sana. Anamka asubuhi anakuambia sehemu mi Leo sipiki kwahiyo utamalizia hicho kiporo Cha wali na maharage.
Ukila ukishiba inaomba Mungu isipite hali yoyote ya uchafuz wa hewa maana shemej yako atajua wewe ndo umeharibu Hali ya hewa, na huwez kukata maana wewe ndo umeshindia kiporo Cha wali maharage
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yaani unaamka halafu hauna mishe zozote au mishe ulikuwa nazo zinegoma aisee inapain sana.

Nilipitia hii hali basi bwana nilipopanga chumba unaona vyumba vya majirani zako Wanaamka Mapema wanaenda mishe kurudi jioni Mimi nipo tu

Hii hali ilinitesa sana kutokuwa na mishe full no respect mtaani yaani unaona kabisa hapa hii kwakuwa sina mishe

Basi bwana, nikaona nisiwe boya nikaanza nami kuamka mapema naoga na vaa vizuri naondoka kumbuka sina kazi yoyote hapo naenda mjini

Naenda zangu mjini kuzurura kumbuka kama hauna mishe jua linachelewa kuzama hatari

Mimepiga hiyo kitu kama miezi mitatu heshima nilipokuwa nakaa ikarejea kidogo, mabinti walikuwa wengi hapo napoishi wakawa wananiambia eeh sikuizi umepata mishe hongera Mimi najibu si unajua tena, kumbe wangejua nazurura tu mjini huko

Nifupishe, katika kuzurura kwangu nikapata Dili hilo Dili ikanipa Hela kidogo hiyo Hela nikaona fursa huko huko mjini nikatembea nayo

Tutoke maghetoni vijana Dunia Haina huruma na mtu asiyekuwa na shughuli ya kumwingizia kipato

Kama ushapitia hali hii pita hapa toa experience yako ilikuwaje

Mungu awapiganie Wote wanaoamka Asubuh halafu sehemu ya kwenda hawana wapate mishe🙏🏿🙏🏿🙏🏿
Uzoefu ni mwalimu mzuri sana. Pia maisha ni safari ndefu. Kwenye safari kuna milima, mabonde, tambalale n.k

Mimi kuna wakati niliwahi kuwa natembea kwa miguu kutoka Kjitonyama kwa Ali Maua hadi Coco Beach kwenda kushangaa mawimbi ya bahari.
 
Uzoefu ni mwalimu mzuri sana. Pia maisha ni safari ndefu. Kwenye safari kuna milima, mabonde, tambalale n.k

Mimi kuna wakati niliwahi kuwa natembea kwa miguu kutoka Kjitonyama kwa Ali Maua hadi Coco Beach kwenda kushangaa mawimbi ya bahari.
Hahahha dah aisee kwanini uliamua kufanya hivyo
 
Back
Top Bottom