Hakuna mabadiliko ndani ya club ya Simba, msidanganyike

Hakuna mabadiliko ndani ya club ya Simba, msidanganyike

Jeff Gemo

Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
34
Reaction score
26
(Cosmopolitan Concepts – Redefining the art of living)

Wanasema leo wamepiga hatua moja mbele, nasema very good! Bila baraza la wadhamini wa Club (nadhani katiba yao inaruhusu) Mwaka huu tumekuwa na upepo mpya kabisa katika Nyanja ya michezo nchini, hasa mpira wa miguu, upepo wa mabadiliko. Ni hitaji la kila mpenda michezo na anayetamani maendeleo na mwenye kiu ya kuinua soka la nchi yetu, hilo halipingiki kabisa na mimi binafsi (Jeff Gemo) ni mpenda mabadiliko, nimetumia muda mrefu sana kuyahubiri na kushawishi watu wakubwa kwa watoto kukubali kubadilisha mfumo, viongozi na watumishi wa kada mbalimbali wanaounda umoja wa Simba Imara waliniamini na tukawapa pamoja ili kushawishi uongozi wa Simba Sports Club chini ya Evans Eveva waridhie mabadiliko kwa ustawi wa club yetu. Baadae walikubali na ninasema nitaunga mkono na kupigania mabadiliko ya kweli katika Club yangu ya Simba Sports na si vinginevyo.

Jana nimesikia muwakilishi wa Baraza la wadhamini la Simba Sports Club akiunguruma mithili ya Simba dume katika Studio za Radio Times, kipindi cha michezo cha wiki “Mita 100”. Msemaji wetu wa zamani Clifford Mario Ndimbo anafanya kazi kubwa ambayo kama watanzania wangekuwa wanafuatilia na kusikiliza kipindi chake, basi tungekuwa tuna uelewa mkubwa sana wa masuala tatanishi katika mpira wetu. Jana mambo mengi makubwa yamezungumzwa na kuwekwa wazi kwa wanachama ili wafunguke na kuhoji lakini ajabu ni kwamba hakuna atakayeweza kufikirisha angalau nusu ya ubongo wake juu ya masuala haya mazito na makubwa.

Kwanza ieleweke kwamba Simba ni taasisi kubwa, na inaongozwa kwa kufuata misingi ya sheria, kanuni na taratibu tulizojiwekea au hata tulizozikuta ambazo zipo kulinda maslahi ya Simba SC, wanachama na Taifa kwa ujumla. Mara kadhaa nimekuwa nikipigia kelele suala la katiba, na ninakumbuka nimewahi kuzungumza na kiongozi mkubwa wa club (Nisingependa kumtaja jina) juu ya suala hili na akanifafanulia vizuri kabisa na kwakweli nililazimika kumuelewa kwasababu kama ningeongea ninachokifahamu na nilichokuwa nakiona pengine tusingemaliza mazungumzo, japo nami nilimpa ushauri ambao kama angeamua kunisikiliza pengine tusingekuwa na huu mvutano katika Club yetu, badala yake alinipuuza tu! Ni kiongozi mwenye uzoefu nadhani kuliko viongozi wote pale klabuni, ni rafiki mzuri na mtu msikivu lakini alinipuuza.

Tunapotaka kubadili mfumo wa uendeshaji ambao utahusisha mali za Club na wanachama wake, basi utaratibu wake ni tofauti na ule wa kubadilisha uongozi kwa njia ya uchaguzi , na tofauti kubwa inaanza kwenye katiba na kisha yanafuata mengineyo. Katiba kongwe ya Simba ambayo ndio inatumika kupata marekebisho ya hizi katiba zingine (ambazo kwa bahati mbaya ndio sisi wanachama tunazifahamu) inabidi ipitiwe na kubadilishwa katika hali ya haki na uwazi. Ni hatari kubwa ikiwa patakuwepo na mazingira ya ujanja-ujanja katika kubadili katiba itakokuwa na dhamana ya club yetu.

Simba Sports Club ina katiba ya Kiswahili, ambayo inaitumia kujiendesha nap engine katika baadhi ya maeneo inatambulika kwa jina hilo. Lakini ukweli ni kwamba mali zote za Simba Sports Club zinamilikiwa na Sunderland Sporst Club na ndio yenye kutambuliwa na pekee inayoweza kufanya maamuzi juu ya Club yetu. Katiba Ya Sunderland ipo katika lugha ya kiingereza, ninayo na nimesoma neno moja mpaka lingine na kwa uchache nitaeleza hapa kilicho ndani yake na kwanini bila Sunderland SC hakuna mabadiliko juu ya Simba SC.

Baraza la wadhamini ndio chombo pekee chenye nguvu na mamlaka juu ya shughuli za Club ikiwa ni pamoja na kumsimika Rais kuwa kiongozi wa club. Sasa utakumbuka vizuri kwamba Aveva hakukutana na baraza hili kwa ujumla wake ili akabidhiwe Club yetu, alifanya “ubabe” tu na kuendelea na mambo yake.

Baraza la wadhamini ni wazee wenye mapenzi na Club, hawapendi misuguano na machafuko ndani ya Club, ni wazee ambao wana hekima ya kutosha. Wameacha Aveva aendeshe Club anavyotaka kwa katiba batili, wamewaachia kila mali ya Club watumie na wafanye wanavyotaka , wakawapa kimya cha kutosha tu katika mambo mengi amabyo kama wangeamua kuyasimamia basi Club ingeingia katika migogoro isiyokwisha. Baraza la wadhamini halikuona “hatari” kuwaacha hawa wakina Aveva kumaliza muda wao ili waje wengine, kwakuwa tu Club ilikuwa salama na inashiriki ligi kuu Tanzania.

Aveva na watu wake hawajatosheka na uhuru huo waliopewa, hawakuona kama “kupuuzwa” kule kuliwatosha, sasa wanataka kuvuka mpaka waliowekewa. Hapa ndio Baraza hili limesema HAPANA!! Mipaka iheshimiwe na wacheze katika eneo lao. Simba walikuwa huru kutafuta wadhamini na kufanya kila njia ya kuinua uchumi bila kubugudhiwa na baraza hili kwani kwa kufanya vile hata kama hawatumii katiba halali na labda jina lenyewe silo, haikuwa na madhara yoyote na haina athari katika milki na jina la Club. Lakini suala la kubadili umiliki wa Club sio jambo dogo nan i lazima baraza la wadhamini washirikishwe, na kimsingi walitakiwa kwenda kuwaona hawa wazee.

Hakuna anayepinga mabadiliko, na hayupo! Lakini kinachotakiwa ni kufuata njia sahihi kuyafikia mabadiliko na sio njia ya mkato. Hawa wazee mnaosema wana “njaa” ndio walipoteza muda, mali na kila kitu chao kuifanya Simba iwe hapo. Vijana wa juzi hapa wamejaa upumbavu kichwani huja na kuongea ujinga usio maana, bila hawa wazee hii Simba unayo”shoboka” ibadilishwe ungeikuta? Bila jasho, damu na afya za hawa wazee leo ungejivunia nini mpumbavu wewe? Ni kwanini tunakosa akili kwa kiwango hiki? Hekima ya hawa wazee kutoingilia uongozi katika masuala yooote hatujaiona? Wewe uliyeikuta Simba ipo uwanjani unatoa wapi uchungu zaidi ya hawa wazee walioikuta Simba mtaani? Hujioni ni mpumbavu??

Mimi mnanitusi na kuniuliza nachangia nini club mpaka niwapinge na mabadiliko yenu! Jibu ni kwamba sichangii kitu, haya na hawa wazee nao mtasemaje?? Kwamba wanataka wapewe pesa na “MO”, hivi na uzee ule mzee wangu Kilomoni atake pesa ya nini? wangeweza kufanya hivyo walivyokuwa vijana tena wakiwa na mamlaka ya moja kwa moja, lakini waliiacha wakijua na sisi tutakuja au pengine wakati ulikuwa haujafika, si vyema na ni utovu wa nidhamu kuhusisha tama ya pesa katika mchakato huu, hasa kwa hawa wazee.

Kwanini tusitafakari uzembe wa viongozi wetu wa hivi sasa ambao hawajaweza japo kuongeza tofali moja juu ya jingo la Club ambalo lilijengwa na hawa wazee kwa pesa zao za mfukoni na ufadhili wa “kuunga-unga”, leo hii mpira umebadilika na soko limekuwa kubwa, lakini viongozi wetu wameshindwa kabisa kuendelea pale walipoishia hawa wazee, zaidi sana wanafanya kazi ya kuibakiza timu ligi kuu. Mafanikio makubwa ya Simba yalipatikana muda mrefu uliopita, bado tunawalaumu hawa wazee? Inakuwaje kama nao wanajiuliza hawa vijana wanashindwaje kuendesha timu kwenye soko kubwa la udhamini kama hili ikiwa sisi tuliweza kwenye soko dogo? Inakuwaje kama hawa wazee hawaoni sababu ya mabadiliko ya umiliki kwakuwa wameona ni wapi tulikosea?? Ni lini Aveva ameenda kuongea na hawa wazee angalau kuwaomba ushauri namna ya kuendesha kwa mafanikio? Sasa kwanini anataka kupita njia ya mkato?

Aveva anaweza kueleza kwanini kashindwa na kipi kimemfanya ashindwe? Anaweza kueleza changamoto za kiuongozi na vipi amejaribu kuzitatua? Anaweza kueleza yeye kama Rais wa kwanza wa Club ni kwanini haoni umuhimu wa kuwa na mtendaji wa wadhafa huo katika maendeleo ya club na badala yake anataka pawepo na aina tofauti ya umiliki? Aveva anaweza kuthibitisha kwa takwimu ni kwa namna gani ameongoza na kuendesha shughuli za Simba kwa hasara? Aveva anaweza kutoka na kuwambia wanachama ni wapi anapata fedha na kwa makubaliano gani kwa ajili ya kuendesha club bila kuwa na mdhamini kwa nusu ya msimu ikiwa wakati mdhamini akiwepo alikuwa analalamika fedha haitoshi?? Aveva anaweza kutwambia ni kwanini hashirikiani na baraza hili ambalo ndio linamuidhisha kwa mujibu wa katiba?? Anaweza pia kutueleza mipango tofauti ya mabadiliko zaidi ya mpango huu wa Hisa?

Mwishoni huku napenda niwaeleze aina za wanachama kwa mujibu wa Katika ya Sunderland Sports Club ambayo ndio mmiliki wa Simba Sports Club (najua hutaki kuamini na pengine inakuchanganya, lakini sio kosa langu, ni ukweli wa mambo huo. Hukana kitu kinachoitwa Simba Sports Club unapokuja kwenye mali za Club), nitajitahidi kukumbuka kadri ya uwezo wangu, ukiwa mfuatiliaji wa mambo kuna raha yake, sio kutoa povu tu kama zuzu! Kuna aina nne za wanachama katika katiba ile, jichuje halafu niambie wewe ni aina gani ya mwanachama na haki zako ni zipi:-
a) Lifetime Membership
b) Permanent Membership
c) Ordinary Membership
d) Temporary Membership

Na labda nikuulize, unawafahamu wajumbe wa kamati ya utendaji ya Simba Sports Club? Unafahamu kwamba Jonas Mkude kwa hivi sasa alitakiwa kuwa mjumbe wa kamati hiyo?? Nadhani inafahamika kwamba Simba ilikuwa na timu za michezo tofauti na mpira wa miguu, hivyo basi Wajumbe ambao wamesahaulika katika kamati ya utendaji kwa mujibu wa Katiba hii niliyonayo kule nyumbani ni
a) Team Captain
b) Librarian
c) Treasurer
d) Sports Secretary

Kuna jambo unaweza kung’amua hapo? Wapo watakaouliza kwamba inakuaje hawa wazee walikuwa kimya muda wote lakini wanajitokeza wakati wa mabadiliko? Jibu ni dogo tu bwana Kilaza, hapo kabla shughuli za klabu hazikugusa maslahi mapana ya club na hazikuwa hatarishi, lakini hii ya sasa hivi ni hatari sana, na tushukuru kwamba tumekuwa na wazee wenye busara sana na waelewa, hawakutaka kutuvuruga mpaka walipoona tunataka “kuvurugwa” ndio wameingia kati.

Imani yangu ni kwamba uongozi wa Simba wanajua yote haya, Aveva hana nyaraka yeyote ya kumuwezesha kubadili mfumo wa Club, na kama anayo atoke hadharani awaoneshe wanachama, nami nitatoka hadharani na nyaraka halali (nitaenda kuziomba kwa wazee wangu, mimi sina nyumbani tafadhali sana) ili tuamini anachokiongea ni sahihi. Aveva labda anamrubuni Mohamed Dewji “MO” ili aendelee kuifadhili Simba SC katika kipindi hiki kigumu lakini anajua wazi hatoweza kufanikwa na anawatumia wanachama kumuaminisha “MO” kwamba mambo yanakwenda vizuri. SI KWELI!

Hakuna njia ya mkato katika jambo hili, hata huyo muwekezaji ikiwa atakubali kwa “kiburi” basi atajichafua kwa kesi nyingi mahakamani ambazo mwisho wa siku atashindwa, na tutakuwa tumewaonesha wawekezaji wengine kwamba sisi hatuna umoja. Bado ushauri wangu niliompa kiongozi wa juu wa Club una mashiko na ni vema wakaufanyia kazi badala ya kuupuuza, maridhiano ni hatua kubwa na nguzo muhimu katika ustawi wa haki, demokrasia na utawala bora. Hatujafikia hatua ya kuwa na makundi ndani ya Club yetu, tunayo nafasi nzuri ya kuokoa muda na kuweka msingi wa mabadiliko ya kweli kwa kuanzia pale tulipoaanguka.

Mchakato kama huu ni lazima uwe na marekebisho kuanzia 1974 mpaka sasa, ili tuwe na kitu kimoja cha kueleweka na kitakachotusaidia kutambua ni aina gani ya mabadiliko tunahitaji. Rai yangu kwa wanachama hasa vijana, waache kukurupuka na kutumia muda huu kuwaza kwa upana na kufuatilia kwa kina historia ya club kiuongozi na sio historia ya uwanjani, wengi wanapewa msukumo na masuala ya uwanjani na hawafikirii mustakabali wa club yetu. Kwangu naona ni ujinga na wanafaa kupewa elimu upya ili kuwasaidia kufikiri na tuwaamini.

HATE ME NOW, THANK ME LATER!

Jeff Gemo Mnyama Machine,
The One Man Army,
Affirmative Gemo The Great!

[HASHTAG]#SeriesFreeLife[/HASHTAG]
Season Two | Episode 7
 
Hakuna anayekuchukia. Haya unayoyasema ungeenda kwenye mkutano. Wenzako 19 walipinga. Wazee walijaribu kutumia court order ikashindikana. Madai yao yakaonekana hayana mashiko. Huko nyuma nilikushauri nenda kwenye mkutano. Hata kama hupendi aina ya mabadiliko au una bifu na uongozi uliopo which is more likely,wanachama wa Simba wameamua kwa majority kubwa tu 98%.
Timing ya hao wadhamini ambao ni watatu inatia mashaka. Mchakato ulianza 31 July 2016 hawakusema chochote. Baraza la wazee wametoa tamko kuunga mkono mkutano wa leo kupitia kwa katibu wao Mzee Omar Mtika.
 
Watanzani ni kama kirusi cha HIV, ukiki-set namna hii basi kinajigeuza namna nyingine, ukifanya hivi chenyewe kinafanya vile.

Nimeoona stooory ndeeefu kumbe nawe ni wale wale, mkiambiwa toeni hata za chai za wachezaji mtaanza kuorodhesha watu wanaoweza kuisaidia Simba... Nani atoe hela yake bure kwa sasa bila ya yeye kupata faida. Mbona ninyi watu ni wagumu sana wa mabadiliko, ukweli mmeenea sehemu nyingi na katika kila sekta. Ni kama wachawi wa maendeleo ya kila kitu Tanzania.

Simba kila leo inalia ukata, mmeshawahi kwenda pale Kariako wewe na wazee wako kuisaidia Simba, machungu gani hayo mnayoyasikia ninyi tu wakati hamtoi hata msaada.

Simba inashindwa kusajili wachezaji wazuri sababu ya pesa. Ninyi mmekalia maneno tuu.

Ichukueni basi ninyi na wazee wako hao, mkishindwa tafuteni kazi nyingine muache kupenda fedha walizotoa wanaume wengine.

Shida sana nchi hii, wajuaji wengi sana!
 
Hizi ni hekaya tu!wakati wa storistori umepitwa ...wacha mabadiliko yaingie hamna namna
 
Hawa watu bado mbumbu na mawazo yao ni pumba tupu.Hawa kina Kilomoni,Ramesh Patel wana interest zao na mali za Simba.MO amtoa ofa ya kununua hisa kwa tzshs bilioni 20 kwa asilimia 51 na amewachia wanachama / mashabiki 49%.Lkn mie siamini kama assets tulizonazo zina thamani ya zaidi ya bilion 10 kama hawa kina mzee Kilomoni wanavyotaka tuamini hivyo.Hayo majengo machakavu yanatusaidia nini ktk kipindi hiki cha globalization?....Kila viongozi wakichaguliwa ni kukarabati jengo la klabu na kodi jengo zima kwa mwaka ni 24 million na mshahara wa wachezaji kwa mwezi ni zaidi milioni 30....sasa hapa wazee wetu kina Kilomoni mtupishe mkae pembeni akacheze zumna ....waachieni wenye uchungu wa kweli wa klabu waliojitolea kuleta mabadiliko chanya ya kuleta maendeleo ya klabu kama TP Mazembe,Al Ahly n.k.Twendeni mbele SIMBA, Nguvu moja na muda ndio huu wa kufanya mabadiliko na treni imeshaanza kushika kasi.
 
...
Katiba kongwe ya Simba ambayo ndio inatumika kupata marekebisho ya hizi katiba zingine (ambazo kwa bahati mbaya ndio sisi wanachama tunazifahamu) inabidi ipitiwe na kubadilishwa katika hali ya haki na uwazi. Ni hatari kubwa ikiwa patakuwepo na mazingira ya ujanja-ujanja katika kubadili katiba itakokuwa na dhamana ya club yetu.
Lakini kwa bahati mbaya au nzuri, katiba hiyo unayosema tunaifahamu wanachama ndio hiyo tu iliyosajiliwa na mamlaka husika nchini!
 
Simba ni kama bidhaa nyingine yoyote. Iuzwe tu. Mnunuzi atakuwa na haki ya kuiuza kwa faida kubwa siku za usoni.
 
Ikiwa kiongozi ambaye umedai kuwa ni rafiki yako wenye uzoefu alikupuuza hata sisi tunakupuuza tu

Miaka yote Timu ipo mnasaidia nini nyingi..? nyasi za uwanja katoeni pesa basi, acheni kutuletea mfumo wa kizamani hapa.
 
Hakuna anayekuchukia. Haya unayoyasema ungeenda kwenye mkutano. Wenzako 19 walipinga. Wazee walijaribu kutumia court order ikashindikana. Madai yao yakaonekana hayana mashiko. Huko nyuma nilikushauri nenda kwenye mkutano. Hata kama hupendi aina ya mabadiliko au una bifu na uongozi uliopo which is more likely,wanachama wa Simba wameamua kwa majority kubwa tu 98%.
Timing ya hao wadhamini ambao ni watatu inatia mashaka. Mchakato ulianza 31 July 2016 hawakusema chochote. Baraza la wazee wametoa tamko kuunga mkono mkutano wa leo kupitia kwa katibu wao Mzee Omar Mtika.
Siyo 98% tu 99.5 maana waliokataa ni 3 kati ya 600 na
 
Ikiwa kiongozi ambaye umedai kuwa ni rafiki yako wenye uzoefu alikupuuza hata sisi tunakupuuza tu

Miaka yote Timu ipo mnasaidia nini nyingi..? nyasi za uwanja katoeni pesa basi, acheni kutuletea mfumo wa kizamani hapa.
Akamuulize Ustadhi jana kashinda amefadhaika ameshindwa akubali mabadiliko au akatae.
Tatizo watu walishazoea kuvuna bila jasho.
Kama huna kazi nenda kijijini kwenu ukalime hatutaki porojo
 
Kuzungumzia Sunderland ni sawa na kuzungumzia Tanganyika na TANU ambavyo havipo vilibinafsishwa viwanda na mashirika ya umma kwa nini timu ishindikane kaa kando acha mabadiliko yafanyike kama Mwl alivyoona viwanda vyake vinabifsishwa akuzuia pamoja na kwamba hakutaka
 
Aina ya mawazo ya mtoa mada ndiyo waliosababisha timu yetu kuitwa wamatopeni. Hivi unadhani baraza la wadhamini linauchungu mkubwa na timu kuliko Mo kama wanauchungu zaidi kuliko Mo waambie huo uchungu hatujauona ukileta positive impact kwa simba zaidi ya kuididimiza klabu.
Timu ya simba imefikia mahali haina tofauti na stand united kutokana na hao wanaosema wanauchungu na klabu mungejua tunavyoumia huku mtaani kwa kutukanwa na wapenzi wa timu nyingine ungeufyata.

Nawapongeza sana tena sana wale wataka mabadiliko kwa ushindi wa jana
 
Hawa watu shida kweli kweli.... Wanakurupuka tu. Kufikia kiwango cha Yanga kunahitaji muda..
 
Hawa watu shida kweli kweli.... Wanakurupuka tu. Kufikia kiwango cha Yanga kunahitaji muda..
Wewe wanaume wanajadiliana funga kanga kapike. Mkodisho wenu umepigwa stop na mahakama mkaufyata.Timu inakodishwa kama masufuria ya hitma halafu bado una uso wa kufungua mdomo. Court order mmeshindwa kuitoa. Mkutano wenu ukaishia hewani. Watu wanapozungumzia mustakbali wa klabu yao wewe kampikie mumeo.
 
Mtoa mada hebu twambie Simba ina mabaraza ya wadhamini mangapi?
kwanini wafatwe kupigiwa magoti? kwani hakuna utaratibu wa kukutana mpaka mfatwe?
Je nyie mnatambulika na Simba?
 
Back
Top Bottom