Hakuna mtu mwenye kujitambua na mwenye Akili Timamu anayeweza kuishabikia au kuiunga mkono CHADEMA kwa Sasa

Kwa kuwa Nahitaji kuona Amani ikitamalaki na siyo kuvurugwa na watu Kama chadema

Wewe unatatizo sehemu. Chadema haipo bungeni Wala kwenye Halmashauri au kwenye mitaa na vijiji, lakini inakuhangaisha. Bila Mbowe kuongelea tozo unadhani ingefutwa?. Aliongea siku moja leo Waziri kafanya mabadiliko. CHADEMA is there to stay.
 
Nyie si mlikimbia ndani ya ukumbi wa bunge la katiba, Sasa kwanini mnaanza kulia Lia hapa Tena?
Tutakaaje Rasimu mkaiongezea upupu, shombo na Kila aina ya uvundo!!!!

Chama chenye laana mkampiga Mzee WARIOBA aibu adabu hamna!!!

Tunairudisha mezani RASIMU alosimamia Judge WARIOBA, ifanyiwe marekebisho kdg, tupate Katiba mpya.
 
Hela alizotoa sabodo mlipeleka wapi Kama hata ofisi zinewashinda kujenga?

Unahangaika Sana. Unazionea donge pesa ya Sabodo lakini unafurahia ufisadi wa CCM miaka nenda Rudi. Kemea kwanza ufisadi CCM ndio uanze kuulizia pesa za chadema zimetumikaje.
 
Labda hamtambuu Samiah Kama Rais wake. Usimlazimishe kumkubali mtu asiyemtaka. Uchaguzi haramu huzaa Viongozi haramu.
 
Mtoa mada anamakasiriko Sana, watu weupe sio wazuri aisee
 

CCM ilipewa ridhaa lini?. Uchaguzi ulitakiwa kurudiwa sio kwa ujinga ule. Unatumia billioni 60 kwa kitu ambacho ukiamini.
 
CCM yenye dira na uelekeo ndio imetufikisha hapa tulipo.Mkitumia kigezo Cha maendeleo Ni kitu endelevu kuficha aibu za kushindwa kufikia malengo na propaganda zenu.
Mmekongoroa nchi wezi nyie.
 
Sasa kibaya Ni kuwa chadema umekosa Safi ya uongozi yenye kutoa msimamo na muelekeo wa chama ikaheshimika na kupokelewa na wanachama,

Huo mwelekeo wanautolea wapi? Wakati Mwenyekiti wa CCM amewakataza kutofanya siasa miaka Saba Sasa?. Unapoongea kitu jaribu kuwa mkweli
 
Tindo ndugu yangu hivi nyie si mlikimbia Wenyewe kwenye bunge la katiba? Sasa mnataka katiba ipi Tena Tindo ndugu yangu, Nenda Katoe maoni kwenye kikosi kazi kilichoundwa, Mimi Naheshimu Sana michango yako humu

Tulisusia bunge la katiba baada ya CCM kuanza kuchezea maoni halali ya wananchi. Nikatoe maoni kwenye kikosi ya nini wakati kila kitu kiko kwenye rasimu ya Warioba? Kikosi kazi ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi, wakati mchakato halali wa kukusanya maoni ya wananchi ulishafanywa na tume ya Jaji Warioba.
 
Endelea na dharau zako. Walikuwepo wengi zaidi yako walioitumia chadema Kama ngazi ya uteuzi, ila leo hawapo.
 
Atawa
Anakwenda kuwakubali covid wao na ruvuku wanapokea kama kawaida, chadema ni rubbish

Punguza ujuaji atawakubalije Covid 19 wakati kesi ipo mahakamani na wameifungua wao Covid 19. Halafu kwa ufupi ili Covid 19 warudi uanachama, inatakiwa halmashauri kuu ikae Tena.
 
Ninyi hat ofisi ya chama tu imewashinda kujenga, Sasa Nani awape nchi nyie? Si mtabomoa hata vilivyojengwa? Hamna nafasi ya uongozi kwa watu Kama nyie hapa, mtaishia kukusanyana hapo hapo ufipa kupiga stori

CHADEMA ndio agenda yako?. Mbona serikali yako yenye Kodi, tozo, mikopo na misaada imeshindwa kujenga vyoo vya shule za msingi?. Ndio nikakuambia anzia kukosoa ndani mwako.
 
Ninyi hat ofisi ya chama tu imewashinda kujenga, Sasa Nani awape nchi nyie? Si mtabomoa hata vilivyojengwa? Hamna nafasi ya uongozi kwa watu Kama nyie hapa, mtaishia kukusanyana hapo hapo ufipa kupiga stori
Ni ofisi ngapi ccm imejenga kwa fedha zake zaidi ya hizi walizorithi kutoka chama kimoja?!
 
Hata Uhuru ulionao wa kuandika na kutukana hapa Ni matokeo ya kazi njema ya CCM ya kusitawisha demokrasia na Uhuru hapa nchini

Punguza uongo. Demokrasia gani unazuia vyama vingine visifanye siasa inafanya CCM pekee yake. Halafu kuhusu Uhuru wa maoni kamuulize mwanachama wa CCM anaitwa Ndugai alichofanyiwa.
 
Punguza uongo. Demokrasia gani unazuia vyama vingine visifanye siasa inafanya CCM pekee yake. Halafu kuhusu Uhuru wa maoni kamuulize mwanachama wa CCM anaitwa Ndugai alichofanyiwa.
Mnataka mpewe Uhuru gani ndio mlizike? Mbona mnatukana viongozi wetu na Hakuna anayewakamata? CCM inachofanya Ni ukaguzi wa utekelezaji wa ilani yake
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hivi vijamaa vinalala na uoga 2025 hawatoamini macho yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…