Hakuna kitu kinaumiza kama unaamka Asubuhi na hujui utaenda wapi

Bora mara kumi iwe na hy idea ya kutoka nje hata ili tuu uendane na majirani kuliko kukaa tuu ndani bila ishu yoyote, kumbuka akiwa huko nje anaweza kubahatisha chcht kuliko akiwa ndani tuu
Nilifanya hivyo kutoka nami niendane siyo kwa ubaya kuwa nawaiga, hata nilikuwa sijui kazi zao wanaenda na kurudi nawaona

Hila nami kutoka ilinisaidia nikakutana na tangazo la kazi ya Msimu nikaenda interview nikapita, nikafanya kwa msimu ukapoisha nikasevu kidogo nikaanzisha mradi wangu mdogo, kwahyo nje kutoka kulinisaidia
 
Dini zote huubiri juu ya upendo, kwa imani yangu ya kikiristu Roho Mtakatifu aliyepandikizwa ndani yangu amenisaidia sana wakati wote kuniongoza ule wakati ambapo wazazi wangu hawakuwepo. Huu ni ushuhuda mwingine πŸ™πŸΎ.
 
Safi sana ukitoka unapata akili mpya na kuona fursa hata za kipato kidogo.
 
Kabisa nduguπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ
 
Mungu awapiganie Wote wanaoamka Asubuh halafu sehemu ya kwenda hawana wapate misheπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ
 
Kwahiyo mzee miezi.mitatu unaamka asubuhi unaenda town kuzurura ili uwende sawa na majirani?

Haya ndio matatizo ya kutoishi maisha yako,kama ulienda kwa ajili ya kutafuta riziki ni sahihi ila kama kwa ajili uonekane nawe unapambana dah pole sana
Ni moja kati ya matukio mawili yaliyotaka kunisabishia pressure na kisukari Cha utotoni.
 
mama bado yupo?
 
Ila hao wengi walishajipanga pesa wanrkula sn ht haziwafikii walengwa
Labda Kwa ambayo ndo walijua wanaanza au Hawana muda mrefu
Kadri unavyopata na matumizi yanakuwa makubwa. Utashangaa wana madeni makubwa kuliko wewe na mimi, huko Bank wamekopa hadi 50m na hakuna cha maana wamefanya, stress juu ya stress.
 
Afadhali wewe ambaye ulikuwa unaamka na hujuwi pa kwenda,,hata ukaamua kuanza kutoka kwenda mjini kuzurura. Inamaana hata nauli ulikuwa nazo.

Mimi nilikuwa naamka na sijuwi tutakula nini Mimi na family yangu..
hata hyo nauli ya kwenda mjini sijuwi ningepataje.

Ila kweli MUNGU sio athumani AISEE.
 
"Mtembea bure si mkaa bure"
"Mgaagaa na upwa hali wali mkavu"
 
Hatar sana,unaweza kuona dunia yote imekuelemea wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…