Hakuna nchi yenye uthubutu Dunia hii kama Iran. Wanajivunia nini?

Na utashangaa zaidi Israel ikifutwa kabisa kule mashariki ya kati
 
So far ni hamas wangapi wameuwawa mpaka sasa?
Issu ni kwamba hamas still wapo na wameendelea kujiimarisha na hata waziri wa vita gallant amegombana na kumpinga netanyahu hadharani na kumwita muongo, kwa sababu netanyahu anaaminisha watu kwamba watawamaliza hamas, huku gallant akisema huwezi kumaliza vikundi kama hamas its impossible na kumtuhumu netanyahu kudanganya waisrael
 
Ishu si kuwapo ni operation capacity, unaweza kuwa na rundo for nothing, or opsec ikawa chini sana kuliko kawaida
 
Ndio utashangaa mwenyewe sasa hiyo Israel inayopewa misaada lukuki na nchi zote za west pamoja na kuwa na jeshi lenye vifaa vya kisasa kabisa ila sasa mbona anaishindwa hata Hamas ambayo haina hata kifaru kimoja?

Hili jambo linawaudhi sana USA and allies na wanaona kabisa kuwa misaada yao haitumiki vizuri au Israel ni taifa dhoofu sana mpaka kuepelekeshwa na Hamas? Ukiondoa mabomu yanayopigwa kwa kutumia ndege vita basi Israel isingeweza kufanya chochote hata kule Gaza.

Hao Iran, hata western countries hawaamini macho yao kwa hizo developments zao na hao ndio watakaoisambaratisha Israel ikafia kimoja kabisa.

Cha kujifunza ni kwamba anayepanga maisha ni Mwenyezi Mungu tu sio USA wala sio UN. Na pia ni commitment na jitihada yenu kama nchi husika. Yani nchi yeyote inaweza kusurvive bila mafungamano na West na ikawa imara.

kwa kifupi Western powers and threat is a dead myth. Na hapa sio Iran tu hata North Korea na Russia wanasurvive bila west.
 
Ishu si kuwapo ni operation capacity, unaweza kuwa na rundo for nothing, or opsec ikawa chini sana kuliko kawaida
Huwa najitahidi sana kufuatili dunia kutoka kwa wataalamu wa mambo haya , hizo hapo analysis za experts, kwa zaidi ya mwaka sasa hamas wanaendelea kupigana na kushambulia huku wakiwa na silaha hafifu
 

Attachments

  • Screenshot_20241009-124743_Chrome.jpg
    402.8 KB · Views: 2
  • Screenshot_20241009-124604_Chrome.jpg
    410.5 KB · Views: 3
Ili kutambua maendeleo ya Iran huna budi kutabahari ktk maisha ya Muanzilishi wa mapinduzi ya Iran Ayatollah Imam Khomein
Alifanya Mapinduzi akiwa France, hakutumia nguvu saana ila alitumia Imani + akili + Maarifa Makubwa

Akiwa Paris aliishi maisha ya chini sana kiasi kwamba ilikuwa ni muhali kutomfikiria kama ana matatizo ya akili. Mara nyingi Makachero wa Kifaransa walipokuwa wakidukuwa chumba chake kulikuwa hakuna cha maana zaidi ya vitabu na mazulia ya kusalia
Wafaransa haikuwajia akilini mwao kama taahira kama yule angeweza kudiriki hata kufikiria kufanya mapinduzi kama Yale

Aliwekeza sana kwa Wanawake na watoto. Siku moja wakati wa utawala Mfalme Shah wa Iran kulikuwa na kusanyiko la kitaifa kama vile sherehe za Uhuru, Imam Khomein alikuwapo uwanjani. Baadhi ya wasaidizi wa Shah wakamuuliza unamjua Khomein anayeleta chokochoko akawaambia niitieni. Akiitwa akaulizwa "nasikia wewe ndio unaeleta chokochoko, eti unataka kunipindua" ?
Imam Khomein akamjibu akawaambia "Mimi natayarisha watu ambao hivi sasa wako viunoni mwa wazazi wao- hao ndio wataokuja kukupindua" Na kweli maneno yake yakasadifu baada ya miongo kadhaa

Kadhia hiyo hapo juu pia inatupa funzo kwamba Imam alikuwa anajua anataka Nini ?
Atatumia rasilimali gani kufikia malengo yake ?
 
Iran wamefanikiwa tu baada ya kujua kuwa ulinzi na maendeleo ya nchi ni jukumu la Wairan, hakuna atakae kuja kukusaidia kila nchi ina changamoto zake, akaamua kuwekeza kwa wasomi wake ndio haya matokeo mnaona leo ana makombora ya kutosha na Drone za kutosha kuweza kumuachia adui maumivu makali, ana jeshi kamili la watu zaidi ya laki tano (500,000), kiufupi kupigana na Iran lazima utoke unachechemea hata kama umeshinda
 
Yule ndio Imam sasa, sio hawa maimamu wetu wa ccm
 
Israel ni simba wa kwenye makaratasi mkuu, jaribu kufikiria mpaka sasa wameshindwa kukomboa mateka wao na Hammas anaendelea kushambulia ndani ya tel aviv.
Hivi sometimes majenerali wa JF mnachekesha kweli.

Hao Hamas wanajeshi linalopigana uso kwa uso na Israel IDF au wanavizia kwa makombora na uvamizi wa kushtukiza wa silaha wakitokea katikati ya jamii au raia.

Mnataka Israel iangamize raia wote wa Gaza ndio mseme Israel kidume?

Sasa hv tu wamekufa watu zaidi ya 40,000 wanalalamika free Gaza. Vipi wakiuliwa wote?

Hao wanamgambo wanajificha kwa raia nao unaweza waita wapiganaji au waviziaji.

Marekani alishindwa Somalia sababu hiyo vinginevyo angeua raia wote
 
Kwa vile ameshindwa imeisha hiyo.
 
Urussi ipo nyuma ya muiran ...muiran ni mjanja sana alisukuma kete yake vizuri alipo msaidia mrussi alijua faida yake nini ....marekani hajawai kuishinda nchi yoyote ambayo mrussi yupo nyuma yake ..kumbuka kuwa Israel inamtegemea mmarekani ...hspo ndipo kiburi chamuiran kkilipo tokea
 
Kitu kingine mnacho sahau wengi wenu ni kuhusu vita kati ya iran na iraq kama Iran iliweza kupambana na sadamu miaka mingi na USA NA NATO WALITUMIA NGUVU KUBWA KUPIGANA NA SADAM PEKE YAKE BASI MJUE IRAN YA SASA NI IMARA MARA 20 YA IRAQ YA SADAM
 
Israel ni simba wa kwenye makaratasi mkuu, jaribu kufikiria mpaka sasa wameshindwa kukomboa mateka wao na Hammas anaendelea kushambulia ndani ya tel aviv.
Hamas lini wameingia Tel Aviv kama watz walivyoingia Kampala Uganda,!!!!!!
wanarusha marocket wakiwa wamevaa hijabu na wamejificha hospitali, mashimoni na mashuleni. Israel ikiamua kama Mrusi alivyoifumua Chechnya siku moja tu anaua wapalestina wote na mateka wote wafe, kazi iishe ila anafuata sheria za vita. Ubingwa ktk vita ni uwezo wa kuingia ktk himaya ya adui yako na adui wako KUKIMBIA NA KUJIFICHA mwaka mzima. hao ndiyo simba wenyewe
 
Kuna Siri kubwa, nyuma ya Ayatoli na marekani juu ya mafuta na Israel na marekani..
 
Hamas wakowapi mpaka sasa?
Hamas wamekimbia kwa uwoga na kujificha mashimoni kama panya na mahospitalini, mashuleni na maeneo ya raia wakitoka wanavaa hijab za wanawake kwa kuwaogopa Waisrael walioingia Gaza mwaka mmoja sasa.
 
Hapo ghaza walipo sema wamapasafisha hakuna yeyote ndipo maroketi yanapotokea.

sijui hata unaongea nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…