Mleta maada, aliyekwambia ni lazima kila nchi iwe na hiyo demokrasia ni nani? Kila jamii yapaswa kuishi vile inavyotaka yenyewe. Na hata pale inapoamua kuwa na demokrasia sharti jamii yenyewe ndiyo iamue aina ya demokrasia inayotaka. Kuna kiwango cha demokrasia nchi yoyote ile ikifikia kunakuwa hapana watu wala utu tena. Linakuwa taifa la wendawazimu.
Ukitaka kunielewa tembelea ukurasa wa twitter wa Trump halafu pitia mijadala ya wamarekani. Tazama mitazamo yao, lugha wanazotumia, kiwango cha heshima/staha, na kisha jiulize ikiwa ni watu au wendawazimu wanajadiliana.
Kwa kifupi demokrasia iliyokubuhu au ulibelali ni kitu cha mwisho nchi yetu itaamua kufanya. Ni afadhali kuwa na viashiria vyote vya maendeleo (demokrasia ni kiashiria kimoja tu cha maendeleo: tena kwa mujibu wa ubepari) isipokuwa hiyo demokrasia kuliko kuwa na demokrasia na kisha kuishi kitaahira kama nchi moja hivi tunayopakana nayo.