Execute
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 3,000
- 7,336
Kwa mujibu wa maelezo ya watu waliokuwapo ndani ya ndege na kufanikiwa kujiokoa, ndege ilijaa maji ndani ya dakika moja tangu ilipoanguka ziwani. Walilazimika kupanda juu ya viti upande wa nyuma.
Ushahidi wa picha za ndege ilipokuwa ziwani unaonesha upande wa mbele wote ukiwa ndani ya maji. Hakuna uwezekano wa mtu aliyekuwa nje kuweza kuona ndani kupitia kioo cha mbele kwasababu kulikuwa na giza kutokana na maji yaliyojaa.
Mfumo wa kielektroniki wa ndege ulikuwa umezimika baada ya kuzimika kwa injini hivyo kusingeweza kuwa na mawasiliano. Hata ukiangalia ndege baada ya kutolewa unaona dhahiri kwamba maji yaliingia kupitia upande wa chini ulioharibika.
Sasa natoa wito kwa shujaa Majaliwa na mkuu wa mkoa wa Kagera ndugu Chalamila kujitokeza na kuomba radhi kutokana na udanganyifu waliofanya.