Hakuna mwanamke mwenye mdomo mbele ya mumewe

Nakadori

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
8,778
Reaction score
21,010
Wanaume wamekuwa wakilalamikia baadhi ya wanawake zao kwamba wana midomo na wamekuwa na gubu na ndio sababu kuu ya wengi kuendeleza michepuko. Sasa mimi kwa imani yangu ninaamini kwamba hiyo midomo, kauli chafu na gubu ni matokeo ya mwanaume kuanza tabia chafu, kutomjali mke na kumuoneshea dharau. Wanawake wanapolalamikia hali hizi ndipo wanapoonekana kwamba wana gubu na midomo.

Huwezi kugundulika una michepuko halafu utegemee mkeo aendelee kuwa kimya...anayekuwa kimya ujue kuna nati zimechia mahali au anapanga revenge.

Huwezi kutosimamia familia yako ikiwemo kuwajali watoto na mkeo kwa mavazi, chakula, afya na elimu halafu utegemee kumuona mkeo akiwa kimya...kama atakuwa kimya basi una msaidizi au pia kuna nati kwenye kichwa cha mkeo haijakaza vizuri.

Sasa wababa amua kuwekeza kwenye furaha ya mkeo halafu uje utoe mrejesho maana nyumba itageuka mbingu ndogo. Halafu kumbuka huyu mwanamke unayemuona Ana gubu Leo ni yuelyule ambaye ulimtongoza na ukamuona anafaa kwa ndoa.
Asanteni. Ngojaikampikie uncle wangu.
 
Wanaume wamekuwa wakilalamikia baadhi ya wanawake zao kwamba wana midomo na wamekuwa na gubu na ndio sababu kuu ya wengi kuendeleza michepuko. Sasa mimi kwa imani yangu ninaamini kwamba hiyo midomo, kauli chafu na gubu ni matokeo ya mwanaume kuanza tabia chafu, kutomjali mke na kumuoneshea dharau. Wanawake wanapolalamikia hali hizi ndipo wanapoonekana kwamba wana gubu na midomo.
Mbona mna maneno mengi wanawake! Hayo mahitaji ya familia kwani hadi mwanume tu,huu usawa mnao upigania upo wapi?, unakuta mwanamke umeajiriwa tena sehemu nzuri tu ila kila kitu unataka afanye mme kwenye familia,hela zenu hazionekani ,muwe na kazi au msiwe na kazi tofauti haipo.

Endeleeni kulalama tu,mm huwa siwaelewi tangu mkiwa eden, shida yenu haijawahi isha.
 
Tatizo lenu ni uchoyo tuu. Sasa wewe mwanaume gani rijari na ana hela anagegeda mwanamke mmoja?
 
Mbona mna maneno mengi wanawake! Hayo mahitaji ya familia kwani hadi mwanume tu,huu usawa mnao upigania upo wapi?, unakuta mwanamke umeajiriwa tena sehemu nzuri tu ila kila kitu unataka afanye mme kwenye familia,hela zenu hazionekani ,muwe na kazi au msiwe na kazi tofauti haipo.

Endeleeni kulalama tu,mm huwa siwaelewi tangu mkiwa eden, shida yenu haijawahi isha.
Ukitaka stress ingia kwenye ndoa ukitegemea kuwa mke atakusaidia majukumu.
 
Ni ukweli mchungu lakini Nakadori amegusia mambo ya muhimu. Inabidi tuukubali tu wanaume.

Mie kinachonikera sio mtu kueleza mawazo yake au kunikumbusha wajibu na majukumu yangu, ila ile njia anayotumia au namna anavyoongea, hiyo ndio mara nyingi inachefua wanaume.

Lakini mwanamke akitumia njia ya staha na ustaarabu kueleza shida yake au dukuduku lake, wanaume wachache sana wataleta ukorofi. Kwa ufupi hatupendi makelele na kufokewa. Hapo tu ndio hua mnaharibu.
 
Back
Top Bottom