Hakuna mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA Taifa nje ya Tarime anaweza kumpigia kura John Heche nafasi ya Makamu Mwenyekiti

Propaganda, heche Yuko serious Sana.Kumpigia kura agent wa Abdul ni kuizika chadema
 
Heche alikuwa mwenyekiti wa BAVICHA taifa.
 
Mimi ni mjumbe, natoka Songea nitampigia Heche, na tumejipanga.
 
Jadili kuhusu katiba mpya sio uchaguzi wa chadema usio na tija kwa taifa!
 
Wenje hawezi kushinda..mchango wa Heche kwa chadema ni mkubwa kuliko Wenje! Lkn pia Tukio lake kuhusishwa na Abdul km daraja kumfikia Lisu linamuondolea sifa kupewa dhamana kuongoza chama..wenje na Lisu hawafai wao waende wakaungane na Abdul kufanya biashara..siasa imewashinda!
 
Ona huyu
 
Mbona uchagyzi wa ndani wa CCM huoni wakitukanana au kukashifiana?
Wanaogopana maana wako madarakani. Acha siku nao wawe wapinzani utaona mambo.

Wakati huu ukim challenge mkuu yeyote anaweza sema " ashikwe huyu".
 
We POPOMA KWELI πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€£πŸ€£πŸ˜ƒ Sasa mbona unatoa siri???
 
Wenje kawanunulia Suti za Mdahalo akina Yeriko πŸ˜‚πŸ˜‚

Chadema mko kizamani sana 🐼
Tunasibiri tuone ushindani kama huu wa cdm kwa chama cha mbeleko ya vyombo vya dola. Cdm wameleta hamasa sana kwa kufanya ushindani wa kisiasa wa midahalo ya wazi, watu wanalumbana kwa hoja. Chama la majizi ya kura sasa, hakuna midahalo, lakini utasikia mwenyekiti wao kapata kura 100%!
 
Mbona uchagyzi wa ndani wa CCM huoni wakitukanana au kukashifiana?
Ccm sio chama cha siasa ndio maana huoni midahalo ya kisiasa. Huko ccm mshindi anatangazwa sio kwa kura wala sera, bali maagizo toka juu.
 
Nadhani tuache Kampeni zichukue Mkondo wake, Maana halisi ya Kampeni ni kushawishi waliokuwa upande mwingine kuja upande wako
Tatizo linakuja kwanini wavuane nguo kiasi kile au ndo demokrasia??
 
Mbowe ni mwizi kama wezi wengine, huiba pesa za chadema kisha kuzitakatisha kwa kisingizio kuwa alikikopesha chama madeni hewa, Mbowe anatumia pesa nyingi kuununua uenyekiti
 
Wajumbe wengi Taifa wapo na Lisu na Heche moyoni lakini machoni wapo na mbowe kwa kuwa anawapa pesa nyingi sana, sasa ni kula kunywa kunawa kwa mbowe lakini kulala ni kwa lisu, ni pesa anayogawa mbowe pekee inamdanganya kuwa anapendwa na Wajumbe
 
Tatizo linakuja kwanini wavuane nguo kiasi kile au ndo demokrasia??
Nguo zipi wanavuana? Nini maana ya kampeni? Maana ya kampeni ni kila mmoja kuongea dukuduku zake ingawa Timu mbowe licha ya kutumia pesa wamezidisha propaganda zaidi ambazo badala ya kuwasaidia zinawaharibia zaidi
 
Wajumbe wanakula pesa za mbowe kama mchwa na wachache wamejitoa fahamu wanakesha mitandaoni kutengeneza Uongo wa kila aina juu ya heche na lisu ili wamfurahishe mbowe aendelee kuwapa pesa , kwa sasa kuna wimbi na kikundi cha wala pesa za mbowe ndiyo wamekuwa wasumbufu mitandaoni, yafaa wamshukuru Lisu na heche kugombea uenyekiti na makamu kwani imepelekea wao lupata Dili kubwa toka kwa mbowe na sasa wanakula pesa nyingi huku kamati ya Roho mbaya ikiongozwa na mdee, Boniface na wenje wakihaha saa 24 kumdhoofisha Lisu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…