Hakuna mwanasiasa/Rais aliweza kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na akashinda!

Mungu - Yehova muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo katika Yesu Kristo mwokozi wa ulimwengu ukiwemo wewe. Soma👇👇

Yohana 3:16-18 SUV
"
...Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu..."

Kama huamini hayo☝️☝️ maneno hilo ni tatizo lako la kutoamini. Ila siku hiyo utakuja kushangaa kukumbushwa kuwa alitokea mtu kwenye mtandao mmoja wa kijamii uitwao Jamii Forum akakuambia habari zangu lakini hukuamini..

Hayo maneno matamu ila hayana ukweli.
Mfano wake ni kama mzee Suzuki kule Japan atengeze Suzuki aina tofauti nyingi sana, mwisho aamue mwanae mmoja amgeuze aina moja wapo ya gari za Suzuki, akaokoe suzuki mitaani?
Au mtengeza fenicha pale keko afanye maamuzi ya kumgeuza mwanae kochi la kukalia ili tu akaokoe fenicha majumbani.
Mungu ndio mueza wa kila jambo sasa inakuwaje tena ajigeuze kiumbe dhaifu alichokiumba mwenyewe.
Yakobo 1:17
Mungu habadiliki, kama kugeuka kwa kivuli.”
Malaki 3:6
Mimi ni Yehova; sikubadilika.”
Qurani: 18:4
"Further, that He may warn those (also) who say, "God" hath begotten a son".
18:15. No knowledge have they of such a thing, nor had their fathers. It is a grievous thing that issues from their mouths as a saying what they say is nothing but falsehood!
 
Magu, hadi pengo akawaruka wenzake hao TEC wanakua na mdomo mrefu rais akiwa muislam
 
Yule si kiongozi wa dini
kwahiyo akiharibu kiongozi mmoja wa dini wote wameharibu? shehe mmoja uarabuni akijilipua kwa bomu kwasababu yeye ni gaidi basi tuseme mashehe wote ni magaidi? ukiwa na mawazo hayo utakuwa umepotea sana. sweeping generalization huwa sio kitu sahihi.
 
Mkuu, Soma hii thread inadadavua vizuri uongozi wa Rais Samia;

GONGA hapo chini usome;
Kwa Rais huyu, CCM wana hali mbaya sana!

Hayo ni mawazo yaliyopo kichwani kwako tu,Samia kama MUNGU atamjalia afya na uhai,ataendelea kuwa raisi wa nchi hii mpaka hapo 2030,na maendeleo mengi makubwa atayafanya na kuiacha hii nchi ikiwa na maendeleo makubwa.
 
Heri yako kutabili yasiyotabirika maana kama kuna jambo Mwenyezi Mungu analichukia ni kutawaliwa na mtu asiye na maono ambaye mtazamo wake unategemea tu utegemezi ili kuendesha nchi yake.
 
Nimesema kama isingekuwa tamko la TEC kwa sasa bunge kingekuwa limeishafanya mchakato wa kuzifuta sheria za umiliki wa maliasili za mwaka 2017.
Hao Tec ni huko huko makanisani tu ndio wanaheshimika, huku mtaani hao ni waropokwaji tu kama wengine, wala watu hata wajui wamesemaje na serikali inaendelea namipango yake bila kujali Tec au yoyote yule.
 
Mkuu, kwani Rais hajui kama "wanaomzunguka" wanangombanisha na Watanganyika?

Hii dhana ya kusema Rais "anapotoshwa" na washauri wake mnaitoa wapi? Kwa hiyo tukubaliane kuwa Rais hana uwezo wa kupambanua mambo ndio maana anakubali kupotoshwa!

Wala hawamaanishi hivyo. Ni namna ya Watanzania kuwa very polite kwa kiti cha uRais. Hapo wanajaribu tu kumpa message yeye mwenyewe indirectly.
 
Ulisimuliwa au ulikuepo? Slaa lini aligombea urais na lini alionesha Nia ya kugombea urais,

Tupe evidence Moja au mbili TEC wakimdenouce JK, na utaje hao watu kutoka huko Galatia waliojounga na kanisa Kwa muktadha huo..
Na utuambie bila shaka familia ya JK iliyoingia kwenye kampeni na uwataje Kwa majina na roles zao. Vinginevyo wewe ni mwimba ngonjra.

TEC haijawahi na haitawahi kumfanyia mtu kampeni awe Rais awe mpagani au mwislamu au mkristo. Umeandika uwongo
2010 ulikuwa na umri gani dogo!
Usidandie dandie tu mazungumzo ya wakubwa, kaa pembeni usikilize utapata faida
 
Kwa wajuzi wa historia ya Tanzania wameishajua kuwa Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) la kuhusu mkataba baina ya serikali ya Tanganyika AKA Tanzania na DP World ni kaa la moto mkali ambao unazidi kumchoma vikali muhusika mkuu na chama chake mpaka watakapokufa kisiasa mapema kama wataendelea kushupaza shingo.

Katika historia ya Tanzania hakuna mwanasiasa au Rais aliwahi kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) halafu akashinda. Haijawahi kutokea na haitawahi kutokea katika miaka hii ya karibuni. Kufanya hivyo ni kujiangamiza kisiasa(political suicide).

Unaweza kuukataa huu ukweli lakini kuukataa kwako hakuwezi kuubadilisha kuwa uongo.

Mwl. Nyerere pamoja na nguvu zote za kikatiba alizokuwa nazo katika utawala wake lakini hakuwahi kutumia nguvu katika kupitisha ajenda zake za kisiasa pale ambapo maaskofu walikuwa na shaka au kumpinga. Alitumia nguvu ya ushawishi wa hoja kwa kujadiliana nao mpaka wakamwelewa na kukubali.

Nguvu za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) zimeendelea hivyo katika tawala zote nchini. Hakuna mwanasiasa mwenye uelewa wa Tanzania na akili timamu aliweza kupuuza sauti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Muhusika mkuu wa mkataba wa DP World hakutegemea kama TEC wanaweza kutoa waraka mkali kama waliotoa kwa sababu sehemu ya 17 ya waraka imepigilia msumari wa mwisho wa jeneza la mkataba.

TEC IMEITAKA SERIKALI IACHANE NA MKATABA HUU.

Sehemu ya 17 ya waraka wa TEC inasema, “Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu”.

Baada ta waraka kutolewa, muhusika mkuu na genge lake akaanza kuhaha akitafuta jinsi ya kukabiliana nao. Amemtuma kiongozi mkuu wa nchi mstaafu ili ajibu hoja lakini hakufanikiwa kuzima moto, amejaribu kutumia mbinu za kidini kwa kuwatuma baadhi ya mashekhe ili wawajibu TEC katika misingi ya kidini lakini pamoja na juhudi zote, moto wa waraka wa TEC ndio unashika kasi ya kumchoma kisiasa. Ametuma “wajinga” fulani washambulie haiba ya maaskofu badala ya kujibu hoja hawajafanikiwa.

Alichofanya kwa sasa ni kuwatuma baadhi ya viongozi ndani ya serikali kwenda Dubai ili kuwaeleza wenye DP World kuhusu moto unavyowaka nchini ili waangalie namna ya kufanya ili kuondokana na moto mkali kisiasa ili kuepuka maafa ya kisiasa. Kwa hivi karibuni ndege ya Rais imekuwa na safari nyingi za kwenda Uarabuni na kurudi.

Katika hali hiyo ya kutapatapa ametangaza eti tenda ya kukaribisha wawekezaji kwenye bandari Terminal 2 ili ionekane hakutaka kugawa bandari zote kwa DP World wakati mkataba(IGA) unabainisha ni bandari zote na maziwa yote ya Tanganyika AKA Tanzania bara. Mjinga gani atakuja kuwekeza kwenye terminal 2 wakati kuna IGA inasema uwekezaji wowote katika bandari na maziwa nchini lazima kwanza uridhiwe na DP World.
Tumeona pia amemuondoa waziri wa katiba na sheria ili eti ionekane kama ndiye aliyesababisha hili sakata la DP World wakati kwenye IGA kuna saini ya Rais! Huku ni kutapatapa.

Kama isingekuwa waraka wa TEC, mchakato wa kuzifuta Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohousu Rasilimali na Maliasili za Nchi za mwaka 2017 ungefanyika bungeni na hili tangazo lingine la tenda ya kukaribisha wawekezaji lisingetolewa! Hii yote ni imefanyika katika hali ya kutapatapa baada ya tamko la TEC.
Ccm mna laana
 
Kwani TEC inashindana na Rais/Wanasiasa?
 
Back
Top Bottom