Ndugu zangu Watanzania,
Liwake jua au inyeshe mvua, Dunia isimame au Dunia izunguke katika mhimili wake. Kamwe na katu maamuzi ya CCM ya kumpitisha na kumuidhinisha Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama yetu Mpendwa kuwa Mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM hayatabadilika wala kubadilishwa hata nukuta au herufi.
CCM haijawahi kuyumba wala kuyumbishwa wala kutetereshwa wala kutishwa wala kutishika na makelele ya watu wachache wenye uchu ,uroho na tamaa ya madaraka. CCM ikifanya maamuzi inakuwa imefanya na ndio unakuwa msimamo wa chama kizima na wanachama wote kwa ujumla wake.
Kikundi cha watu wachache ambao kwa Upofu wao wa akili na macho wanaoweza kujaribu kutaka kushawishi au kuchochea kutaka kufanya Mapinduzi ya maamuzi ya CCM hawawezi kamwe na katu kupindua au kubadilisha maamuzi ya CCM yaliyofikiwa pale Mkoani Dodoma.
CCM haikukurupuka wala kukurupushwa kumpitisha Rais Samia kuwa mgombea wake wa Urais. Ni maamuzi yaliyofanywa kwa umakini kabisa. Ni maamuzi ambayo yameungwa mkono na wana CCM wote Nchini Kwote katika kukata kiu ya mamilioni kwa mamilioni ya watanzania wenye kutaka kuona Rais Samia anaendelea kuongoza Taifa Letu.,hasa kutokana na uchapakazi wake, uzalendo wake na maono makubwa aliyonayo.
Kwa hiyo wanaotumika na kutumiwa kutaka kuleta vurugu ndani ya CCM kwa lengo la kutaka kuhujumu chama pamoja na kuleta migawanyiko na kupandikiza chuki kamwe na katu hawataweza kufanikiwa.
Wapo waliojaribu kufanya hivyo Mwaka 2015 kuitisha CCM kuwa mtu fulani asipopitishwa basi kitawaka au chama kitakufa na watu kugawana mbao . Lakini walishangaa CCM ukisonga mbele kwa nguvu ,kasi na uimara wa hali ya juu sana kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Taifa letu.
Kwa hiyo asije akatokea mtu pembeni akawa anadanganya watu kuwa yeye ndiye chama na bila yeye hakuna CCM au kwamba yeye ndiye mwenye nguvu ndani ya CCM na chochote atakacho ni lazima kifanikiwe na kutekelezwa. Narudia kusema tena kuwa CCM ni Dude Moja kubwa sana ambalo huwezi kushindana nalo maana utakuwa unashindana na nguvu ambayo huwezi kuikabili na huwezi kujua uikabili kutokea wapi na kwa silaha ipi.
Kumshambulia au kujaribu kumtageti Rais Samia kwa kumchafua au kutaka kupandikiza chuki ili achukiwe .unakuwa unajisumbua tu maana siku alipotangazwa kuwa mgombea wa CCM uchaguzi ujao akawa tayari ni mali ya CCM na wana CCM wote. Kwa hiyo vita yoyote ile itakayo inuka inakuwa ni vita ya wana CCM wote na chama kwa ujumla wake. Adui wa Rais Samia ni adui wa CCM yote na wana CCM kwa ujumla wake. Kwa hiyo vita yake ni kubwa sana kwa yeyote atakaye jaribu kumtikisa au Kumyumbisha au kumhujumu Rais Samia kwa sasa.
Uwe tayari kupambana na mamilioni kwa mamilioni ya wanachama,wafuasi na wakereketwa wa CCM kabla ya kumfikia Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Anayetaka kufanya hivyo ni lazima ajipime na kujitathmini Kabla ya kuja kujutia baadaye. CCM tulishakula viapo vya kulinda viongozi wetu na wagombea wetu kwa kuwapigania mpaka tone na dakika ya mwisho. Kwa umoja wetu tutamlinda na kumtetea Rais Samia kwa gharama yoyote ile iwayo.
View attachment 3413439
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.