A
Anonymous
Guest
Habari,
Ninaishi Arusha, na nimekuwa nikikabiliwa na changamoto ya bili kubwa za maji ambazo hazieleweki. Kwa muda wote nimekuwa nikiishi hapa tangu mwezi Julai, bili ya maji imekuwa ikija ikiwa si chini ya Sh 80,000.
Awali, nilidhani huenda kuna siku nitakutana na msoma mita ili nipate kumuuliza kuhusu hali hiyo. Hivyo, nilitoa taarifa kwa wapangaji wote ndani ya nyumba kwamba yeyote atakayemuona msoma mita ya maji anijulishe. Sikueleza sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa nilitaka kwanza kufanya uchunguzi wangu mwenyewe.
Nyumba ninayoishi ina geti, na mita za maji zipo ndani ya ua. Mtu yeyote anapoingia ndani, hata kama upo chumbani, ni rahisi kusikia au kugundua uwepo wake.
Cha kushangaza, kwa takribani miezi minne sasa sijawahi kumuona wala kusikia msoma mita akifika kusoma mita za maji, lakini bili zinaendelea kutoka kila mwezi zikiwa na kiasi kikubwa cha fedha.
Nina uhakika wa asilimia 100 kwamba katika kipindi hicho hakuna msoma mita aliyefika hapa. Hali hii inanipa maswali mengi kuhusu namna bili hizi zinavyotengenezwa na msingi wa makadirio ya kiasi cha maji kinachotumika.