Hakuna mkataba wa mradi wowote wananchi tumewahi kuhusishwa kuupitia. Huu wa Bandari ya Bagamoyo hawawezi kuuweka wazi

Sasa unavyoona wanaapa kila siku kulinda siri unafikiri ni siri zipi?
 
Afadhali hata kama wangekuwa wanavimbiwa! Tatizo wanamatumbo kama ile "blackhole" kwenye galaxy! Hawashibi, hawatosheki, hawashibi?!
Sasa twajiuliza binadamu gani hawa kila kukicha wanawaibia tu wananchi wao bila kikomo?!
 
Mikataba mingi ina kifungu cha usiri (confidentiality), ambacho ninamaanisha kifungu ambacho kinazuia wahusika (Authorized personnel) kwenye mkataba kutangaza, au kufichua wengine habari zingine in (public).

Kwa ufupi mikataba mingi ipo CLASSIFIED
 
Hili jambo ni la Watanzania wote bila kujali Itikadi za Vyama vyao

Inakuwa ni Okoa Jahazi Movement.
Watu wana masilahi yao tofauti tofauti kwenye siasa sasa sijui hao watu wataongonishwa na nini?
 
Jikite kwenye maada husika mkuu! Naona unahangaika Sana na Mbowe, sijui kakufanyaje? Inabidi umfungulie uzi maalum
 
eti Nchi HURU inayoficha MIKATABA YAKE inayoingia na wawekezaji kwamba ni SIRI. . na endapo mwananchi ukatumia mbunu zao ukauchapisha mkataba huo kwa umma utashitakiwa kwa kukutwa kwa kusambaza SIRI za Serikali yaani kosa lako na la yule aliyekutwa na NYARA ni sawa....

Tuna safari ndefu sana Watanzania - Uhuru wa kweli bado HATUJAUPATA, kunarudi kulekule KATIBA iliyopo inawapa Watawala JEURI ya kufanya watakavyo !!
 
Babu achana na mbowe hapa mada ni kuhusu mikataba kuwekwa wazi raia nao wShirikishwe

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…