Uchaguzi 2020 Hakuna pingamizi atawekewa mgombea wa CHADEMA

Uchaguzi 2020 Hakuna pingamizi atawekewa mgombea wa CHADEMA

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Zile saa nane ama yale masaa manane jana ya tar 25. August. 2020 ya kumsubirisha mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA kuanzia saa sita mchana mpaka jioni ya saa moja na dk 40 yalikuwa ni faida tupu kwakwe.

Trust me wale wagombea wengine waliopewa kipaumbele na kuharibu ratiba wakaingia fasta wakapokelewa na kupitishwa haraka wamefanya makosa mengi ya kisheria na hili litawagharimu pakubwa.

Mgombea wa CHADEMA ndie pekee kazunguka mikoa 16 katika uhalisia wake kutafuta wadhamini...hii imempa credit kubwa sana..ni awali njema..awali iliyokosa mawaa wananchi katika uhalisia wao na kwa furaha bila shuruti wakamdhamini kwa mikono yao na vidole vyao wenyewe..hii kiroho ni hali chanya yenye uhai.

Wagombea wengine wamepata wadhamini kupitia daftari la kupigia kura(pengine kupitia tume ya uchaguzi) yamenyofolewa majina wakajaziwa...akidi ikatimia tume ikapitisha kwa mtazamo wa haraka unaweza kudhani hakuna shida...! Lakini kiroho kuna shida kubwa sana.

Udhamini wa hawa wagombea wengine ni mfu hauna uhai kwakuwa mgombea hajakutana ana kwa ana na hao anaotaka wamdhamini. Udhamini wa hawa hauna msingi chanya kwakuwa baadhi ya hayo majina kuna marehemu ndani yake. kuna wengine hawampendi tena mgombea..kuna wengine wameshahama vyama nknk. Nina hakika hata wengine number zao za simu hazipatikani tena ama wao wenyewe hawajulikana walipo. Kwahiyo hapa tunaona wazi kabisa hakuna muunganiko wa kiroho na hata kimwili kati ya mdhamini na mdhaminiwa

Ukiachana na hayo upangaji wa mipango na ratiba ya kuomba udhamini kwa CHADEMA vilikuwa vizuri na vya viwango vinavyotakikana na tume ya uchaguzi na kwa sheria za uchaguzi..namna watu walivyojikusanya na kukusanyika..vibe chanya waliyokuwa nayo..zoezi zima la udhamini lilivyoenda nknk..ukiachana na delayments zisizozuilika zoezi zima la kutafuta wadhamini lilikuwa perfect..Hili limekishape chama na kukiongezea credit kubwa!

Uwezo na matumizi ya fedha...kwenye hili tena CHADEMA wamepiga bao lingine la haja..Jamani inahitajika mipango kabambe na fungu la kutosha kuweza kuzunguka mikoa 16 na mfasara wa watu wasiopungua 20 na wote hao wapate chakula malazi nk na magari yapate mafuta nk

Udhamini wa kimyakimya ni udhamini wa kificho na uliojaa makandokando mengi hata kijamii pia ukiachana na kisheria..hauleti tumaini na hisia za umoja na kuwa wamoja kati ya mdhamini na mdhaminiwa.

Tuna masaa chini ya 15 kwa ajili ya kuwekeana mapingamizi ni masaa machache lakini yaliyobeba simulizi nyingi...wewe wakati uko kitandani mwako umelala kuna watu hawajalala wala kupumzika wako busy kuhakikisha wanaruka na kukwepa vizingiti na hila zote za pingamizi.
 
Majimbo aliyozunguka Lisu kutafuta wadhamini Ni 20 CCM tayari imeshachukua majimbo 22 ambayo wabunge wa CCM wanepita bila kupingwa

Hapo unaweza kuona kuwa ziara zake Ni hopeless sababu Hadi Sasa Hana mbunge kote alikozunguka
 
Hivi huwa ukiandika unafikiri kweli au unaandika tu almradi uonekane umeandika!?
 
Tundu ni mtu wa pekee sana, ana utofauti na hao wengine wagombea, sikuwahi sikia hata mkuu wa nchi kuzunguka kutafuta saini mbali na pale alipopokea lile gimbi. Hivi hakujua mtaani au kijijini mtu mpaka ufuge gimbi lifikie pale linakuwa limebeba maroho yote, hili mtani utalijua kiroho.

Gimbi linaona watu wakizaliwa, wakiroga, wakitambika, wakifa, limeshughudia misiba limesikia watu wakisema na linaongea na ardhi, leo hii mkuu top leader unalishika kwenye kadamnasi, haikuwa nzuri.

Mwalimu Nyerere alipokuwa anapewa zawadi walikuwa wanampokelea. Na akitoka hapo anaenda kwa kiongozi wa mila kusema naye.

Anyways hayatuhusu,

Ya Lissu leo ni makubwa, ni nini kimewalazimisha kushezesha orodha? Suala la kiroho sana hilo.

Je hao wagombea wengine waliopitishwa tu yaani bora liende si ni lazima watakuwa bora liende, tutaona.

Ni nini kilikusudiwa kimtokee, mpaka ikafika tunaona namba za magari kuwa yanamngoja nje tukasikia mengi mengi vile.

Mwisho nguvu zao zikamezwa, Ikawa kimyaaa.

Sitaki kumalizia kuandika kitu ambacho kilishaandikwa, ardhi ni shahidi. We will see.

Mshana Jr hulali ?
 
Mimi binafsi moyo wangu umetulia, Jana mapigo ya moyo yalikuwa juu nikiwazia Nani tofauti na Lisu ataikomboa hii nchi kutoka kwa mkoloni CCM.

Mapingamizi yoyote ya Lisu Ni takataka tu, mwenye akili hawawezi kufanya hivyo maana Ni kujidhalilisha mbele ya uma wa Watanzania
 
Tundu ni mtu wa pekee sana, ana utofauti na hao wengine wagombea, sikuwahi sikia hata mkuu wa nchi kuzunguka kutafuta saini mbali na pale alipopokea lile gimbi. Hivi hakujua mtaani au kijijini mtu mpaka ufuge gimbi lifikie pale linakuwa limebeba maroho yote, hili mtani utalijua kiroho.

Gimbi linaona watu wakizaliwa, wakiroga, wakitambika, wakifa, limeshughudia misiba limesikia watu wakisema na linaongea na ardhi, leo hii mkuu top leader unalishika kwenye kadamnasi, haikuwa nzuri.

Mwalimu Nyerere alipokuwa anapewa zawadi walikuwa wanampokelea. Na akitoka hapo anaenda kwa kiongozi wa mila kusema naye.

Anyways hayatuhusu,

Ya Lissu leo ni makubwa, ni nini kimewalazimisha kushezesha orodha? Suala la kiroho sana hilo.

Je hao wagombea wengine waliopitishwa tu yaani bora liende si ni lazima watakuwa bora liende, tutaona.

Ni nini kilikusudiwa kimtokee, mpaka ikafika tunaona namba za magari kuwa yanamngoja nje tukasikia mengi mengi vile.

Mwisho nguvu zao zikamezwa, Ikawa kimyaaa.

Sitaki kumalizia kuandika kitu ambacho kilishaandikwa, ardhi ni shahidi. We will see.

Mshana Jr hulali ?
Gimbi linaona watu wakizaliwa, wakiroga, wakitambika, wakifa, limeshughudia misiba limesikia watu wakisema na linaongea na ardhi, leo hii mkuu top leader unalishika kwenye kadamnasi, haikuwa nzuri.

Mwalimu Nyerere alipokuwa anapewa zawadi walikuwa wanampokelea. Na akitoka hapo anaenda kwa kiongozi wa mila kusema naye[emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji1534][emoji1548][emoji1534]
Mtani niko zamu..lakini leo mochwati kumepooza mno
 
Lissu nimpango wa Mungu na lazima yuko na backup kubwa nyuma yake ambayo haiyonekani kwa macho.
Mimi binafsi moyo wangu umetulia, Jana mapigo ya moyo yalikuwa juu nikiwazia Nani tofauti na Lisu ataikomboa hii nchi kutoka kwa mkoloni ccm. Mapingamizi yoyote ya Lisu Ni takataka tu, mwenye akili hawawezi kufanya hivyo maana Ni kujidhalilisha mbele ya uma wa Watanzania
Mashaka shemeji yangu, TAL ni game changer of the year. The guy is gifted
JamiiForums21093436.jpg
 
Umeandika vema, well articulated.
1. Inahitajika timu ya watu tangu jana alipoitishwa kupitia jina kwa jina na kupiga smu kuhakiki kama hao bado wanaishi.. unawapigia simu wote kuona atakaye pokea au ambazo hazitapokelewa zitakuwa ngapi. Ukipata 10% hzijapokelewa, then unaweka pingamizi

2. Wanasheria kupitia fomu za waliopitishwa kuzihakiki.. kutafuta dosari kama zipo....sijui taratibu huwa zinakuwaje , unapewa kila kopi ya aliyepitishwa?

LAKINI: Mshana jr was it deliberate kutohakikiwa mikoani au walikuwa hawajui? Kama walikuwa hawajui, that is a grave mistake to recorn!
 
LAKINI: Mshana jr was it deliberate kutohakikiwa mikoani au walikuwa hawajui? Kama walikuwa hawajui, that is a grave mistake to recorn! Why CHADEMA ONLY !? It might be a grave mistake 'as well' but trust me we will get EVEN to it..!!!
 
Mimi binafsi moyo wangu umetulia, Jana mapigo ya moyo yalikuwa juu nikiwazia Nani tofauti na Lisu ataikomboa hii nchi kutoka kwa mkoloni ccm. Mapingamizi yoyote ya Lisu Ni takataka tu, mwenye akili hawawezi kufanya hivyo maana Ni kujidhalilisha mbele ya uma wa Watanzania

Kama mimi. Alhamdulillah [emoji120]
 
Chadema wajipange na kampeni tu sasa. And vile vile waweke pingamizi kwa hawa waliopita bila kupingwa.
Aibu hata enzi ya chama kimoja Nyerere alikuwa anashindanishwa na kivuli chake ndiyo inapatikana hiyo % sasa leo wajumbe 150 ndiyo wanatupa Mbunge Aibu Sheet hole kweli kweli halafu tunasema tuna wasomi karne hii vitu vya ajabu hapo hata helkopta ya mabua hatuwezi tengeneza
 
Back
Top Bottom