Hakuna mtu aliwasiliana na rubani wa ndege iliyoanguka ziwani, shujaa Majaliwa na Chalamila watuombe radhi

Execute

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
3,000
Reaction score
7,336
Kwa mujibu wa maelezo ya watu waliokuwapo ndani ya ndege na kufanikiwa kujiokoa, ndege ilijaa maji ndani ya dakika moja tangu ilipoanguka ziwani. Walilazimika kupanda juu ya viti upande wa nyuma.

Ushahidi wa picha za ndege ilipokuwa ziwani unaonesha upande wa mbele wote ukiwa ndani ya maji. Hakuna uwezekano wa mtu aliyekuwa nje kuweza kuona ndani kupitia kioo cha mbele kwasababu kulikuwa na giza kutokana na maji yaliyojaa.

Mfumo wa kielektroniki wa ndege ulikuwa umezimika baada ya kuzimika kwa injini hivyo kusingeweza kuwa na mawasiliano. Hata ukiangalia ndege baada ya kutolewa unaona dhahiri kwamba maji yaliingia kupitia upande wa chini ulioharibika.

Sasa natoa wito kwa shujaa Majaliwa na mkuu wa mkoa wa Kagera ndugu Chalamila kujitokeza na kuomba radhi kutokana na udanganyifu waliofanya.
 
Kilichotokea kwa Majaliwa ni kisa sawa kama cha Mandonga, unapigwa lkn unakuwa maarufu kuliko mshindi. Ni bahati nzuri tuu imemdondokea Majaliwa lasivyo asingepaswa kuwa hapo alipo sasa.
 
Mkuu
Hao abiria hakuna hata mmoja aliyepiga mbizi kwenda kuangalia namnanya kuwachomoa rubani na msaidizi wake

Kuna wakati haya mambo tuwaachie wataalam, tumeshapikiwa jungu la shubiri tunalila na waheshimiwa wamefanya kikao majuzi wanaendelea kulindana huku wakititaka tuwe watulivu

Kama siyo kafara ni nini basi tunafanyiwa? Timepoteza binadamu wengi kwenye ajali hiyo.

Inauma
 
Hiyo picha unayosema maji yalijaa dk 1 moja iko wapi? Pengine una hoja sababu ndege imetoka imeharibika, lakini kama imeharibika wakati wa kuvutwa tutajuaje?

Dogo hakusema maji hayakuingia ila alisema yalikuwa yanaingia taratibu na baada ya muda yangejaa. Na kwa hali ya kawaida kama yangejaa ndani ya dk 1 wasingetoka watu 23. Yaani kusingekuwa na muda hata wa kujua kama kuna upande wa nyuma.

Hao hostees wenyewe wasingefika nyuma maana wao huwa wanakaa pale mbele ndege ikitaka kupaa au kutua.
 
Mfumo wa kielektroniki wa ndege ulikuwa umezimika baada ya kuzimika kwa injini hivyo kusingeweza kuwa na mawasiliano. Hata ukiangalia ndege baada ya kutolewa unaona dhahiri kwamba maji yaliingia kupitia upande wa chini ulioharibika.
Zamani kulikuwa na teknolojia ya kupata image ya mhalifu kupitia mboni ya marehemu, je haiwezekani kutumia Mboni ya Majaliwa aliye hai kupata image ya kile alichoona majini?

Je yote yanayosimuliwa juu ya Majaliwa yalitoka kinywani mwake baada ya kuzinduka huko hospitali au mashuhuda wa tukio? Ni nani ametia kikolezo mpaka Majaliwa kutajwa kila kona kama shujaa au ni nani hakushuhudia juhudi za majaliwa na sasa anataka kuweka usahihi wa habari haddharani?
 
Hiyo tech ya kupata image kupitia mboni ya mfu inafanyaje kazi
 
Hiyo picha unayosema maji yalijaa dk 1 moja iko wapi? Pengine una hoja sababu ndege imetoka imeharibika, lakini kama imeharibika wakati wa kuvutwa tutajuaje?
Ndege iharibike na kukatika katikati kwasababu ya kuvutwa? Hujaona upande wa chini ulivyoharibika?
Dogo hakusema maji hayakuingia ila alisema yalikuwa yanaingia taratibu na baada ya muda yangejaa. Na kwa hali ya kawaida kama yangejaa ndani ya dk 1 wasingetoka watu 23. Yaani kusingekuwa na muda hata wa kujua kama kuna upande wa nyuma.
Kama maji yangeingia taratibu sana basi hakuna mtu angekufa unless kama kifo kiwe cha mshtuko au kuvunjika.

Kuna mtu alitokea upande wa mbele ambaye anasema kilichomuokoa ni kuweza kuogelea.

Yaani maji yalivyojaa yeye alifanikiwa kufungua mkanda na kuanza kuogelea kwenda nyuma.

Ni bahati kwamba hakuzimia baada ya kile kishindo na hiyo ikawa pona yake
Hao hostees wenyewe wasingefika nyuma maana wao huwa wanakaa pale mbele ndege ikitaka kupaa au kutua.
Air hostess wanakaa mbele na nyuma. Waliopona ni wale waliokaa nyuma.
 
Shida vile vimilioni alivyopewa majaliwa.
Mmejiuliza chanzo cha ajali ni Nini?
Mmejiuliza rubani alishindwa vipi kurudi mwanza mpaka akaamua kwenda kutua ziwa viktoria?
Hivi hapo wewe huoni tatizo? Ndugu wa wale marubani wanajisikiaje kuambiwa mtu wao alikuwa hai na kuwasiliana na mkuu wa mkoa halafu wakaachwa wafe? Vipi kuhusu uongo kwamba alitaka kuvunja kioo na akazuiwa?
 
Zamani kulikuwa na teknolojia ya kupata image ya mhalifu kupitia mboni ya marehemu, je haiwezekani kutumia Mboni ya Majaliwa aliye hai kupata image ya kile alichoona majini?

Je yote yanayosimuliwa juu ya Majaliwa yalitoka kinywani mwake baada ya kuzinduka huko hospitali au mashuhuda wa tukio? Ni nani ametia kikolezo mpaka Majaliwa kutajwa kila kona kama shujaa au ni nani hakushuhudia juhudi za majaliwa na sasa anataka kuweka usahihi wa habari haddharani?
Unapo sema zamani unamaanisha zamani zipi au za muvi za kina adolf? 😁😁😁😁😁
 
Mvuvi kuona ndani ya Maji au kufanya mawasiliano ni kawaida sana

Labda ujiulize tu Nyundo ndogo ililetwa na nani?
Kuona ndani ya ndege iliyojaa maji ni uongo mkubwa. Mambo ya nyundo ni porojo za wanasiasa na muigizaji wao.
 
Ata wewe mwenyewe unaandika hakuna Kama vile ulikua eneo la tukio,Kuna mengi hatuyajui kwa hiyo hiyo Ni nadharia yako tu,vile vile maji inawezekana kweli yalikua yanaingia taratibu,na rubani kufanya mawasiliano na wa nje pia inawezekana,si ana simu ya,mkononi,na kuwasiliana na majaiwa si ata kwa body language
 
Acheni kuunga mkono uongo wa Majaliwa na serikali. Kama aliweza kufanya yote hayo kwanini hakufungua mkanda na kutoka? Mtu mmoja aliyepona kutokea pale nyuma ya cockpit anasema kilichomuokoa ni kuweza kufungua mkanda na kuogelea kurudi nyuma.
 
Back
Top Bottom