Hakuna record label ninayoweza kukubali inisainishe, watanipa nini ambacho sijafanya! – Diamond

Hakuna record label ninayoweza kukubali inisainishe, watanipa nini ambacho sijafanya! – Diamond

Sawa mkuu sijakataa swala la capital na network ni zuri kwa kila mfanya biashara.Ila unaamini kuwa kwa mafanikio ya Diamond anamzidi Nick Minaj au P Didy???
Hayo ni mambo ya kitoto kuponda mafanikio ya wengine so haoni kuwa wale waliochini yake pia wanajihisi inferiority kwa hizo kauli zake.
Mkuu wale ni tofauti mikataba yao wanayoingia wanalipwa pesa kubwa tofauti na uku kwetu.Ali Kiba kasaini Sony lakini ajaweka wazi ni kiasi gani kalipwa kwasababu ni aibu.
 
Wasanii wa mbelez ni tofauti kabisa na Afrika.. Hizi management zinawafaidisha zaidi wasanii wakubwa compared to wadogo, chukulia mfano tu;- Adele amesaini Sony amelipwa dola milioni 90 (kibongo ni zaidi ya BILIONI 180) huku mwenzetu Alikiba amelipwa mil 100... Hii ni kutokana na industry ya mziki wao ulivyoendelea unamambo mengi ndio maana ni muhimu uwe na watu kama hawa..

Chukua mfano Davido amesaini Sony tokea January mwaka huu, Je mpaka leo hii nusu mwaka huu kuna kitu gani kipya amefanya ambacho hakufanikisha miaka ya nyuma zaidi ya ukimya tu huku Wizkid akijipakulia minyama, hata nomination ya BET kakosa mwaka wa pili mfululizo....

Uje tena upande wa Dbanj baada ya kuwa chini ya Kanye alifanya lipi la maana zaidi ya kujichimbia kaburi mazima mpaka leo?
 
kuna uhusiano wa moja kwa moja wa uswahili na utandale yeye ni nani mbona wakina chris brown lil wayne kanye jay z nk wapo chini ya record lebel yan huyu ni ili mradi tu aonekane hamkubali kiba ila akubali akatae ishamuingia haina namna atulie na kiki zake #aje
Anafanya kila kitu ili deal la kiba ionekane KA bug mtu anakubal tangazo la tomato akatae deal la Sony inaamaana davido Hana pesa za video au promotion maana nikisema Chris natania
Wivu utawauwa pumbavu
 
kuna uhusiano wa moja kwa moja wa uswahili na utandale yeye ni nani mbona wakina chris brown lil wayne kanye jay z nk wapo chini ya record lebel yan huyu ni ili mradi tu aonekane hamkubali kiba ila akubali akatae ishamuingia haina namna atulie na kiki zake #aje
Sasa huko ni kufananisha chungwa na embe, yote matunda lkn ladha na mwonekano tofauti
 
Dogo na lebo ya kumsaini harmonise toka Ntwara anataka kuleta nyodo. by the way kajitahidi alipofikia aongeze bidii sio mara jii kama Hasheem Thabeet maana mchawi wetu sisi katangulia.
 
kuna kitu kimoja mnatakiwa kukifahamu kuhusu alichosema diamond sio kuanza kumlinganisha sijui na kina nani.....

hao kina michael jackson mnaowataja maisha yao yote wamekuwa under label, kuanzia motown hadi sony ila diamond ameanza muziki akiwa chini ya managers tu bila kuwa na label yoyote na amefanikiwa kutengeneza label yake WCB ambayo kwa hapa afrika inafanya vizuri sana, sasa kwanini aiache label yake ambayo kimsingi ni biashara yake aende kwenye label nyingine wakati yeye anategemea kusign wasanii wengine label iwe kubwa na atengeneze pesa zaidi..

kuna majukumu mengi sana ya kimkataba kwa msanii na makato kibao ya mkwanja pindi msanii anapokuwa chini ya kampuni fulani, sasa kwanini yeye aende akaongeze mzunguko wa pesa zake kuliwa wakati anamiliki label yake ambayo itamlipa vizuri zaidi

Anachokifanya diamond sio kipya katika biashara ya muziki, mtu kama jay z baada ya kutengeneza mkwanja na connection akaunda label yake ya Roc nation na inafanya vizuri tu, unapoona rihanna anatamba ujue account ya jay z inazidi kutuna maana rihanna ni biashara ya jay z, vivyo hivyo dimond ni msanii A list hapa africa... tuseme tu ukweli ni label gani atasaini ambayo itampush zaidi ya hapo kwenye muziki huu wa afrika, zaidi kumuongezea stress na majukumu kibao ya kimkataba ambayo anaweza kuyaepuka kwa kuendelea kulamba hela taratibu huku akikuza label yake ya WCB.
 
Anafanya kila kitu ili deal la kiba ionekane KA bug mtu anakubal tangazo la tomato akatae deal la Sony inaamaana davido Hana pesa za video au promotion maana nikisema Chris natania
Wivu utawauwa pumbavu

1. Diamond alishawahi kuongelea kutozikubali label hata kabla ya kiba hajasainiwa na sony, kipindi wanatambulisha bado ya harmonize... Kwahiyo Kiba hahusiki kwenye huu uzi labda kama unataka kumsafishia nyota akiki maana kila anachofanya chibu Mara ooh anataka kuzima aje, yote haya ni INSECURITY na KUTOKUJIAMINI

2. Deal la uongozi ni tofauti na deal la utangazaji bidhaa. Kama hufahamu nikutoe tongotongo, deal la redgold la diamond ni sawa na deal la upishi na vyakula la alikiba utofauti tu ni kwamba alikiba ni balozi wa kujitolea bila malipo wakati diamond analipwa

3. Kila msanii anamlengo wake, kwahiyo Davido kuingia aliingia na malengo yake japokuwa ameingia chaka.. Tokea januari amejiunganayo mpaka leo (nusu mwaka) hana jipya alilopata huko Sony aisumbue Afrika zaidi ya kushughulikia wasanii anaowasaini kwenye label yake DMW.
 
Diamond aseme tu hayuko tayari kuwa chini lebel sababu ana label yake ya WCB na sio kujisifu kijinga kuwa hakuna lebel ambayo itaweza kumsimamia yeye
 
Good move Diamond, issue ya big names kuwa chini ya label haiwezi kusababisha mtu asifuate utashi wake, huwezi kunishawishi kuwa bila kuwa chini ya label kubwa msanii hawezi fanikiwa kimataifa. Btw kipaji ni cha kwake kwnn asifanye anachokiona ni sahihi kwake
 
humu ndo tutajua watu wenye akili na vilaza,mjadala uendelee....
 
Kweli nimeamini maskini akipata matako hulia mbwata
 
Kweli lakini, ila hata hao ma top wenyewe wanasainishwa tuu, inategemea ni nini unataka, diamond hajafikia na sijui kama atafikia hiyo level(namuombea afikie huko)level ya kufanyiwa fitna na record labels za kimataifa akifikia huko atasaini tuu pamoja na hao madogo wake machoko, tena watasaini kama package hadi fela, tale na salam, drake yuko under record label awe diamond bana, bado ni our African best musician ila akienda kidunia(global) atabadilika
 
Hili sio tatizo la Diamond pekee. Ni tatizo la Watanzania wengi wenye mafanikio kuhusu management ya mambo yao. Utakuta mtu ana hiteli 3 kubwa tu, maduka 5 makubwa, malori 10 hata zaidi lakini yeye ndiye mkurugenzi, meneja, mhasibu, asifa utumishi n.k. Bila yeye kuarifiwa hakuna kitu kitasogea hata kama yuko nje ya nchi. Hata zikihitajika shs 5,000 za dharura mpaka apigiwe simu. Ndio anachokifanya Diamond sasa, anaamini yeye ndie kila kitu, mchezaji, mwaimbaji, mtungaji, mwongozaji, msaini mikataba n.k. Ni tabia tu tunatakiwa kubadilika.
Zamani makampuni ya magazeti yaliwaweka waandishi kuwa wakurugenzi wakuu, sasa mambo yamebadilika wakurugenzi wakuu kwenye makampuni ya habari ni watu waliobobea kwenye menejimenti na masoko na wanafanikiwa.
 
Hoja ya msingi labda aseme hajapata offer nzuri lakini sio kwamba label za nje hazina kipya kwake. Hivi upate offer nzuri kwa Def Jam, Dre au shady utakataa? Tatizo labda ni kuwa offer za wasanii wetu wa Africa zinakuwa poor, Unaweza kuwekwa foleni hata miezi 8 bila kutoa kazi.
 
Kweli lakini, ila hata hao ma top wenyewe wanasainishwa tuu, inategemea ni nini unataka, diamond hajafikia na sijui kama atafikia hiyo level(namuombea afikie huko)level ya kufanyiwa fitna na record labels za kimataifa akifikia huko atasaini tuu pamoja na hao madogo wake machoko, tena watasaini kama package hadi fela, tale na salam, drake yuko under record label awe diamond bana, bado ni our African best musician ila akienda kidunia(global) atabadilika
Hongera, unakipaji cha chuki unastahili kuajiliwa kama mnyongaji.
 
  • Thanks
Reactions: ora
Back
Top Bottom