Hakuna kitu kizuri kama kufanya biashara au kilimo kwenye makaratasi ukisaidiwa na calculator, lakini kiuhalisia inaweza isewe hivyo

Hakuna kitu kizuri kama kufanya biashara au kilimo kwenye makaratasi ukisaidiwa na calculator, lakini kiuhalisia inaweza isewe hivyo

Bravo snr

Senior Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
182
Reaction score
477
Nilipomaliza chuo sikutaka kuajiriwa. Nikaona nijiajiri ili niweze kupata utajiri wa haraka ndani ya miaka michache.

Nikafanya biashara ya kwenye makaratasi nikaona nitapata faida kibao huku nikisaidiwa na calculator yangu.

Nikaomba mtaji home, huyo nikaenda Songea kununua mahindi na kupeleka ghala la taifa. Nilichokikuta kule ni tofauti na biashara ya kwenye makaratasi, asikuambie mtu kuna gharama nyingi zinaongezeka tofauti na mategemeo. Nashukuru Mungu sikupata hasara ila faida ilikuwa kiduchu sana tofauti na ya kwenye makaratasi ila nilijifunza kitu kuwa ukitaka upate faida kubwa lazima uwe mjanja mjanja kwa kupunguza gharama zisizo za lazima.

Msimu ukaisha nikaona biashara nyingine huko huko ya mayai ya kuku wa kisasa maana kuna watu kutoka Mozambique walikuwa wanakuja kununua mayai Songea.

Kama ada nikachukua karatasi na calculator kufanya faida zangu. Nikaona faida kubwa.

Nikakodisha nyumba nzima ila uzuri wa kule nyumba hazina gharama. Nikanunua vifaranga 500 nikanza kufuga na kuvipa chanjo kila zinazo hitajika. Kitu ambacho sikujua kwanye ufugaji wa kuku ni kuwa wale wadudu wanakula balaa ko nilitakiwa kuwa na pesa za kutosha mpaka ifike miezi sita ndo waanze kujilisha wenyewe kwa kuuza mayai.

Walipo fikisha miezi sita wakaanza kutaga mayai ila madogo hapo nilifurahi sana kuwa naanza kuona matunda, maana walibaki hai kuku kama 469 na wawili waligoma kukua ko walikuwa kama vifaranga na hawakuwa na uwezo wa kutaga.

Siku moja naenda kutoa mayai ili nisafishe vyumba nikakutana na usemi ule ng'ombe wa masikini hazai, yaani kama kuku kumi wamekufa tena wale wakubwa wakubwa.

Nikapiga moyo konde nikawatoa na kusafisha vyumba, kesho yake nikakuta tena wamekufa wengine, hapo kichwa kiliuma sana na kufikiria mambo mengi sana na kukumbuka ajira.

Hali hiyo ikaendelea mpaka Walipo fika kama 100 kufa nikakata tamaa na kuanza kuuza tena kwa hasara kama kuku wa nyama.

Hapo nilipata hasara kubwa sana, niliwalisha kwa miezi sita bure. Ikanibidi nipige simu home kuulizia kuwa kwenye kabati langu waangalie kama vyeti vyangu vipo salama?

Ikabidi nirudi home mnyonge sana, Nikaomba ushauri kwa ndugu yangu mmoja akaniambia una kiasi gani nikamtajia akasema njoo Arusha tufanye biashara.

Kule ndo nilijifunza biashara inavyotakiwa kufanya. Nikajifunza ukitaka biashara fanya biashara zisizo mulikwa sana na TRA tena uswahilini ambako utakuwa unalipa tu kodi ya nyumba na ushuru mdogo mdogo. Pia nikagundua kuwa biashara zile tunazo zizarau watu wengi zina faida sana tena sana, hapa nazungumzia sisi wenye mitaji midogo midogo na tunataka kufanya biashara na tunataka kukuua kibiashara,sijazungumzia wale wenye mitaji mkubwa mikubwa.

Ila jua biashara sio kama tunavyo fikiria faida tu kuna hasara pia ila nashukuru Mungu safari nilipata faida na kukuza mtaji na kujifunza mengi sana.

Pia unaweza ukawa na mauzo labda 250k ila ukihesabu ulivyo uza wakati wa kufunga hesabu za siku na huja kopesha ila kwenye cash una 230k hapo ndo utajiuliza hiyo 20k imeenda wapi? Cha msingi ni kuwa makini katika kutunza kumbukumbu za biashara.

Hiyo ni mifano michache katika biashara nilizo fanya ila nimeamua kutoa hizo hapo juu kama mfano.

Mwishoe nikaona niukuze mtaji kwa haraka ikanibidi nikimbilie ajira huku nikiendelea na kujifunza na uendeshaji wa biashara.

Je wewe kama unafanya biashara au kilimo, faida ilikuwa kama ulivyo fanya kwenye makaratasi ukisaidiwa na calculator?

Kama ndio au hapana tupe uzoefu wako. Ili watu wapate kujifunza maana saivi kila ukipita kila kona vijana wanaambiwa wajiari bila kuwapa jinsi ya kujiajiri.
 
Dah baishara ni changamoto sana yaan una amakaa asubuhi unaanza kusibiria wateja mtaji jumlisha kodi millioni 10 mauzo to elfu 20 per day unaweza sema umelogwa
Kabisa biashara ni changamoto bale unapo kosea market niche ya biashara yako.
 
Kilimo cha ndani ya nyumba na calculator huwa kina faida kubwa hadi unaona Elon Musk unamkamata ndani ya mwezi mmoja.
Ndio maana huwa wanashauri kwamba ni vizuri kama utafanya biashara kama ukiwa umetoka kuajiriwa katika biashara ya aina hiyo hiyo.

Yaaani kama wewe uliajiriwa Bureau De Change kisha ukaacha kazi na kuamua kufungua ya kwako ni afadhali zaidi kuliko kuanzisha biashara ambayo hauijui kabisa.
 
Ndio maana huwa wanashauri kwamba ni vizuri kama utafanya biashara kama ukiwa umetoka kuajiriwa katika biashara ya aina hiyo hiyo.

Yaaani kama wewe uliajiriwa Bureau De Change kisha ukaacha kazi na kuamua kufungua ya kwako ni afadhali zaidi kuliko kuanzisha biashara ambayo hauijui kabisa.
Tehehehehehhhehe
 
Back
Top Bottom