Hakuna mwanasiasa/Rais aliweza kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na akashinda!

Hakuna mwanasiasa/Rais aliweza kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na akashinda!

Angalia utachekwa sana kwenye huu mjadala unapiga Dana Dana na kuruka ruka! Hata yeye akisoma atakushangaa.
Wewe tuambie walifanikiwa nini?
TEC walipiga jalamba makanisani nchi nzima kumwangusha JK, mpk wagalatia wa CCM wakaungana na kanisa.
Mtoto wa mjini akaiingiza familia yake kwenye kampeni mwisho wa siku hiyo TEC haikuweza kumweka Padri Slaa
 
Kwa kifupi kabisa, Viongozi wa Serikali yetu hawawezi hata kidogo kushindana na TEC.
TEC hawana tabia ya kuropoka ropoka, lakini wana power kweli kweli.
Ilikuwa zamani hiyo enzi za Nyenyere.
Sasa hv wanaropoka hovyo hovyo tu dalili za kuishiwa
 
kutoka ndani ya korido za vatican

1 . dubai wakipewa bandari mfumo wa udini utakua kwa kasi na kuleta mpasuko mkubwa
2. kuna agenda ya siri nyuma ya bandari kwamba wakishaingia rasmi.. taratibu watahakikisha mfumo wa utawala na uongizi nchini unatoka dini ya kiislam...
3. vikundi vya kigaidi vitaibuka na upitishwaji wa silaha kiholela utaongezeka kwa kasi kubwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe(watanzania) yataibuka
4.mfumo wa ajira utakuwa wa dini moja ya kislam na kuwacha wakristo kwa idadi kubwa bila ajira
5. umasikini utaongezeka kwa kasi kubwa maana bandari zote na maeneo mengi ya nchi kavu yatakuwa mikononi mwa waarabu na wazawa watapewa mashart magumu sana hata kufika maeneo hayo.
6. watahakikisha bara inaingia kwenye machafuko na hapo zanzibata itavunja muungano..ikumbukwe bandari za zanzibar hazimo kwenye mkataba.


'' the vatican intelligence and its fields of resources are second to none''
Utamani iwe hivyo?
 
Wewe tuambie walifanikiwa nini?
TEC walipiga jalamba makanisani nchi nzima kumwangusha JK, mpk wagalatia wa CCM wakaungana na kanisa.
Mtoto wa mjini akaiingiza familia yake kwenye kampeni mwisho wa siku hiyo TEC haikuweza kumweka Padri Slaa
Ulisimuliwa au ulikuepo? Slaa lini aligombea urais na lini alionesha Nia ya kugombea urais,

Tupe evidence Moja au mbili TEC wakimdenouce JK, na utaje hao watu kutoka huko Galatia waliojounga na kanisa Kwa muktadha huo..
Na utuambie bila shaka familia ya JK iliyoingia kwenye kampeni na uwataje Kwa majina na roles zao. Vinginevyo wewe ni mwimba ngonjra.

TEC haijawahi na haitawahi kumfanyia mtu kampeni awe Rais awe mpagani au mwislamu au mkristo. Umeandika uwongo
 
Jifunze hta kuandika 🤣🤣...Mimi sili rushwa wala kulewa ni haramu kwangu kabisa..

Nataenda haki na sio kuwa mjinga wa kupelekwa na tamaa za kidunia ,naheshimu mawazo ya kila mtu bila kuleta vitisho kama kikund chenu cha ngoma hicho .
Kulewa kwako ni haramu ila RUSHWA,KUUWA NA KUPORA MALI ZA WATU ni halali kwako.
 
Mbona unahama mada,kwenye post yako unasema Magufuli alipingana na TEC kwenye kuvaa barakoa na akashindwa.
nikakujibu Magufuli hakupinga barakoa ila alitoa tahadhari ya barakoa zinazotoka nje.

nikasema ni kumchafua Magufuli kwamba alipingana na TEC wakati si kweli,Magufuli hakuwai kupingana na taasisi yeyote ya dini hata waraka wa TEC wa kupingana na Magufuli kuhusu Covid haupo ni uzushi wako tu wa kusema alishindana na TEC na akashindwa.
Jibu ni kwamba ALIPINGA hakuna cha kuhama mada,Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 
Kwa wajuzi wa historia ya Tanzania wameishajua kuwa Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) la kuhusu mkataba baina ya serikali ya Tanganyika AKA Tanzania na DP World ni kaa la moto mkali ambao unazidi kumchoma vikali muhusika mkuu na chama chake mpaka watakapokufa kisiasa mapema kama wataendelea kushupaza shingo.

Katika historia ya Tanzania hakuna mwanasiasa au Rais aliwahi kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) halafu akashinda. Haijawahi kutokea na haitawahi kutokea katika miaka hii ya karibuni. Kufanya hivyo ni kujiangamiza kisiasa(political suicide).

Unaweza kuukataa huu ukweli lakini kuukataa kwako hakuwezi kuubadilisha kuwa uongo.

Mwl. Nyerere pamoja na nguvu zote za kikatiba alizokuwa nazo katika utawala wake lakini hakuwahi kutumia nguvu katika kupitisha ajenda zake za kisiasa pale ambapo maaskofu walikuwa na shaka au kumpinga. Alitumia nguvu ya ushawishi wa hoja kwa kujadiliana nao mpaka wakamwelewa na kukubali.

Nguvu za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) zimeendelea hivyo katika tawala zote nchini. Hakuna mwanasiasa mwenye uelewa wa Tanzania na akili timamu aliweza kupuuza sauti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Muhusika mkuu wa mkataba wa DP World hakutegemea kama TEC wanaweza kutoa waraka mkali kama waliotoa kwa sababu sehemu ya 17 ya waraka imepigilia msumari wa mwisho wa jeneza la mkataba.

TEC IMEITAKA SERIKALI IACHANE NA MKATABA HUU.

Sehemu ya 17 ya waraka wa TEC inasema, “Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu”.

Baada ta waraka kutolewa, muhusika mkuu na genge lake akaanza kuhaha akitafuta jinsi ya kukabiliana nao. Amemtuma kiongozi mkuu wa nchi mstaafu ili ajibu hoja lakini hakufanikiwa kuzima moto, amejaribu kutumia mbinu za kidini kwa kuwatuma baadhi ya mashekhe ili wawajibu TEC katika misingi ya kidini lakini pamoja na juhudi zote, moto wa waraka wa TEC ndio unashika kasi ya kumchoma kisiasa. Ametuma “wajinga” fulani washambulie haiba ya maaskofu badala ya kujibu hoja hawajafanikiwa.

Alichofanya kwa sasa ni kuwatuma baadhi ya viongozi ndani ya serikali kwenda Dubai ili kuwaeleza wenye DP World kuhusu moto unavyowaka nchini ili waangalie namna ya kufanya ili kuondokana na moto mkali kisiasa ili kuepuka maafa ya kisiasa. Kwa hivi karibuni ndege ya Rais imekuwa na safari nyingi za kwenda Uarabuni na kurudi.

Katika hali hiyo ya kutapatapa ametangaza eti tenda ya kukaribisha wawekezaji kwenye bandari Terminal 2 ili ionekane hakutaka kugawa bandari zote kwa DP World wakati mkataba(IGA) unabainisha ni bandari zote na maziwa yote ya Tanganyika AKA Tanzania bara. Mjinga gani atakuja kuwekeza kwenye terminal 2 wakati kuna IGA inasema uwekezaji wowote katika bandari na maziwa nchini lazima kwanza uridhiwe na DP World.
Tumeona pia amemuondoa waziri wa katiba na sheria ili eti ionekane kama ndiye aliyesababisha hili sakata la DP World wakati kwenye IGA kuna saini ya Rais! Huku ni kutapatapa.

Kama isingekuwa waraka wa TEC, mchakato wa kuzifuta Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohousu Rasilimali na Maliasili za Nchi za mwaka 2017 ungefanyika bungeni na hili tangazo lingine la tenda ya kukaribisha wawekezaji lisingetolewa! Hii yote ni imefanyika katika hali ya kutapatapa baada ya tamko la TEC.
Unachonganisha kanisa na watu wasiolipenda ujue?! Sio sifa. Hii inapelekea vita vya chini kwa chini na watu kutengeneza agenda za kuwaangamiza. Stop this foolishness.
 
kuanza kupambana na TEC ni utoto mkubwa tec wana watu wengi kuliko taasisi nyingine yoyote, na wana mfumo wa kuwafikia watu wao kwa ufanisi mkubwa, ni kweli anayecheza karata vibaya na TEC, njia pekee atayobaki nayo ni kutumia jeshi la wezi wa kura.
 
Mkuu, ninachokiona katika hoja zako ni personal incredulity fallacy!

Yaani kwa fikra zako unadhani TEC kwa historia yake nchini wanaweza kupambania suala ambalo halina maslahi kwa taifa?

Nadhani wewe ndiye unayedhani hoja za TEC niza kidini.


Hapa sidhani Kama unamaanisha kutoka moyoni?!

Umeongea kisukari sana.


Siku zote inajulikana na wala sio Siri kwamba linapokuja suala la maslahi basi Kanisa Katoliki linasimamia maslahi ya kanisa lake kwanza kabla ya yeyote yule na chochote kile.

Kumbukumbu za Rwanda’s genocide na role waliyoplay RC ni mbichi bado.

Kumbukumbu za matukio ya Zanzibar Revolution in 1964 na juhudi zao katika hilo bado zipo barazani.

Huko DRC wala sitaki kupagusia.

Kanisa Katoliki ni jeshi kubwa sana, hilo halina upinzani na wakitaka jambo lao litimie kweli linatimia ila pia tukumbuke kuna history mbaya dhidi yao katika matukio mengi ya kusimamia maslahi ya yeyote na chochote.


Kama Papa Francis alivyosema alipotembelewa na Rais Kagame in 2017, Catholic Priests & Nuns are just mare humans and some will succumb to their own desires just because of their human nature.







Suala la Bandari za Tanzania, tuendelee kuwashukuru kwa kupunguza angalau speed ya huu mchakato wa uwekezaji ili tuzione picha halisi za pande zote kwa ukamilifu.


Nimesema wamepunguza speed ya huu mchakato wa ndoa kati ya Tanganyika na DP World maana sioni dalili za ‘Serikali’ ya Madam President Samia iki back down.

The current political geography & international hookups we are involved in simply makes it almost deadly to make any move, any! Kuinywa ya moto, Kuitema tamu.
 
Raisi Samia lazima awe makini na watu wanaomzunguka.
Wanamgombanisha na Watanganyika.
Hao wapigaji.

Wapigaji (Wanaume) kwa niaba ya Dr. Mongela.

Ila Raisi lazima atuombe radhi Watanganyika.
Tulisha uzwa kwa Waarabu
Mkuu, kwani Rais hajui kama "wanaomzunguka" wanangombanisha na Watanganyika?

Hii dhana ya kusema Rais "anapotoshwa" na washauri wake mnaitoa wapi? Kwa hiyo tukubaliane kuwa Rais hana uwezo wa kupambanua mambo ndio maana anakubali kupotoshwa!
 
Zitto ameanza Vita na TEC ya livelive
 
Back
Top Bottom