Hakuna mtu aliwasiliana na rubani wa ndege iliyoanguka ziwani, shujaa Majaliwa na Chalamila watuombe radhi

Hakuna mtu aliwasiliana na rubani wa ndege iliyoanguka ziwani, shujaa Majaliwa na Chalamila watuombe radhi

Maswali yangu mimi hayako kwa ajili ya Majaliwa wala Chalamila. Kwa majaliwa hiyo ndo ilikuwa njia ya yeye kutoka kwa sababu hajatengeneza ajali yeye. Swali ambalo tunapaswa kujiuliza kwa nini Bukoba Airport Tower controllers hawajajitokeza kuelezea mawasiliano ya mwisho kati yao na rubani? Ikiwa rubani alishatangaza kutua na kuandaa abiria manake hali ya hewa ilikuwa inaruhusu kutua, tofauti na hapo Tower controllers wasingemruhusu kushusha ndege, bali angeelekezwa kuelekea kiwanja cha jirani mara moja. Na eneo la karibu kwake lilikuwa ni Mwanza na Musoma. Na vipi rubani alishindwa kuona uwanja ili hali abiria walikuwa wanaweza kuona maeneo yote alikokuwa wanaweza kupita.
Kwa hiyo nadharia kuwa tairi za ndege ziligoma kushuka linaweza kuwa na ukweli, ukumsikiliza ABIRIA mmoja anaseka kuna muda cabin Crew mmoja alikuwa anakuja nyuma anachungulia anarudi kwa rubani kulikuwa na vitu anaangalia. Kuna abiria anasema kuna wakati rubani alitaka kushusha ndege shambani au uwanja wenye nyasi.

Lakini ndege hii PW 494 kama mwezi hivi kuna mtu aliipoti kuwa wako angani na injini moja imezima. Na walilazimika kutua uwanja wa karibu.
Soma report yote acha assumption. Bukoba hakuna control tower, rubani anatumia frequency, rubani alizunguka mara mbili mara ya tatu ndio akaona kuna angalau uono akataka kutua ila upepo ukamchota, tairi kufunguka zilishafunguka. Niendelee? Au report kwa sababu lugha ni ya malkia?
 
Sisi watanzania ni Mungu tu anatusaidia ila kwa kweli tuna matatizo makubwa kiufahamu Kwenye hili hakuna cha Msomi wa asiyesoma
Hata Mtu akisoma ndio anakuwa hovyo kabisa.

Mnaandika viposti vya kijinga kabisa kisa ni wivu wa kijana wa Watu.
Uliyeandika hii post sidhani kama unajua kuogelea Kwa kina kile Ile ndege ilipokuwa hakuna giza chini. Kwa taarifa yako Giza linakuwa kwenye kina kirefu mno. Huyu mtoto Majaliwa Hadi sasa sijaona uongo wowote amesema

Lingine. Kama wahudumu walitoa lock ya kitasa ili wapate msaada kwa watu walioko nje Sasa hapo tatizo liko wapi? Walipaswa kutoa ushirikiano ili waokolewe. Labda wewe ulitakaje?

Hivi unafikiri ni Jambo rahisi au ni ujasiri wa namna gani kusogelea chombo kama Ndege kwenye ajali ambayo hujui principles zake za uokozi wala madhara unayoweza kukutana nayo?

Wengi tunakumbuka ajali ya lory la mafuta Morogoro kilichokuwa kimetokea
Sasa twende na picha Ile pale na madhara yake.
Then Angalia Majaliwa alivyojitoa mhanga akawapa na wengine ujasiri wa kuliendea tukio
Hilo Kwangu naona linatosha Sana kusema Majaliwa anastahili si zawadi tu, Bali pia tuonyeshe tumeheshimu mchango wake na wenzie pia

Imagine wote tungeamua kuwa watazamaji na kuchukua video kusambaza mtandaoni nini kingetokea?
Naomba Sana tulinde Upendo na Mshikamano wetu, Mwenzetu akifanya Jambo nzuri tulikubali
na kumpongeza badala ya wivu na majungu
Ili wawepo akina Majaliwa wengine wa kesho watakaokubali kuingia gharama kwa ajili ya wengine

Asante. Ni hayo tu.
Soma report yote utapata majibu ya maswali yako
 
Halafu kwanini mnaamini saana maneno ya majeruhi wakati uwezekano ni kuwa wengi hawakuwa sawa immediately baada ya ajali kutokana na sudden impact.I believe nao kuna part ya story hawana hasa kuhusu efforts zilizokuwa zinafanywa nje.Wasiwe wepesi kusema
 
Ripoti ya kitaalamu inaonesha huyo Majaliwa wenu ni wa mchongo tu. Na Chalamila ni mropokaji asiye na akili.
Wataalamu gani hao, hawa hawa mandengereko?

Labda kungekua na third part isiyohusiana na serikali hapo sawa.
 
Shida vile vimilioni alivyopewa majaliwa.
Mmejiuliza chanzo cha ajali ni Nini?
Mmejiuliza rubani alishindwa vipi kurudi mwanza mpaka akaamua kwenda kutua ziwa viktoria?
Huwa wanatishwa kufukuzwa kazi akirudi maana anatia hasara kampuni
 
Shida vile vimilioni alivyopewa majaliwa.
Mmejiuliza chanzo cha ajali ni Nini?
Mmejiuliza rubani alishindwa vipi kurudi mwanza mpaka akaamua kwenda kutua ziwa viktoria?
Nchi inavilaza hii uwiiii, watu hawajadili vtu vya msingi kama hvyo wamekomalia tuu ujinga
 
Kwa hii ripoti wale wa mbele walikufa fasta kutokana na impact na pia mlango usingefunguliwa na muhudumu ingekua balaaana maji yalikua yanaingia kwa presha

Sent from my Pixel 3a using JamiiForums mobile app
Wale watu walipona simply kwasababu ndege iliangukia sehemu yenye kina kifupi. Kinyume na hapo hakuna mtu angetoka.
 
Halafu kwanini mnaamini saana maneno ya majeruhi wakati uwezekano ni kuwa wengi hawakuwa sawa immediately baada ya ajali kutokana na sudden impact.I believe nao kuna part ya story hawana hasa kuhusu efforts zilizokuwa zinafanywa nje.Wasiwe wepesi kusema
Watu walioweza kukumbuka kufungua mlango wa dharura ndio unasema hawakuwa timamu? Watu walikufa kwasababu maji yaliingia kwa presha kubwa hivyo marubani na wale wa mbele walikufa ndani ya dakika tano.

Wavuvi walisaidia kwa kuweza kuleta mitumbwi yao kuokoa watu lakini kinachoongelewa kuhusu shujaa Majaliwa peke yake ni utapeli mtupu. Ushahidi wake ni uongo.
 
Wataalamu gani hao, hawa hawa mandengereko?

Labda kungekua na third part isiyohusiana na serikali hapo sawa.
Third party wapo sana na ripoti zote zinafuata utaratibu wa kimataifa. Huoni hapo udhaifu wa serikali umeanikwa waziwazi? Ingekuwa ya ccm peke yao wangesema uongo.
 
Nchi inavilaza hii uwiiii, watu hawajadili vtu vya msingi kama hvyo wamekomalia tuu ujinga
Haya yote utayajibu vipi bila ripoti? Haya sasa ripoti imetoka na kuonesha maigizo na upumbavu uliofanywa na serikali.
 
Hiyo picha unayosema maji yalijaa dk 1 moja iko wapi? Pengine una hoja sababu ndege imetoka imeharibika, lakini kama imeharibika wakati wa kuvutwa tutajuaje?

Dogo hakusema maji hayakuingia ila alisema yalikuwa yanaingia taratibu na baada ya muda yangejaa. Na kwa hali ya kawaida kama yangejaa ndani ya dk 1 wasingetoka watu 23. Yaani kusingekuwa na muda hata wa kujua kama kuna upande wa nyuma.

Hao hostees wenyewe wasingefika nyuma maana wao huwa wanakaa pale mbele ndege ikitaka kupaa au kutua.
Rudi hapa kwenye hii komenti yako baada ya ripoti ya awali uondoe pumba.
 
Kwa mujibu wa maelezo ya watu waliokuwapo ndani ya ndege na kufanikiwa kujiokoa, ndege ilijaa maji ndani ya dakika moja tangu ilipoanguka ziwani. Walilazimika kupanda juu ya viti upande wa nyuma.

Ushahidi wa picha za ndege ilipokuwa ziwani unaonesha upande wa mbele wote ukiwa ndani ya maji. Hakuna uwezekano wa mtu aliyekuwa nje kuweza kuona ndani kupitia kioo cha mbele kwasababu kulikuwa na giza kutokana na maji yaliyojaa.

Mfumo wa kielektroniki wa ndege ulikuwa umezimika baada ya kuzimika kwa injini hivyo kusingeweza kuwa na mawasiliano. Hata ukiangalia ndege baada ya kutolewa unaona dhahiri kwamba maji yaliingia kupitia upande wa chini ulioharibika.

Sasa natoa wito kwa shujaa Majaliwa na mkuu wa mkoa wa Kagera ndugu Chalamila kujitokeza na kuomba radhi kutokana na udanganyifu waliofanya.
Kisa cha Majaliwa ni sawa na akina Nabii Tito, Steve Nyerere, Kikombe Cha babu, Mandonga, Dr Shika nk nk...
 
Rudi hapa kwenye hii komenti yako baada ya ripoti ya awali uondoe pumba.
Ripoti??!! Ripoti imeandaliwa na watu walioshindwa kuokoa watu kwa masaa sita.

Alikuwepo hapo afisa wa serikali hata mmoja kabla ya kuokolewa watu 27??
 
Back
Top Bottom